D Voice amebakisha siku chache kutambulishwa WCB, dogo ameshaula tayari

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,427
21,118
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.

Hatimaye ile ndoto ya muda mrefu ya msanii wa singeli kutokea Temeke ukipenda muite London boy D voice jinii inakaribia kutimia siku chache zijazo.

Msanii D voice yupo wasafi muda mrefu sana, kula yake, vaa yake mpaka sehemu anapoishi yote ipo chini ya wasafi.

D voice ameshawahi kutamba na ngoma kadhaa kama vile kuachana Sh ngapi aliyomshirikisha Barnaba Classic, Mchanganyiko aliyomshirikisha Baddest.

Pia aliwahi kutamba na wimbo wa madanga ya mke wangu alioshirikishwa na Meja Kunta.

D Voice aliachana na management yake ya awali mwishoni mwa mwaka jana hivyo Wasafi wakaona wasiache hiki kipaji kipotee hivi hivi wakaamua kumchukua na mpaka sasa yupo mikononi mwao anasuburiwa tu kutambulishwa rasmi hiyo tarehe 16.

Ukimya wake D Voice utakuwa na kishindo kikuu.

Kila la heri kwake ila asianze kuwavimbia wenzake awe kama mwanzo na tabia ile ile ya kuwaheshimu wenzake walimtangulia kwenye muziki wa singeli.


-1805718260.jpg
 
Back
Top Bottom