Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu, ipitie pia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
BARUA YA WAZI KWA RAIS WANGU MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

(KK)

IPITIE PIA KWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC)

YAH: OMBI JUU YA KUPATIWA KAZI KWENYE SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA (TRC) KIPINDI IKI BAADA YA KUMALIZIKA KWA ROT 1 YA DAR ES SALAAM TO MOROGORO, SISI VIJANA AMBAO TUPO CHINI YA MKANDARASI MKUU WA SGR YAPI MERKEZI.

Shikamoo mama,Pole na majukumu mazito ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania na hongera kwa kutimiza mwaka mmoja tangu uapishwe kama Rais wa awamu ya sita wa Tanzania.

Pia Ongera sana sana kwa mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania baba yangu MASANJA KADOGOSA hakika unafanya kazi kubwa sana ya kumsaidia rais wetu kuijenga Tanzania bora.

Nimeona Vyema nitumie nafasi hii ya jukwaa ili kwa unyeyekevu mkubwa kabisa kukuomba MH Rais wetu mpendwa pamoja na baba yetu mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania uweze kutukumbuka sisi vijana ambao tupo chini ya mkandarasi mkuu YAPI MERKEZI ambao tulianza ujenzi wa reli hii toka mwaka 2017 mpaka ivi sasa reli hii ya kiwango cha standard gauge inayo tembelea kwa nishati ya umeme.

Kutoka kwa mkandarasi uyu ambaye ni mkandarasi Bora kabisa wa ujenzi wa reli duniani ameajili vijana wengi na wenye taaluma tofauti tofauti (ma Engineer, wataalamu wa technologia, madakatari, idara ya rasilimali watu, wanasheri nk)

Hakika niwe muwazi sisi watu ambao tunafanya kazi na mkandarasi uyu tumejifunza vitu vingi mnoo katika sekta hii ya reli ya umeme (SGR).

Kwa sasa reli hii imekamilika kwa kiwango kikubwa na tumeona majaribio yakiwa yameanza tarehe 27.04.2022, hakika ni jambo kubwa na muhimu sana na lilikuwa likisubiliwa kwa muda mwingi sana.

Mh rais pamoja na mkurugenzi mkuu wa TRC, kwa sasa baada ya kazi kumalizika kwa mkandarasi yapi merkezi kumekuwa na utaratibu wa kawaida kabisa wa kupunguza wafanyakazi, ni ombi letu Sisi wafanyakazi wenye Taaluma muhimu sana katika sekta hii ya usafirishaji wa njia ya reli tunaomba mtuangalie kwa jicho la pekee ili tuweze kupata nafasi ya ajira katika shirika la reli ili tuweze kuendeleza ukuzaji na maendeleo mapana ya shirika letu la reli Tanzania.

Mh rais pamoja na Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania, marehemu Mh John Joseph Pombe magufuli kipindi cha uhai wake alisha tuhakikishia kuwa tungepata nafasi ya ajira kwa sisi wafanyakazi ambao tupo kwa mkandarasi mkuu wa YAPI MERKEZI.

Tunakuomba sana Mama yetu mpendwa uweze kutuangalia na sisi uku ambao tumekuwa tukifanya kazi ya kujenga reli hii kwa masaa 24 kwa siku, kwa siku zote 7 kwa week. Tumekuwa tukijenga reli hii kwa usiku na mchana kwenye mvua, kiangazi na jua kwenye mapoli makubwa kabisa ila kikubwa tunafanya kazi ili kuijenga Tanzania mpya.

Naamini kabisa ujumbe huu utakufikia moja kwa moja mama yetu mpendwa rais SAMIA SULUHU HASAN na baba yetu mpendwa mkurugenzi wa shirika la reli Tanzania MASANJA KADOGOSA.

Sisi wafanyakazi wa mkandarasi mkuu shirika la reli tuna imani kubwa sana na MH RAIS pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TRC, ninyi ni watu wasikivu na wanyeyekevu tuna amini kabisa ombi letu ili litapokerewa vyema kabisa na kufanyiwa kazi.

Mungu awabariki sana na awape nguvu na afya njema zaidi na zaidi ya kufanya kazi na kuifanya Tanzania kuwa na maendelea makubwa zaidi.

Kazi iendeleee, reli yetu kwa maendeleo yetu.
 
Ushasema una imani nae huyo mama ss na baba masanja .

Acha kulilia subiri imani yao waifanyie kazi.
 
Kwa uandishi huu watakuona haupo makini na possibly hutawashawishi kulitia maanani suala lako

tumekuwa tukifanya kazi ya kujenga reli hii kwa masaa 24 kwa siku, kwa siku zote 7 kwa week. Tumekuwa tukijenga reli hii kwa usiku na mchana kwenye mvua

Hata mashine huwa zinapumzishwa, wewe uliwezaje kufanya kazi 24/7/30/365
 
Shukuru Mungu angalau hata nyie mmeajiriwa muda wote huo Kuna wenzako wanajitolea tu kwa malipo ya chai na elfu tano ya nauli tangu 2015. Subira yavuta Kheri,Serikali haiajiri watu kwa kuwahurumia ila kwa mipango mahitaji husika na bajeti ya wakati huo.
Naomba kuwasilisha🙏🙏
 
Back
Top Bottom