Dada aliyemuua jambazi katika harakati za kumuokoa mume wake: Sheria imekaaje? Je, ana kesi yoyote ya kujibu?

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Sheria zetu zinasemaje juu ya hili?

======

MWANAMKE ALIYEPIGANA NA JAMBAZI MWENYE BASTOLA NA KUFANIKIWA KUMUUA

Mke wa Mfanyabishara Castola Mnoge, Juliana Damiani, mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma, amesimulia jinsi alivyopata ujasiri wa kumpiga na gongo jambazi na baadaye kushika jiwe kupambana na majambazi wengine ambao walivamia nyumbani kwao usiku kwa lengo la kuwaibia fedha.

Tukio hilo la kutisha limetokea hivi karibuni saa chache mara baada ya mumewe kuwasili nyumbani akitokea kwenye biashara yake ya Mpesa akiwa na mauzo ya siku ndipo alipofanikiwa kumpiga na gongo kisha kupata msaada wa majirani wenye hasira kali ambao walimshambulia zaidi hadi kumuua huku majambazi wenzake wakifanikiwa kutoroka.

Chanzo: Global TV
 
hapo kuna self defence, defence of property na defence of a person. lakini hadi hiyo ifanyike jalada linatakiwa kufanyika committal liende High Court (ambayo ndio mahakama inayoshughulikia mauaji) na yeye akiri kosa kwamba ni kweli aliua lakini alikuwa anatetea mumewe, yeye mwenyewe na mali zao. atakuwa acquitted.
 
Yeye hajaua alimdhibiti jambazi, ila wananchi wenye hasira kali walijichukulia sheria kali mikononi mwao.
 
Ukimuua jambazi mwenye silaha tena home kwako Hakuna kesi wala laana. Damu ya jambazi, mwizi na mchawi hazina password zile hazina laana huwezi dhurika, wale ni watoto wa shetani Hakuna hatia yeyeto wala dhambi.
 
Back
Top Bottom