sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,022
- 5,254
Unasemaje ni la kisiasa wakati bodi ya mawakili (TLS) imeshiriki kumfutia uwakili? Kwa nini ulione ni la kisiasa wakati halijafanywa kwenye jukwaa lolote la chama chochote bali limefanywa mahakamani na kwenye kamati za chama cha mawakili (professional)? Na mahakama ikaja kubaini kuwa taratibu hazikufuatwaSuala la Fatma ni la kisiasa.
Hilo hatuwezi kulilinganisha na Walimu ambao hatuwaoni kwenye uharakati.
Lengo la Bodi ya Ualimu(kama zilivyo bodi zingine za kitaaluma) ni kulinda miiko, maadili ya utendaji kazi kupitia usajili na leseni zao za kazi.
Kuna mambo mengi yanayofanywa na Walimu ambayo ni kinyume na maadili ya kazi zao na wameshindwa kuwajibishwa kisa hamna chombo kinachosimamia taaluma yao.
Mwalimu akihofia kupoteza ugali kwa kwenda kinyume na maadili hatathubutu kufanya kosa.
Haya ndio mambo ambayo Bodi itatakiwa kujihusisha nayo.
Sambamba na hilo, Bodi itaweza kuwapika Walimu kupitia mchakato wa mafunzo kwa vitendo pamoja na mitihani ya usajili. Walimu akifuzu hizo hatua atakuwa kaiva kwa kiasi fulani ukilinganisha na ambaye hajapita hizo hatua, na hatimaye atasajiliwa na kupewa leseni ya kazi.
Kuna hii kesi ya Mwalimu Ezekiah Olouch Ezekiah T. Olouch vs The Permanent, Secretary, President's Office, Public Service Management & Others (Civil Appeal No.140 of 2018 ) [2020] TZCA 2; (06 January 2020) | Tanzania Legal Information Institute, Katibu Mkuu wa Wizara alimfukuza kazi huyo mwalimu pasipo kuwa na mamlaka wala pasipo kufuata taratibu na CWT alikokuwa Naibu KM wa Chama nako wakamsimamisha kazi baada ya KM kumfukuza kazi. Mwalimu amepambana sana na hatimae Mahakama ya Rufaa ikaamuru kuwa uamuzi wa KM ulikuwa batili maana hakuwa na mamlaka ya kumfukuza kazi jamaa na hivyo akarudi kazini.
Sasa hiyo bodi ya walimu inayopambaniwa ndio itakuwa fimbo rahisi ya kuwachapia walimu kwa kuwafutia uanachama ili wasifanye kazi licha ya kuwa na elimu. Huo ni ujinga, badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma
Kuhusu mafunzo ya vitendo, hakuna mwalimu anayekuwa mwalimu bila kufanya mazoezi ya vitendo, kwa hiyo yatakuwa ni marudio tu ya kilichofanyika tayari. Walimu huenda BTP/Field na kudeal na kazi halisi (wanafunzi halisi, masomo halisi nk).