Katiba ya znz ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 imetoa uwezo kwa BLW kufanya jambo lolote bila idihini ya JMT. Wamefanya hivyo si kwa jambo moja bali zaidi ya 10 na hakuna aliyewazuia.
Hivyo uwezo wanao isipokuwa ni woga na sijui ni kwanini.
Leo wasingekuja Dodoma nani angejadili muungano wasioutaka?
Leo wasingekuwa na hoja ya serikali 3 nani angejadili muungano?
Leo wasingekuwa na hoja za mkataba nani angejadili muungano?
Makundi yote ya wznz hakuna, narudia hakuna hata moja lililowahi kuja na option tofauti na hizo hapo juu. Leo unatuaminisha wamefungwa mikono. Wameanzisha kila kitu chao bila hata kuulizwa. Wana wimbo wa taifa, bendera yao, nembo yao, Ikulu yao, BLW, SMZ. Hakuna hata siku moja mwakilishi ndani ya BLM au BLW ameahi kufikisha mswada wa kukataa muungano.
Leo wanaotafuta cha uvunguni ni hao akina Pandu, Duni na Jusa.
Oktoba 6 2012 pale bwawani wafutao wamesema kwa meneno yao wanataka muungano
Jusa Ismail
Nasor Moyo
Manosur Himid
Prof Sheriff
Maalimu yeye keshachukua kitambulisho pale kareimjee mapema kabisa.
Naye pia hataki muungano!!! lakini ana kitambulisho mfukoni
Sheni juzi kazindua sherehe za muungano Maalim Seif akiwa pembeni, nao wanataka cha uvunguni eti.
Vuai keshasema muungano wanautaka.
Hawana mtu aliyewashika, na ndani ya BMLK siyo lazima ni hiari ya mtu.
Walikuwa na hiari ya kusema hatuji Dodoma kwasababu hatupendi kuwa wajumbe, hadi hapo muungano unegefika tamati. Wamejaa tele Dodoma wanavuta laki 3 useme eti wameshikiliwa na system! Kweli, real hoja ina chembe ya mantiki hiyo.