Current four star Generals in Tanzania

Nijuavyo "majenerali hufa wakiwa majenerali"
 
Dr Slaa ana miaka mingapi?? Dr Slaa ni mkubwa hata JK ni mdogo! Mbona ni Balozi wetu Denmark au Swiden huko! Ni utashi wa Rais tu! Hata Marehemu Jonh Kijazi kama asingefariki,angeongezewa miaka mingine na Marehemu Magu!
Usichanganye civil service na appointment posts. Civil service ni ajira za umma, kwa nafasi za kawaida umri wa kustaafu ni miaka 60, unaruhusiwa kuongezwa miaka miwili miwili mwisho ni mara 2, umri wa mwisho kwa civil service ni miaka 65. Kwa appointment, mtu anaweza kuteuliwa hata akiwa na miaka 70!, nafasi kama za ubalozi, ubunge, uwaziri na wenyeviti wa bodi.
P
 
kaka Pascal naomba kujua kidogo hapa, Civil Service kwani si ni ajira za Umma ambazo haziwahusu Military Personnel maana wao sio civilian, je hiyo ya mwisho miaka 65 ya Civil Service inaingiaje Jeshini? Natanguliza shukrani
 
kaka Pascal naomba kujua kidogo hapa, Civil Service kwani si ni ajira za Umma ambazo haziwahusu Military Personnel maana wao sio civilian, je hiyo ya mwisho miaka 65 ya Civil Service inaingiaje Jeshini? Natanguliza shukrani
Civil service inahusu ajira zote za serikalini ikiwemo jeshini, public service ni ajira zote za umma. Umri wa kustaafu kwa ordinary public service ni miaka 60. Lakini kwa viongozi fulani ni miaka 65, wakiwemo constitutional officers. Hivyo wakuu wa taasisi za umma wanapofikisha umri wa miaka 60 wa kustaafu kwa lazima, rais anaweza kuwaongezea miaka 2, kama hajapata mtu, anaongezwa miaka 2 tena na hapo ndio mwisho.

Ukiwa mkuu wa taasisi, unapofikisha umri wa miaka 55, unatakiwa kuandaa succession plan ya mrithi wako, kwa spotting na grooming. Wakuu wachoyo hili huwa hawafanyi ili waongezewe ile miaka miwili miwili ya kutafuta succesor.

Huu uteuzi wa juzi kumuondoa Lt. Gen kwa kumpa ubalozi ni kumzuia asiwe CDF, hivyo any moment from now, kuna mtu atapandishwa cheo kuwa Lt. Gen, ndie atakuwa mnadhimu na kumpokea CDF.
P
 
Ahksante sana kwa ufafanuzi kaka. Nmekupata vyema bila chenga
 
Hii paragraph ya mwisho imebeba ujumbe mzito sana ila tatzo linakuja ni kua pamoja na kua balozi ila bado anabaki kua mtumishi wa jeshi, means incase akitenguliwa huko atarudi jeshini km kwa aliekua mkurugenzi wa Takukuru ambae anarudi jeshini kupangiwa majukumu mengine?...sasa swali la msingi ni Je tutakua na ma Lt Jenerali wawili?kwani asingemtaafisha then akamteua balozi?
 
jeshi gani brother? embu tuambie by example
 
JWTZ imewahi kuwa na maafisa jenerali wenye cheo cha luteni jenerali zaidi ya mmoja wakitumikia jeshi pamoja, mfano wa siku za karibuni maafisa hao ni Luteni jenerali Yacoub Hassan Mohamed mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Luteni jenerali Paul Peter Massao mkuu wa Chuo cha Taifa cha ulinzi NDC


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya peni, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13. 2018
 
Inawezekana ni kwa sababu idadi ya wanajeshi siyo kubwa kwa hiyo haina haja ya kuwa na majenerali wa four star wengi

marekani unayoisema ina wanajeshi wengi mno hivyo haliwez kuongozwa na general mmoja
 
Naona wengi hapa wanabishana kuhusu uwezekano wa kuwa na Four Stars Generals wengi kwa wkt mmoja, issue ni kuwa Ukubwa wa Jeshi ndio una-determine aina ya maafisa wa kuongoza sehem husika, ndo maana unaona kuna vinchi ambavyo vijeshi vyao vidogo CDF wao wala sio four star generals, kuna vinchi CDF ni Kanali tu wa Jeshi kutokana na ukubwa wa Jeshi lao, na sisi kwa ukubwa wa Jeshi letu halihitaji kuwa na Four Star Generals zaidi ya mmoja, wkt ukifka itakua tu!!!
 
Mkuu hii umeitoa mahali mazima ukaja kuitupa hapa. Huku kwetu bongo kuna tofauti na hayo uliyoyaweka hapo juu.
Huku hakuna advice, nominations wala confirmations. CIC anachagua poti wake anamweka pale, kwisha kazi. Hata kama ni luteni usu atarushwa tu apate hizo four stars.
 
bro umetisha eti hata Luteni Usu anarushwa tu, hii htr sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…