SoC01 Dada alivyohitimisha maisha ya ndoto yake

Stories of Change - 2021 Competition

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Anaitwa Bahati, tangu akiwa mdogo alishaamua atapambana na maisha na kuboresha maisha ya familia yao. Baba yake alikua Mchungaji wa kanisa, mama mwalimu. Wakizaliwa sita na kati ya hao wa kike walikua wanne.

Baba yao alipokea wageni wengi wa kanisa kutoka nchi mbalimbali. Kuna wakati walipokea vijana kutoka Australia walikuja kufundishia Kiingereza kwa kujitolea katika shule za Tanzania. Wale vijana walipewa hifadhi ya kulala katika nyumba ya mchungaji.

Baada ya Christmas, mkusanyo wa ada na nauli za watoto kurudi shuleni ulimsumbua kidogo mzee mchungaji, katika maongezi, mgeni mmoja kutoka Autralia aliwaambia kwa shule zao hazilipi ada na elimu inatolewa nzuri kabisa.

Bahati aliyaweka haya moyoni. Aliwaza siku moja atawapeleka watoto wake kusoma Ulaya au Australia. Alianza kufuatilia maisha ya nchi hizo.

Baada ya kumaliza form six na division II ya PCB aliamua kusoma shahada ya uuguzi Muhimbili. Alimaliza shule, aliolewa na kupata watoto. Ndoto yake ikiwa bado kichwani. Aliweza kuomba nafasi ya kusoma shahada ya Uzamili katika masomo ya uiguuzi Ulaya.

Kazini hakupata ufadhili. Ilimlazimu kuchukua likizo bila malipo. Amefika Ulaya na akiba ya kama milioni 5 pesa za Tanzania. Ada anatakiwa kulipa ni milioni 20. Alianza kazi katika nyumba ya kulea wazee akifanya kazi hii usiku na asubuhi alikwenda darasani.

Aliomba shule alipe ada kidogo kidogo. Kila mwisho wa mwezi aliipa milioni 1.5 shule na nyingine alinunua chakula na kulipa pango la nyumba. Mara nyingi alisinzia darasani kwani alikua akitoka kazini usiku.

Alifanikiwa kumaliza shahada yake na ufaulu mzuri. Alipata ajira na kuchukua watoto wake. Alitamani watoto wapate elimu ya Ulaya na alifanikiwa kufikia ndoto yake.
 
Ok nishapata funzo hapo kwamba kama una ndoto unawaza kuifanya Basi pambana utatoboa siku moja pamoja na changamoto zote utakazopitia..SI ndio mam mdogo sky
 
Somo. Tupokee wageni nyumbani. Haijulikani mbaraka utatoka wapi. The mind is not a container to be filled but a fire to be ignited.
 
Back
Top Bottom