Dada Juliana Shonza, haya ni ya kweli?

Dada Juliana Shonza, haya ni ya kweli?

Status
Not open for further replies.

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
Wana-JF!

Katika pekua pekua zangu, nimekuta taarifa isemayo kuwa, dada Juliana Shonza alihakikishiwa ubunge wa viti maalumu kama angekosa fursa ya kugombea jimboni katika majimbo ya uchaguzi.

Kuhakikishiwa huko kulifuatia kukubali kwake kushiriki katika kukinadi CCM na kueleza mabaya ya CHADEMA kwenye majukwaa katika harakati zake za kisiasa.

Ila ndoto zake hizo za ubunge wa viti maalumu ziko njia panda, kwani mapendekezo ya awali ya rasimu ya katiba yana eleza kuwa;

"hakuta kuwa na viti maalumu isipokuwa kwa makundi maalumu tu kwenye jamii", na mimi nijuavyo dada Shonza wewe sio kundi maalumu.

Dada Shonza, taarifa hii imetapakaa tayari, jambo la msingi ni kuitolea ufafanuzi taarifa hii ili uweze kusafisha hali hii ya sintofahamu kwa wana-CCM na jamii kwa ujumla.
 
Na alivyojiharibia kwa kusema ccm imejaa mafisadi ndo kabisa tutamsahau
 
Usimkatishe tama dada yetu viti maalumu bado vitakuwepo kwenye Bunge la Tanganyika.
 
Kawa dada leo? hahahahahahaaaaaahaha
 
Kuahidiwa NDIZI huku MGOMBA unafyekwa!

Ila wewe jamaa yangu Safari ni Safari uwaga unanifuraisha sana na hii misemo yako. Hii hapa inamaanisha nini Mkuu: Zogolo Dangu Dawika Miye! Kitakuwa kilugulu cha Matombo hiki. Au? Ameahidiwa Ndizi eti? ha ha ha
 
Anaandaa sahani wakati ugali umemwagiwa maji na Warioba. Kwanza na Mwigulu mwenyewe ubunge atausikia TBC. Singida wakitakiwa kutoa mbunge mmoja tunazungumzia mpambano unaomhusisha mbunge wa Taifa Lissu. Sasa kufikiria Mwigulu kwenye mazingira kama hayo ka.
 
Mkuu, Kabla ya kufikia uamuzi wa kumtaka aje kukanusha ungejenga hoja mbadala kwanza ya PROCESS ambayo CCM walikuwa wanaitumia kuwapata wabunge wa viti maalum na kama ungepata upenyo wa shimo linalotumika kufanya kile ambacho unadai Juliana Shonza aliahidiwa, ndiyo ungekuja na hoja ya kumtaka akanushe.

PROCESS ambazo CCM ilikuwa inazitumia katika kuwapata wabunge wa viti maalum ziko wazi na siyo kama baadhi ya vyama vingine ambavyo wabunge wake wa viti maalum walipatikana kwa njia ambazo ni viongozi wachache wanazijua.

Hata nafasi ambazo Rais alitakiwa kikatiba kuzitoa kwa watu anaopenda bila kuulizwa sababu yake, Rais alizitoa kwa uangalifu mkubwa kwa watu ambao kila mwenye akili pevu alijua sababu za msingi za kufanya hivyo kwa maslahi ya Taifa.

Hoja yako inakosa nguvu kwa vile msingi wa hoja hauko.

Anyway, hili ni juu ya Juliana Shonza kulitolea ufafanuzi kama atapenda pamoja na kwamba hakuna basis za kufanya hivyo.
 
Rais wako alimpaje ubunge Vicky Kamata? Unazijua sababu?
 
CCM ni kwa nia ya ulaji tu!! Mi namtakia kila la kheri dada shonza!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom