CWT yapinga walimu kusafiri bure

CWT yapinga walimu kusafiri bure

mimi naona afadhali angefanya utaratibu wa kununua STAFF BUSES... Mbona wanajeshi asa hivi wana "military buses"

Lengo lake linaweza likawa zuri ila idea yake ya kufanikisha ilo lengo ndo utata unaazia apo....

Alaf ingekua poa zaidi kama ayo mabasi yanakua STAFF kwa wafanyakazi wa Manispaa nzima... inawezekana kabisa kufanikisha ilo jambo!!
Wazo Zuri Lakn Kumbuka Askari Wanaishi Sehemu1 Wakat Walimu Wanaishi Sehemu Tofauti Tena Si Kwa Umoja
 
kwan wameambiwa walimu hawawezi kumdu naul kwenye daladala au ?
 
Bizzle for shizzle umeongea jambo la msingi sana kiukweli hawa walimu kama ni shida tu wanayo nina rafiki yangu mwalimu sametimes huwa na muonea huruma sana tokea michango ifutwe mashuleni hata msosi tu wakula mchana ishu akipata mshahara tu analipia madeni kwa mangi yani anaishi kibishi sana
 
Hii nchi hiii
Walimu shida yao si usafiri
Shida ni kipato kidogo
 
Sifa nyingine bwana ni hatari,sasa hata mwalimu hujaongea nae kama anashida ya nauli,unakurupuka tu ,unataka wasafiri bure kwenye daladala!!basi waambie wakachukue na mboga bure kariakoo!!!
Hawakulazimishwa, kama hawataki si waendelee kulipa nauli tu kwani Kuna shida?
 
Angesema wanafunzi wapande bure kidogo ningemuona anafikra pevu lakini kwa hili la waalimu kachemka tena sana tu.
 
unajua watu wanaichukulia hii issue ni kama vile Amri imetolewa kumbe wala... asiye taka hachukui kitambulisho anayetaka anapewa ... take it as a favor mnapewa na wamiliki wa mabasi kutokana na mchango wenu kwa watoto wao na sio sheria
Good comment!!!
 
Serikali inabidi iruhusu hata kutukana mara moja kwa mwezi tusi kubwakubwa huyu rais wa chama cha walimu ni wa hovyo sana na siku akija mchapakazi na anaejali maslahi ya walimu watu ndio wataamka na kutaman kumnyonga huyu jamaa yeye anachojua nikutafuta upenyo apige hela tu makonda kambania safi sana,kabla hajakataa atueleze walimu gani wamesaidiwa na chama chake na michango yao ni lini matumizi yatakua wazi kwa kila mwanachama, jinga sana.
 
inawezekana ata kama wanaishi sehemu tofauti... wanaweza kuanzisha route moja ndefu kupitia barabara zote kubwa....

Tena kama ikiwa ni "integrated plan" inayohusisha manispaa zote za jiji la Dar-es-salaam itakua ni rahisi zaid... itampunguzia gharama mtumishi wa manispaa...

mfano anakaa charambe anahitaji kulipia 400 mpaka rangi tatu alaf badala ya kulipia 600 mpaka mwenge anapofanyia kazi inabid apande staff bus la manispaa kupunguza gharama....

mbezi-kkoo (morogoro road)

mbagala-kawe-msasani (kawawa road)

G.mboto-mnazi mmoja!! (pugu road... nyerere road)

mwenge-mbagala (mandela road)

Bunju-posta (bagamoyo na mwinyi road)

kinyerezi na Tabata wanakua na route yao.... n.k
 
Sifa nyingine bwana ni hatari,sasa hata mwalimu hujaongea nae kama anashida ya nauli,unakurupuka tu ,unataka wasafiri bure kwenye daladala!!basi waambie wakachukue na mboga bure kariakoo!!!
mkuu hata mimi nachukia juu ya kukurupuka kwa huyu mfuta viatu ila hapa nampa yule rais kilaza walimu wanamchukia sana.
 
Nahc kama kunajambo ambalo makonda alishauriwa vibaya ni hili, swala la waalim kupanda magar buree ni unyanyasaji wa kijinsia, tena ni ubaguzi wa hali ya juu, na hii inataka kuchora pc kuwa waalim wanapata mshahara mdogo sana..

Hoja isingekuwa kuwasafirisha waalim bure ila wangetatua changamoto za waalm kwa kuboresha masilhi yao, na kuondoa changamoto zao, waalim hawana haja ya kutokulipa nauli,

Au makonda angekuja na hoja y usafiri wao kama puplic car au kuwakopesha vifaa vya usafr kwa mashart nafuu, haiingii akilin waalim kusafr buree watapata shida isiyokuwa na tija

Sina uhakika kama waalim watakubali, kwa mara ya kwanza katika uhai wangu wa jf naungana na g.mkoba..
Kwa hiyo na askari ambao hawalipi nauli nao wamedhalilishwa??
 
Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania G. Mkoba amesema haoni kama ni sahihi kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuingia kwenye makubaliano na wenye mabasi ya daladala ya kuwasafirisha walimu bure bila kuwashirikisha walimu wenyewe, hivyo ameshauri kuwa ni vizuri mambo yanayowahusu waalimu yakawa yanawashirikisha walimu.

Chanzo: Clouds tv
Nina msimamo wangu juu ya Makonda, nikisikia tamko lakupinga ametoa kiongozi wa UKAWA au mwanaharakati mwingine nitatafakari mawazo yake ILA, Mkoba wewe ni Jipu, Mnyonyaji wa wa walimu, na tunatafakari jinsi ya kukutumbua. Kifupi hauna sifa wala haustahili kuongea kwa niaba ya Mwalimu. HAUNA TOFAUTI NA WALE VIONGOZI WANAOBAKA DEMOKRASIA. Unabahati ya sheria za mtandao. TENA WALIMU WANAHASIRA NA WEWE LAITI UNGELIJUA....
 
Misifa.Afu kibaya zaidi katoa tangazo la kimkoa bila kumshirikisha hata mkuu wa mkoa.
 
Walimu subirini muyaone manyanyaso na matusi ya makondakta wa daladala.
Anafika kituoni anasema hata wale walimu kitambulisho juu! Mnanyoosha saba anasema nachukua wawili tuu na bus lina nafasi. Linakuja lingine mikono juu, ingia watatu. Nani ataweza manyanyaso hayo?
Suluhisho ni kuwapa transport allowance au kuamuru magari ya serikali yawe yanasimama vituoni na kutoa lift
Hiyo lift na allowance ni kwa walimu tu au na watumishi wote wa serikali??

Kama ni kwa walimu tu, why?? Kwani watumishi Wengine km manesi, wahudumu wa ofisi, makatibu muhutasi, watunza kumbukumbu, walinzi, watendaji wa vijiji na mitaa etc, etc wao hawastahili hiyo allowance na lift?
 
Hivi ni kweli walimu wana shida na nauli ya kwenda kazini? Hapana walimu hawana shida ya nauli isipokuwa walimu wana shida ya mshahara mdogo,malimbikizo yao toka kipindi cha Kikwete,kutopanda vyeo na mazingira duni ya kazi
Hivyo hayo ndio baadhi ya matatizo ya msingi waliyo nayo walimu na sio nauli ya daladala
Kwa hiyo makonda awalipe mshahara mnono walimu na kuwalipa malimbikizo yao??
 
Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania G. Mkoba amesema haoni kama ni sahihi kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuingia kwenye makubaliano na wenye mabasi ya daladala ya kuwasafirisha walimu bure bila kuwashirikisha walimu wenyewe, hivyo ameshauri kuwa ni vizuri mambo yanayowahusu waalimu yakawa yanawashirikisha walimu.

Chanzo: Clouds tv
Iko vere simpo, hutaki kupanda bure, ingia kimya kimya kisha lipa, kelele za nini???
 
Walimu kupanda daladala bure si.kipaumbele kabisa. Hata hivyo hiyo hela ya daladala ni ndogo kwa mwalimu kuimudu. Shida ni.fedheha watakayokuwa wanapata wakati wa kupanda hayo magari kwa sababu makonda kaingia makubsliano na wenye magari si madereva wala makondakta,ni aibu kwa mtu mzima kuitwa maiti. Hii nilishuhudia wakati wanajeshi wakipanda bure haya madaladala utasikia hiyo maiti sijui picha itakuwaje kwa waalimu
 
Back
Top Bottom