Tathmini: Zikiwa zimebaki siku saba birthday ya Diamond Platnumz

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Katika miaka yote hakika mwaka 2015 umekuwa wa mafanikio sana kwa Diamond Platnumz kikazi na maisha binafsi.

(1) Princess Tiffah
: Hii ni furaha ya Diamond kwa sasa, kwa muda mrefu amekuwa akihangaikia suala la kupata mtoto lakini, mwaka huu baada ya kumpata Zari (the boss lady) ndio akafanikiwa. Hata hivyo mtoto kaja na nyota kama ya wazazi wake, kwa siku ya kwanza tu akapata mkataba wa milioni 50, na endorsement ya shopping milioni moja kila mwezi kwa mwaka mmoja jumla mil 62.. Tena baada ya siku arobaini kwenye kuonyesha sura yake akaend3lea kukusanya pesa kutoka kwa NMB, na kupitia tv rights za kipindi kilichoonyeshwa live Clouds tv..

(2) Tuzo na nominations:
Kwa mwaka huu diamond ameendeleza rekodi zake kwenye tuzo mbali mbali kwani mpaka sasa amepata tuzo 9 (6 zikiwa za kimataifa) kwa 2015;

- Hipipo (Uganda 1)
- Ktma (Tz 2)
- Archievers by UDSM (Tz 1)
- African archievers (South Africa 1)
- MTV MAMA (South Africa 1)
- Africa Nafca (USA 2)
- UEA (Uganda 1)

Na hapo bado kuna Tuzo 7 zinazosubiriwa kutolewa zenye jumla ya nominations zaidi ya 17..

(3) Hit songs na Collaborations: Kwa mwaka 2015 Diamond ametoa nyimbo mbili tu! Nasema nawe na Nana.. hizi zote zimefanya vizuri na zinaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania, Charts kwenye vituo vikubwa, views Youtube, nominations kwenye tuzo, hadi mitaani mpaka wilfred bony aliopo uingereza ikamfikia Nasema nawe akapost instagram account yake akiyarudi mauno. Na ameshirikishwa na Iyanya, K cee, Donald, Ney wa mitego na Linex...

Hata hivyo ngoma zinazosubiriwa;
- Za kwake (Ft. Neyo, Psquare, na nyingine hazijawekwa wazi)
- Za kushirikishwa (Fally ipupa, AKA, Flavour, Toofan na nyingine hazijawekwa wazi)

Vitu vingi sana vikubwa ikiwemo kutajwa kama NEMBO YA TAIFA LA TANZANIA (SHUJAA), kafanya shows zilizompa mkwanja mrefu sana, show za bila kukata tokea tar 1 (Huku akiendelea kuwa mwanamuziki ghali Afrika mashariki), kuumaliza mjengo wake STATE HOUSE unaowatoa mate kila siku wasanii wenzake.

Kuzidi kuongeza mashabiki kila kukicha MITAANI NA MITANDAONI mfano tu instagram mwaka unaanza hakuwa hata na followers laki tatu ila ndani ya miezi tisa kafika milioni, Kufungua studio yake binafsi ya WCB RECORDS ambayo mpaka sasa imemsaini msanii mmoja Harmonize, na ngoma kibao za wasanii zimerekodiwa tayari.

WANAMUZIKI WA BONGO FLAVOUR WANA VINGI SANA VYA KUJIFUNZA HAPO KUTOKA KWA KING OF AFROPOP HIFADHI YA TAIFA.

PRESIDENT DIAMOND PLATNUMZ OF WCB..

Tukiwa tunasubiria kwa hamu kubwa ile collabo bora ya kimataifa kati ya Diamond Platinumz na Neyo, mtoto wa Alicia Keys akiwa ndani ya gari la baba yake ameshindwa kuvumilia na kujikuta akisankoroka vilivyo. Baba yake bila kusita ikabidi arushe kwenye mtandao maarufu kabisa wa instagram ili kuionyesha dunia namna gani Nana ilivyompa homa mwanae.

Hizi dalili njema kwamba mziki wetu umeshatoboa tobo USA kiasi kwamba producer maarufu kama huyu mume wa Alicia Keys anasikiliza muziki wetu tena ndani ya gari yake mwenyewe. Rai yangu kwa wasanii wa Tanzania ni kuwa acheni chuki na wivu wa kijinga kwa Diamond, bali angalieni kafanyaje hadi kaweza kufanikiwa kiasi hicho ili nanyi muweze kufikia kiwango hicho na pengine kuzidi. Tunapofanikiwa si sifa kwenu binafsi bali ni sifa kwa taifa nzima.

Hongera sana Diamond na uongozi mzima wa Wasafi kwa kazi nzuri mnayoifanya.

attachment.php
Post ya mume wake na Alicia Keys huko instagram

attachment.php

Post ya Diamond Platinumz kuhusu collabo yake na Neyo

Attachment ya tatu ni video ya mtoto wa Alicia Keys akisankoroka.

.......................................................................
UPDATES>>

Baada mashabiki wa Diamond Platinumz kuvamia post ya Swiz Beats ikimuonesha binti yake anavyosankoroka na Nana fever, jamaa kapost clip nyingine ikionesha binti yake akimfundisha namna ya kucheza wimbo wa Nataka kulewa wa Diamond Platinumz. Bonyeza hapa kupakua clip hiyo.

View attachment 291906View attachment 291917
 
Mkuu vp collabo yake na dbanj bado hawajarecord? maana jamaa dbanj amemwambia kabla mwaka haujaisha wawe wameshafanya kazi
 
Hadi raha jamani kusoma uliyoandika

Mungu amwongezee yeye na familia yake zaidi na zaidi
 
mi sipendi bongo fleva hasa kama za diamond lakini namkubali sana anavyojituma...
sometimes anaingia studio usiku sana halali yuko bize...kila siku ye ni safari tu za kazi yake...sio siri anajituma sana na anajua kutumia fursa....

Kila la heri kwake.
 
Mkuu vp collabo yake na dbanj bado hawajarecord? maana jamaa dbanj amemwambia kabla mwaka haujaisha wawe wameshafanya kazi

Hiyo bado haijarecodiwa ndio maana hta na ya davido haipo hapo japokuwa zote zimeahidiwa
 
Halafu mimi sikuwaga shabiki wake kabisa wala sikuwa na time nae,ila kadili nilipokuwa nafungua mitandao nakuta watu wanamrushia madongo ndo nikasema hebu nimfuatilie nimjue huyu ni nani basi nikajiingiza ktk vita ya kupambana na wanaomponda na nimeamua sitoacha hadi nione mwisho wao na sijutii kujiingiza katika kumtetea kwa vile kuna watu wanachuki zao binafsi wanachanganya na muziki anaoufanya.
 
Back
Top Bottom