Wanzanzibar acheni unafiki, Acheni ubinafsi na mtawafanya wanzanzibar walioko Bara wavamiwe na kunyanganywa mali zao. Kwanza mnatutesa sana ondokeni mtuachie nchi yetu. Na mkiingia Bara mnaingia na passport. Tumewalea sana. Mara tuwasomeshe bure, mara tuwaleteee maharagwe bure. kilakitu bure.:target:
unajua huu ni upuuzi viongozi kufikiri.changu tule wote,chako ufiche.muungano gani huu.Mungu ibariki Tanganyika!
Nyie watu wabaguzi sana, sasa wewe msukuma umelala wazungu wamechukuwa migodi yote.kwani hiyo kauli wewe umeifurahia? Je hicho alichozungumzia sio chuki?
Kumbe wewe chuki yako ni waarabu.mkuu ni walewale waarabu wenye kubobea zenjibar!
kwani lazima wapewe? Cha msingi katiba ya zanzibar imekosea kuendekeza huo ubaguzi wa wazi!
wapemba wajiandae kuja kumiliki ardhi huko pemba na unguja! Tumechoka na huo unyanyasaji wenu kwa wabara walioko zanzibar!
Bimani mwenyewe aliyetoa press conference huyo hapo kwenye picha. Mwangalie kwa makini halafu tuambie umegundua nini. Kazi kwako.
View attachment 143741
Ukiwa na maana watutowe muhanga Wazanzibari tulio wengi kwa faida ya hao wachache? Wazanzibari tutamuunga mkono yeyote kwa hili la kumiliki ardhi.Hizo ndio siasa za vibaraka wa ccm, ukiwa kibaraka ccm inakubidi ujitoe ufahamu kwanza, cuf hawajui kuwa wanaumiza ndugu zao wanaoishi bara.
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.
Mkuu hapa swala ni utanzania,kama sheria ni kwamba ardhi siyo mali ya muungano mbona wazanzibar wanamiliki ardhi huku bara?
kama issue ni ukubwa wa ardhi kwa nini wanyarwanda wamarudishwa kwao kama waamihaji haramu?
Ikija kwenye masuala ya kibaguzi kama haya wanasema "waasisi wa muungano" na yakija mambo serious "wanasema ulikuwa muungano wa Karume na Nyerere"
Chama Cha Wananchi(CUF) kimepinga wazo na rai ya kupunguza masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kulegeza nguvu zake kisheria na kuwapa fursa Watanzania Bara kumiliki ardhi Visiwani Zanzibar.
Msimamo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mwasiliano ya Umma wa CUF Salum Bimani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana visiwani humo, siku chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano) Samia Suluhu Hassan, kushauri Katiba ya Zanzibar kuangaliwa upya na kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar.
Bimani alisema kuwa suala la ardhi siyo la Muungano tangu mkataba wa awali wenye orodha ya mambo ya Muungano na siyo sahihi kufanyika marekebisho ili kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar kwani ni ndogo na ndiyo sababu hata waasisi wa Muumgano waliamua ardhi hiyo imilikiwe na wazanzibari pekee. Chanzo mwananchi
Na kina wabunge wangapi bara(tanganyika)? Au lengo limeshatimia yakhe?

pole sana mkuu, naomba uhangaike na uitafute katiba ya zanzibar utaiona inasemaje kuhusu haki ya kumiliki ardhi ipo kwa nani! Huu ubaguzi hauvumiliki hata kidogo mkuu!Kwani kuna kipengele chochote kinachosema Mtanganyika hana haki ya kumiliki ardhi? Natowa challenge aje mtu kuthibitisha hili kuwaq Mtanganyika katajwa kwenye katiba kuwa asimiliki ardhi Zanzibar.
huo uzushi usiulete hapa mkuu!Mtanganyika anaweza kumiliki ardhi Zanzibar mradi afuate taratibu. Unataka kuelewa taratibu?
Mkuu hilo ni jema sana na ndivyo inavyotakiwa kuwa.kuna aliyeandika kwamba wabara milioni 2 wakija huko watapata wapi ardhi nilikuwa napingana na hilo,kama inaruhusiwa kumiliki ardhi ni vyema.Mtanganyika anaweza kumiliki ardhi Zanzibar mradi afuate taratibu. Unataka kuelewa taratibu?