..yaani Maalim Seif amiliki mashamba makubwa makubwa pamoja na majumba huku Tanganyika, lakini Prof.Lipumba hana ruhusu ya kumiliki ardhi Zanzibar hata kiduchu?
Daah! Teeh! Teeh! Teeh!...yaani hapo,"kisu kimegota mfupani"! Umenivunja mbavu!
Traditionally,hakuna Mtanganyika alozuiliwa ati kuwa na ardhi/kumiliki pale takriban Zanzibar yoote. Mie binafsi nawafahamu wenyeji wengi tu wa Mwambao/Pwani hiyo ya Tanganyika ambao wana mahusiano ya centuries nyingi pale Zanzibar na pia wanamiliki ardhi pale,bila ya matata!
Halikadhaklika hata ndugu zetu wa Zanzibar nao pia kwa centuries nyingi mno wakimiliki ardhi huko mabara/Tanganyika katika maeneo mbalimbali!
Lakini kama tutatazama tu kwa jicho la kukhis "ubaguzi" kwenye hiyo sharia ya umiliki wa ardhi pale Zanzibar,itakua hatuwatendei haki ndugu zetu wa Zanzibar!
Kwani leo hii pana Wagogo au Watanganyika wangapi ambao sio Wachaga...wenye kumiliki ardhi pale Marangu au Machame!? Jibu itakua zero au hata kama wapo,basi itakua hawafiki hata chembe ya thuluthi!? Daah!
Sasa hiyo sharia ambayo labda sio ya "kibaguzi" huko Bara/Tanganyika...hapo ndo ina function vipi!? Nafikiri ni muhimu pia wakti mwangine sisi Wananchi pia kutumia ile common sense,busara na hikma tulizojaaliwa!...though I appreciate that common sense can be a bit of grey area!
Pale Unguja...nakumbuka kwenye myka ile kabla ya "zogo" la vyama vingi kungia...palikua na Wabara/Watanganyika wengi tu,ambao tena walikua wala si wazaliwa wa visiwani mle...lakini waliruhusiwa kumiliki ardhi na wakiishi kwa raha mstarehe bila ya kubughudhiwa!
Wengi wao wakti huo walikua kule maeneo ya Dole na Mwakaje...tena walijenga hata Makanisa yao machache...namkumbuka Marehemu Padri Mabura...nafikiri huyu jamaa alikua ni Mnyamwezi!? Alikua ni mstaarabu na wenyeji nao pia walikua wakimpa staha zake!
Nafikiri kama ulivyosema majuzi,yakua pia pana Wanasiasa uchwara na pia labda watu wachache,wenye nia mbaya/potofu na hiyo social cohesion kiduchu iliyopo hapa nchini!?...ambao wanajaribu ku-exploit current political situation na kuzidisha khofu na mihemuko kwenye takriban kila jambo litokealo hivi sasa! Daah!
Lakini hapa hatujagusia asilan,ile history/fact ya kwamba hata hicho kipande cha Mwambao takriban woote/Coastal strip ya East Afrika pia ilikua ni mali ya ile Zanzibar Empire na Wazanzibary!
Hata baada ya huo "Muungano",pia taratibu hata za Serikali hizo mbili kupeana ardhi kwa mikataba makhusus mbona pia ziliendelea!?
Mfano ni lile Shamba/Ranch ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar-SMZ pale Makurunge-Bagamoyo...iliyokua kubwa mno na ya kisasa mno kwa wakti ule! Ambayo hatimae ikafanziwa ufisadi na ubadhilifu mkubwa mno chini ya uongozi wa yule Hassan Nassor Moyo na kundi lake! Daah! Nakhis tuyaache haya,maana hapa si pahala pake!?
Kwa kifupi,inalazim tujue zile sababu na mantik/criteria zilizomo kwenye hii sharia iliyopo hivi sasa kwenye umiliki wa ardhi pale Zanzibar!?
Baada ya hapo ndo tutazame labda validity ya hiyo sharia,au vipi wenzangu!?
Ahsanta.