CWT inaenda kinyume na malengo yake, walimu jitoeni

CWT inaenda kinyume na malengo yake, walimu jitoeni

Ni kweli hawana msimamo Ila ni wale wenye elimu ya darasa la saba kwa sasa kuna vijana wengi wanaoweza kuleta mabadiliko makubwa kwa kuleta chama mbadala.
Hicho chama mbadala kitasajiliwa na nani?!!! Chezea TZ
 
Walimu ni watu muhimu sana katika taifa hili, ni walipaji wakubwa wa kodi kwa serikali na ni kada yenye watu wengi sana. Tatizo hawana umoja. Hata raisi wao (wa CWT) anakuwa kama mfalme, sijajua katiba yao inasemaje lakini kwa kweli chama chao kinahitaji mageuzi makubwa, kama sio mabadiliko.

Waalimu wangekuwa na kauli moja wangeleta mapinduzi makubwa katika taifa -mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kifikra. Kada ya ualimu ni taasisi kubwa kuliko taasisi yeyote katika nchi kwa kigezo cha mustakabali wa taifa. Taifa likiwa na walimu mbumbumbu nalo litakuwa mbumbumbu. ukisikia nchi imefanya mageuzi -yawe ya kilimo au kiuchumi na kisiasa, tambua kwamba ni walimu waliochochea mageuzi hayo.

Hakuma taasisi, ya uma au binafsi, wanasiasa au viongozi wa serikali wanaweza kufanya mageuzi katika dola pasipo waalimu kushiriki. Waalimu wanaojitambua ni sawa na taifa linalojitambua. Waalimu kaeni chini mtafakari.
 
Juzi nimeshangaa kuona PRADO ya chama cha walimu. Ilipopitishwa kuwa walimu wote ni wanachama automatically ndipo CWT ikaanza kujigeuza kampuni ya kiuchumi.

Ile ni kampuni hizo gari za kifahari wananunua kwa mshahara ya walimu, japo ni midogo ila bado wanaikata asilimia mbili tena, hakika kufa kufaana
 
Cha msingi hapa pigeni Nazi na kumbukeni nje kuna walimu wengi wanasubili ajira.Ukibweka tu panga linapita
 
Mkuu una hoja nzuri sana, nashangaa hata katiba yao hawasambazi, halafu sheria ya kuwaingiza walimu kwenye hicho chama sijui wanaipata wapi
 
Hicho chama mbadala kitasajiliwa na nani?!!! Chezea TZ

Kuna chama kipya kimeeshasajiliwa nimeambiwa na moja wa viongozi hao inbox, na niliwaona EATV wakihojiwa, hivyo walimu hasa wanaojielewa wagugo tu watapata habari kibao kuhusu chama hicho kipya cha walimu kinaitwa Chakamwata.
 
Walimu ni watu waoga sana. Waongee wapoteze ugali wao walio unga unga???!! Mpk ugali huo kuiva imechukua mikao kibao kwa baadhi yao
 
Hawa jamaa hawanaga msimamo kabisa.... Viongozi na walimu wenyewe hawana solidarity
Hawawezi kuwa na msimamo mkuu, walimu ni wengi sana mitaani na hawana ajira!
 
Kwa jinsi walimu wa Tanzania walivyo na maisha magumu, mazingira ya kazi mabaya, mshahara mdogo, kudhalilishwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa nk. Walihitaji chama imara kinachoweza kuwatetea, kuwapigania na kuishauri serikali kuwapatia haki zao ili utendaji kazi wao uwe mzuri na elimu ya Tanzania kuwa bora.

Cha ajabu ni kwamba chama cha walimu kimekuwa na kashfa mbaya zinazoonyesha wazi kuwa sasa hiki chama cha walimu kimezeeka kinatakiwa chama mmbadala cha kutetea haki za walimu

Zifuatazo ni kashfa zinazolifiisha chama cha walimu;

(1). Kujihusisha na siasa za chama tawala; viongozi wa CWT wengi ni wanachama wa CCM na kiongozi wao wa CCM ni Rais wa nchi hivyo imakuwa ngumu kudai haki zao kwa kiongozi wa chama chao cha siasa, wanaogopa kuonekana kuwa wanaipinga serikali ya chama chao cha siasa, mfano, tumeshuhudia kiongozi wa CWT taifa kugombea uongozi wa CCM huko nyanda za juu kusini na kushinda.

Kugeuza CWT kuwa kampuni ya kiuchumi; viongozi wa chama cha walimu wamesahau kudai haki za walimu kama nyongeza ya mishahara, kupanda madaraja, malipo ya likizo, Teaching allowernce nk.ambazo ndizo changamoto za walimu zilizowafanya wakaanzisha chama ajabu wanang'ang'ania kuanzisha SACCOS, BANK, Kuongezewa posho za vikao na makato makubwa kwa walimu wenye maisha magumu.

Kuikopesha CCM mabilioni ya pesa uchaguzi wa 2015, kashfa hii ni mbaya sana na hakuna kiongozi wa CWT aliye jitokeza kukanusha hizi tuhuma kukaa kimya kwao kunaonesha wazi kuwa ni habari za kweli.

Kimeshindwa kutoa tamko lolote au kuwaunganisha walimu juu ya haki zao za kimkataba wa kazi wanazokosa katika serikali ya awamu ya tano, ni miaka miwili sasa walimu hawapati nyongeza ya mwaka, hawapandi madalaja, hamna malipo ya likizo.

Inaonesha wazi kuwa viongozi wa CWT wameungana na CCM kuwa dhulumu walimu kisha kuharibu elimu yetu wa Tanzania maana kama maslahi ya walimu hayazingatiwi hawata weza kutoa taaluma nzuri kwa watoto wetu.

=>Walimu vijana jiondoeni kwenye hicho chama kimesha zeeka hakiendi na wakati, ni tawi la CCM, ni wanyonyaji wa mshahara wenu tu.
Kuandika kuhusu walimu tanzania ni kupoteza wakati. Watumishi wa umma wa Tanzania ni tabaka la watu wanaoishi Tanzania ambao HAWAJIELEWI. Kumtetea mtu asiyejielewa kuna gharama sana na miongoni mwa hizo ni pamoja na kupoteza nguvu.
1. Ukisoma mikataba/barua zote za ajira zinasisitiza kabisa uwepo wa nyongeza ya mishahara kila mwaka . Hawajaongezewa tangu 2015 mpaka leo bila maelezo wamechukua hatua gani?
 
Walimu ni watu muhimu sana katika taifa hili, ni walipaji wakubwa wa kodi kwa serikali na ni kada yenye watu wengi sana. Tatizo hawana umoja. Hata raisi wao (wa CWT) anakuwa kama mfalme, sijajua katiba yao inasemaje lakini kwa kweli chama chao kinahitaji mageuzi makubwa, kama sio mabadiliko.

Waalimu wangekuwa na kauli moja wangeleta mapinduzi makubwa katika taifa -mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kifikra. Kada ya ualimu ni taasisi kubwa kuliko taasisi yeyote katika nchi kwa kigezo cha mustakabali wa taifa. Taifa likiwa na walimu mbumbumbu nalo litakuwa mbumbumbu. ukisikia nchi imefanya mageuzi -yawe ya kilimo au kiuchumi na kisiasa, tambua kwamba ni walimu waliochochea mageuzi hayo.

Hakuma taasisi, ya uma au binafsi, wanasiasa au viongozi wa serikali wanaweza kufanya mageuzi katika dola pasipo waalimu kushiriki. Waalimu wanaojitambua ni sawa na taifa linalojitambua. Waalimu kaeni chini mtafakari.

Dondoo zako nzuri sana
 
Kuandika kuhusu walimu tanzania ni kupoteza wakati. Watumishi wa umma wa Tanzania ni tabaka la watu wanaoishi Tanzania ambao HAWAJIELEWI. Kumtetea mtu asiyejielewa kuna gharama sana na miongoni mwa hizo ni pamoja na kupoteza nguvu.
1. Ukisoma mikataba/barua zote za ajira zinasisitiza kabisa uwepo wa nyongeza ya mishahara kila mwaka . Hawajaongezewa tangu 2015 mpaka leo bila maelezo wamechukua hatua gani?

Ni wajibu wa tunaojielewa kuwafanya wasio jielewa wajielewe
 
Hawawezi kuwa na msimamo mkuu, walimu ni wengi sana mitaani na hawana ajira!

Msimamo sio kugoma tu ila ni pamoja na kuwaeleza ukweli wananchi madhara ya kutotimiziwa madai yao, kuishitaki serikali kwa wananchi ni vizuri zaidi kuliko kugoma
 
Walimu ni watu waoga sana. Waongee wapoteze ugali wao walio unga unga???!! Mpk ugali huo kuiva imechukua mikao kibao kwa baadhi yao

Wapo majasiri na wanao jielewa wengi sana
 
Msimamo sio kugoma tu ila ni pamoja na kuwaeleza ukweli wananchi madhara ya kutotimiziwa madai yao, kuishitaki serikali kwa wananchi ni vizuri zaidi kuliko kugoma
Serikali ipi hiyo? Hii inayotaka kuonekana imeletwa na Mungu?
 
Serikali ipi hiyo? Hii inayotaka kuonekana imeletwa na Mungu?

Hakuna serikali jasiri inaposhitakiwa kwa wananchi wenye hoja nzito na wenye uwezo wa kuongea kama walimu.
 
Walimu ni watu waoga sana. Waongee wapoteze ugali wao walio unga unga???!! Mpk ugali huo kuiva imechukua mikao kibao kwa baadhi yao

Walimu ni majasiri sana ila CWT ni waoga sana so chama mbadala kinatakiwa kwa UDI na UVUMBA
 
Back
Top Bottom