Jamani wadau...nasikia sheikh Gorogosi ana shule kali sana sana ya elimu ya dini.....
amesoma chuo kikuu misri kama miaka 7 na chuo kikuu cha makka miaka kama 7...pia amesoma sana sheria za dini.....hadi leo nafikiri hakuna anaemfikia kwa elimu ya dini hapa tanzania......yaani ilikuwa karibia apate PHD ya elimu ya dini....hata sheikh Husein analijua hili...nimeumwa sikio na mdau mmoja nae ni mwana ulamaa....
__________________
Re: CV ya Sheik Gorogosi Japo CV yake sina ila kwa kadri nilivyowahi kuzungumza nae, anaonyesha ilmu duniya anayo na sifa yake ya ziada ni heshima kwa mamlaka husilka. Sheikh Mkuu alipoakiumwa, Ni Gorogosi ndiye aliyeendesha Bakwata, hata ili fukuza fukuza, Sheikh Mkuu aliibariki.
Miongoni mwa wenye ilmu kubwa ya dini, ukiondoa Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, na Sheikh Nurdin Hussein Bafadhili, waliobaki wote badobado, Sheikh Yahya Hussein pia yupo, tatizo ni longolongo za unajimu na mambo ya majini.
Mungu awaweke mahali pema peponi, Sheikh Nurdin Hussein, Hemed Bi Jumaa na Gorogosi.
Labda nishereheshe kidogo point mbili tatu za hapo juu. Almarhuum Gologosi hakumaliza degree kule misri alikatiza bila kupewa kwani degree a dini misri ni ya miaka 10. Yeye alimaliza Saudia katika fani ya Sheria specilized katika social islamic.
Mpka umauti wake alikwenda Hija mara 14.
Kuna engi sana wenye visomo va juu sana katika dini nao woooote wakiongozwa na
Prof Juma Mikidadi ( B islamic law madina, m social islam madina, PhD islamic social islamic sScotland. huyu ni mbunge wa jimbo la kibiti aliyestahafu.
Kuna Sheikh Mattaka( aliyefukuzwa bakwata ) ana masters alizosomea Misri na madina za islamic culture. na sasa anfana masters mbili kwa mpigo Open Univ dar ( MA na LL M.
Kuna akina Khalifa Khamis ( yeye ana b islamic law na B mass com. .
Kuna sheikh Chizenga ana masters
Kuna sheikh Kilemile ana Bachelor aliyosomea Misri miaka 10.
Kuna sheikh Muharami Doga. ( Huyu ndio mkali wa Nahau ( bachelor in islamic law na bachelor in arabic literature.
Mtoto wa sheikh mkuu hemed bin jumaa, yeye ana masterd aliyyochukulia Saudia.
Kuna wengi.
Al marhum Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed ( yeye hakuwa na degrii yoyote bali alisomea ndumi tanga, kisha lamu.
Al Marhum sheikh Noordin husein hakuwa na degrii oote ee alisomea kilwa, tanga na lamu.
Vile vile sheikh Yahya husein hana degrii
Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
Mapumzikoni
Mwera , Znz