Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu. Kama kuna jambo zuri ambalo Rais Magufuli analifanya basi ni kuheshimu taaluma katika kila eneo. Sehemu ambazo zinahitaji wasomi wa taaluma fulani anamuweka mtu sahihi kutokana na sifa na uzoefu alionao mtu huyo.
Miongoni mwa watu ambao kwa hakika Rais Magufuli amewaweka katika mahala pake ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara. Naamini kuwa Rais amejifunza kutoka kwa Prof Muhongo na hivyo kuwaona wasomi wabobezi ni wa msaada mkubwa sana kwake na kwa maendeleo ya nchi
Hongera sana Rais Magufuli. Najua watu watakuchukia sana ila usikate tamaa. Nchi itasonga mbele kama hutasikia sauti za wapiga zumari.