CUF wawavaa wachina: Wataka wasilete wafanyakazi wachina, watanzania wanaweza

Feb 26, 2012
39
42

Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.

Serikali iwe makini na kuhakikisha hatuleti Wawekezaji matapeli kama muwekezaji wa Ujenzi wa Terminal ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Ulinzi wa mazingira uzingatiwe katika uwekezaji wa viwandani na katika uvunaji wa maliasili yakiwemo madini.

TUMKARIBISHE RAIS XI JINPING LAKINI TUWE NA MIPANGO MADHUBUTI ILI TUNUFAIKE NA USHIRIKIANO NA CHINA

Kesho Tarehe 24 Machi 2013, Rais Xi Jiping atazuru nchi yetu. Tanzania itakuwa nchi ya pili baada ya Urusi kwa Rais Xi kutembelea tangu achaguliwe rasmi na Bunge la Jamhuri ya Watu wa China kuwa Rais wa nchi hiyo tarehe 14 Machi 2013. Kuteuliwa kwake kuwa Rais wa China kunafuatia uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu wa China na kuwa Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Majeshi ya China (na kwa hiyo kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la China) Novemba 2012 katika mkutano mkuu wa 18 wa chama hicho. Utaratibu wa kuwa na uongozi wa juu wa Chama na Serikali wa muda wa miaka 10 na viongozi wasizidi umri wa miaka 70 uliasisiwa na Deng aliyeleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini China kuanzia mwaka 1978. Uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu. China waliunga mkono mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 1964. Mwalimu Nyerere alitembelea China mwaka 1965 na alivutiwa sana na sera za Ujamaa za Mwenyekiti Mao. Katika uhai wake kabla na baada ya kun'gatuka wadhifa wa Urais, Mwalimu alitembelea China mara 13.

Katika nyanja za uhusiano wa kimataifa Dr. Salim Ahmed Salim aliyekuwa balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York alisimamia kidete kukubaliwa kwa China kujiunga katika Umoja wa Mataifa na kuchukua kiti kilichokuwa kinakaliwa na Taiwan tarehe 25 Novemba 1971. Sherehe aliyofanya Balozi Salim katika ukumbi wa Umoja Mataifa tarehe 25 Oktoba 1971, wakati Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha azimio la kuifukuza Taiwan na kuikaribisha China, ulimuudhi sana George W. H. Bush ambaye alikuwa balozi wa Marekani wa wakati huo na hatimaye akawa Rais wa Marekani 1988 – 92.

Ushirikiano na China katika miaka ya 1960 na 1970 ulifanikisha miradi kama vile Kiwanda cha nguo cha Urafiki, kiwanda cha zana za kilimo cha Ubungo na mradi mkubwa wa reli ya TAZARA. Kwa sababu ya udhaifu wa kiutendaji miradi hii imekuwa siyo endelevu. Kiwanda cha zana za kilimo kimekufa. Hata baada ya kubinafsishwa kiwanda cha Urafiki kinasuasua. Reli ya Tazara haifanyi kazi kwa kiwango chake. Mwaka 2002 ilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani elfu 677 lakini mwaka 2011 kiwango hicho kilipungua na kufikia tani elfu 248.

Katika Mkutano wa Tano wa Mawaziri kuhusu ushirikiano wa China na Afrika uliofanyika Beijing Julai 18-20 2012, Rais Hu Jintao wa China aliahidi nchi za Kiafrika mikopo ya riba nafuu ya dola bilioni 20 katika kipindi cha miaka 3 ijayo.Hili ni ongezeko la mara mbili ya msaada uliotolewa wa dola bilioni 10 katika mkutano kama huu mwaka 2009.

Mikopo itakayotolewa na China itasaidia ujenzi wa barabara, reli na miundombinu mingine, kilimo, viwanda na shughuli za uzalishaji na biashara ndogo na kati. Katika miaka 12 iliyopita biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa kasi kubwa. Mwaka 2011 thamani ya biashara yote kati ya China na Afrika ilikuwa dola bilioni 166.

Afrika iliuza China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 93. Bidhaa hizo zilikuwa malighafi hasa mafuta ghafi ya petroli, madini megine kama vile shaba na chuma. Afrika iliagiza toka China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 73 nyingi kati ya hizo zikiwa ni bidhaa za viwandani. Katika nchi nyingi za kiafrika kuna manun'guniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika. Makampuni ya China yanawekeza katika nchi za kiafrika hasa katika sekta ya madini na yanashiriki katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara.

Wafanya biashara ndogo ndogo toka China wamejitokeza katika nchi nyingi na kuzua mjadala kuwa wanachukua fursa zinazopaswa kuachiwa Waafrika wenyewe. Baada ya kifo cha Mwenyekiti Mao mwaka 1976, Deng Xiaoping alishika uongozi wa China 1978 na kuanza kubadilisha sera za Mao hatua kwa hatua. Kwanza alianza kwa kuachana na mashamba ya ujamaa na badala yake akawapa fursa familia za wakulima kulima mashamba kwa mkataba wa kuuza sehemu ya mazao yao kwenye vyombo vya dola kwa bei zilizopangwa na ziada kuuza kwenye soko huria ambako bei ilikua juu.

Wakulima wakawa na shauku ya kupata ziada kubwa ya mazao ili kuyauza kwenye soko huria na kuongeza kipato chao. Mabadiliko ya sera kutoka mashamba ya ujamaa na kwenda kwenye mashamba yanayomilikiwa na familia yaliongeza kasi ya ukuaji wa pato la sekta ya kilimo na kusaidia kupunguza umaskini.

Wakati China imeanza mabadiliko ya sera za uchumi mwaka 1978, pato la wastani la Mchina lilikuwa dola za Marekani 190 chini ya wastani wa pato la taifa la Mtanzania. Mabadiliko ya uchumi yamefanikisha ukuaji wa pato la taifa kwa kasi ya juu ya wastani wa asilimia 10 kwa mwaka kwa muda wa miaka 34. Katika historia ya dunia hakuna nchi iliyofanikiwa kukuza uchumi kwa muda mrefu na kwa kasi ya juu kama China ilivyofanya. Katika kipindi hiki biashara na nchi za nje ilikua kwa kasi ya wastani wa asilimia 16.3 kwa mwaka.

China yenye watu bilioni 1.34 hivi sasa ina wastani wa pato la taifa la dola 4930 wakati Tanzania ina wastani wa pato la taifa la dola 530. Ukuaji wa uchumi umepunguza umaskini wa kipato. Inakadiriwa Wachina zaidi ya milioni 600 wameondokana na umaskini wa kipato katika kipidi cha miaka 30. Mwaka 1979 asilimia 86 ya wananchi wa China walikuwa maskini wakiishi kwa kutumia chini ya dola 1 kwa siku. Kwa sababu ya ukuaji wa kilimo, asilimia ya watu maskini ilipungua na kufikia 54 mwaka 1987 na asilimia 36 mwaka 1996.

Ukuaji wa uchumi kwa wastan wa asilimia 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 30 umepunguza sana umaskini na kufikia asilimia 13 mwaka 2008 kwa kutumia kigezo cha kimataifa cha mtu mzima kutumia dola 1 kwa siku. Maendeleo ya viwanda yaliongezeka kwa kasi kwa serikali kuruhusu uongozi wa vijiji kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ambavyo viliwanufaisha wafanyakazi na mameneja wa viwanda hivyo ambavyo havikuwa mali ya serikali kuu. Mwaka 1980 China ilifungua eneo moja la Shenzen kilichokuwa kijiji kidogo cha wavuvi na kukifanya eneo maalum la uchumi ambapo wawekezaji kutoka nje waliruhusiwa kuanzisha viwanda.

Eneo la Shenzen lilikuwa na wakazi laki 3 mwaka 1980. Sasa limekuwa jiji kubwa la watu zaidi ya milioni 10 na maarufu kwa uzalishaji wa kila aina ya bidhaa za viwandani. Sera ya kufungua maeneo na kukaribisha wawekezaji toka nje imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uzalishaji za bidhaa za viwandani na umeifanya China kuwa karakana ya dunia. Kwa nini China ilifanikiwa kukuza uchumi wake kwa kasi ya juu baada ya mabadiliko ya sera.

Ukuaji wa uchumi unaambatana na mabadiliko ya mfumo wa uchumi kutoka kutegemea sana kilimo na kuelekea kwenye ongezeko la ajira viwandani, kutoka nguvu kazi inayoishi vijijini kuelekea nguvu kazi inayoishi mijini. Mabadiliko ya mfumo wa uchumi husababishwa na ushindani wa soko.

Serikali ya China ilikuza uchumi kwa kuruhusu ushindani wa soko na kuyapa fursa makampuni mapya yenye tija kuanza na makampuni yanayopata hasara kufilisika. Soko la ajira ukiacha mashirika ya umma liliruhusu makampuni mapya kuajiri wafanya kazi na makampuni yanayopata hasara kupunguza wafanyakazi. Sheria za kazi zilijikita katika kurahisisha uanzishwaji wa ajira. Ni vizuri kuwa na utaratibu wa hifadhi za jamii kwa wafanya kazi wanaopoteza ajira ili kupunguza makali na kuwepo kwa soko la ajira linalonyumbulika.

Wanaopoteza ajira wapate kipato cha kuwawezesha kuishi wakati wakitafuta ajira mpya. Katika kipindi cha mabadiliko ya mfumo wa uchumi, China haikuwa na mfumo mzuri wa hifadhi za jamii. Wafanyakazi wengi wanaotoka vijijini hawakuwa na huduma za jamii na vibali vya kuishi katika miji walioenda kufanya kazi. Kwa sababu ya ukosefu wa hifadhi za jamii, familia ziliwajibika kuweka akiba itakayowasaidia watakapougua na pia kuwaelimisha watoto wao.

Nchi yeyote haiwezi kuondokana na umaskini bila kukuza uchumi unaoongeza ajira. Katika suala la kukuza uchumi hakuna miujiza. Uchumi unakua kwa kuongeza elimu, ujuzi na utaalamu wa wafanyakazi, ongezeko la raslimali na vitendea kazi, na kuongezeka kwa ufanisi na tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma. Maendeleo ya teknolojia ndiyo yanayochea ukuaji wa uchumi. Kabla ya mapinduzi ya viwanda ya karne ya 18, maendeleo ya teknolojia yalitokana na uzoefu wa wakulima kwenye mashamba yao na mafundi kwenye karakana zao.

Baada ya mapinduzi ya viwanda maendeleo ya teknolojia na uvumbuzi ulitokana na majaribio ya maksudi na badae uliimarishwa na matumizi ya sayansi katika majaribio. Ukuaji wa uchumi wa nchi ambazo ziko mstari wa mbele wa maendeleo na matumizi ya teknolojia uvumbuzi wa teknolojia mpya au oboreshaji wa teknolojia ya zamani. Kasi ya uvumbuzi wa teknolojia mpya unategemea uwekezaji katika elimu ya sayansi, teknolojia na utafiti. Nchi ambazo ziko nyuma katika maendeleo ya uchumi na matumizi ya teknolojia zina fursa ya kutumia teknolojia ambayo tayari imeisha gunduliwa.

Kinachohitajika ni kutumia teknolojia iliyopo ukizingatia raslimali ulizonazo, nguvukazi yako na elimu na ujuzi wake na mazingira ya nchi yako. Wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Mao, mkakati wa maendeleo ya uchumi ulijikita katika kuwekeza kwenye viwanda vizito na kujitosheleza bila kushiriki sana katika biashara za nchi za nje. Taratibu za uchumi wa soko hazikukubaliwa.

Lengo ilikuwa kujenga jamii mpya ya kikomunisti ambapo kila mtu alitegemewa achangie katika jamii kwa kuchapa kazi kwa kadri ya uwezo wake na jamii imuwezeshe kupata mahitaji yake muhimu sawa na wananchi wengine. Matumizi ya bei za soko na motisha kwa wafanyakazi vilionekana kuwa nyenzo za kibepari. Sera nyingine kama za Hatua Kubwa Mbele (The Great Leap Forward) na Mapinduzi makubwa ya utamaduni (The Great Cultural Revolution) yalileta vurugu na kusababisha kuanguka kwa uzalishaji.

Baada ya kufanikisha mapinduzi ya kikomunisti mwaka 1949 na kuanzia mwaka 1953 China ilianza kutekeleza mipango ya maendeleo ya miaka mitano. Mipango hii ilikuwa na lengo la kujenga viwanda vizito na kutumia utaratibu wa kiutawala wa kugawa raslimali, malighafi na nguvu kazi katika sekta za uchumi. Pamoja na upungufu wa tija katika uzalishaji, jambo moja ambalo China ilifanikiwa ni kuboresha huduma za afya na hasa huduma za kinga ya maradhi na kusambaza elimu ya msingi kwa wananchi wote.

Katika uongozi wa Deng Xiaoping, China ililegeza masharti ya biashara na ikaanza kuagiza bidhaa na teknolojia kutoka nje ili kusaidia kuleta maendeleo ya haraka ya uzalishaji viwandani. Ilianza kutumia vizuri fursa za kuwa nyuma na kuzalisha bidhaa katika viwanda vilivyoajiri watu wengi kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu, vifaa vya umeme na elektronoki.

Sehemu kubwa ya bidhaa za viwanda hivi viliuzwa nchi za nje. Ukuaji wa uzalishaji viwandani ulisaidiwa na ujenzi wa miundombinu imara ya kufua na kusambaza umeme, ujenzi wa njia za usafirishaji hasa barabara, reli na viwanja vya ndege. Sera za thamani ya sarafu ya China zilihakikisha kuwa bidhaa za China zinakuwa na ushindani mkubwa katika soko la dunia.

China haikusita kupunguza thamani ya sarafu yake ili kuongeza ushindani wa bidhaa zake katika soko la dunia. Thamani ya sarafu ya China ilishuka toka yuan 1.5 mwaka 1980 na kufikia yuan 8.6 mwaka 1994 kwa dola moja ya Marekani. Baada ya 1994 sarafu ya China ilikongomewa kwenye dola ya Marekani, yuan 8.3 zikiwa sawa na dola 1. Ushindani wa bidhaa za China katika soko la dunia uliongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa tija na ufanisi uliopunguza gharama za uzalishaji za China ukilinganisha na nchi nyingine.

Sera za China zimehamasisha uwekaji wa akiba na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi. Sehemu ya pato la taifa linalowekwa kama akiba limeongezeka toka wastani wa asilimia 37 katika kipndi cha miaka 1982 – 92 mpaka kufikia asilimia 50 katika miaka ya 2003 – 2010. Uwekaji mkubwa wa akiba umeiwezesha China kugharamia uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi mkubwa sana uliofikia wastani wa asilimia 42 kwa mwaka katika kipindi 2003 - 2011. Katika miaka 10 iliyopita ukuaji wa uchumi wa China umechochewa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi ndani ya China.

Kwa kuwa China inauza bidhaa nyingi nchi za nje kuliko inazoagiza, imekuwa na ziada katika urari wa malipo ya nchi za nje na kwa hiyo kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni. Akiba ya fedha za kigeni ya China inazidi dola trilioni 3.2 sehemu kubwa ikiwa imewekwa Marekani. Tangu mwaka 2002, Marekani imekuwa inategemea akiba ya China kuziba pengo la nakisi ya bajeti ya serikali. Hivi sasa China inashinikizwa ibadilishe sera, iongeze thamani ya sarafu yake na kuongeza matumizi ya kawaida ndani ya nchi na kupunguza uwekaji mkubwa wa akiba ili inunue bidhaa nyingi kutoka nje na ipunguze uuzaji wa bidhaa zake nchi za nje.

Sera ya Ujamaa ya Tanzania ilishawishiwa sana na ujamaa wa China. China ilipoanza kubadili sera mwaka 1978, Tanzania iliendelea kusisitiza msimamo mkali wa ujamaa kama ulivyoainishwa katika Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981. Mabadiliko ya sera Tanzania yalishinikizwa na mashirika ya kimataifa hususani IMF na Benki ya Dunia na wahisani wa nchi za magharibi baada ya uchumi luporomoka mwanzoni wa miaka ya 1980. Mabadiliko ya sera nchini China ulitokana na mapambano ya kisiasa na fikra ndani ya China yenyewe.

Deng alitumia ushauri hasa wa Lee Kuan Yew, Waziri Mkuu wa Singapore na wataalam wa Benki ya Dunia lakini Wachina wenyewe ndiyo walioendesha usukani wa mabadiliko. Utekelezaji wa sera za mabadiliko nchini Chinaulifanywa kwa majaribio. Mabadiliko ya sera za kilimo yalijaribiwa katika eneo dogo. Yalipoonekana kuwa na mafanikio yalisambazwa maeneo mengine. Ukaribishaji wa wawekezaji viwandani kutoka nje ulianza Shenzen eneo lilioko karibu na Hongkong na ulipofanikiwa maeneo mengine yaliruhusu uwekezaji toka nje.

China haikubinafsisha mashirika ya umma, bali hatua kwa hatua waliruhusu makampuni binafsi kuanzishwa na kushindana na mashirika ya umma. Sekta ya fedha na mabenki bado inashikiliwa na dola. Serikali ya China iliweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu na kwa hiyo kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa vitega uchumi katika sekta ya viwanda. Mambo muhimu tunayoweza kujifunza kutoka China.

Kwanza Watanzania wenyewe ndiyo tuendeshe usukani wa mabadiliko. Tujifunze toka uzoefu wa nchi nyingine lakini tusiendeshwe na wengine. Katika utekelezaji wa sera mpya serikali inapaswa kufanya majaribio eneo dogo, kujifunza kama sera ina mafanikio itekelezwa katika maeneo mengine. Kama haifai iachwe. Kwa mfano sera ya maeneo maalum ya uchumi itekelezwe vizuri katika eneo moja na kuona matunda yake badala ya kuanza maeneo mengi madogo madogo yasiyokuwa na miundombinu ya kutosha kama ilivyo hivi sasa.

Serikali ya China imeweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu. Kila inapowezekana China inatumia utaratibu wa wale wanaonufaika na huduma za miundombinu walipie huduma hizo. Tanzania inaweza kujifunza toka China kwa kukamilisha miradi ya miundombinu inayoanzishwa kabla ya kuanza mingine na kuwa na mipango ya ujenzi wa miundimbinu inayotekelezeka.

Sera za sarafu zinazohakikisha ushindani wa kibiashara ni muhimu katika maendeleo ya viwanda. Hata hivyo izingatiwe kuwa ongezeko la tija na ufanisi katika uzalishaji liambatane na sera ya sarafu inayohakikisha ushindani wa kibiashara. Tanzania inaweza kutumia fursa zilizopo katika kuwa nyuma katika maendeleo ya uchumi na teknolojia. Ikiwa tutajipanga na kutumia teknolojia iliyopo tunaweza kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji kama walivyofanya Wachina. Mfumo wa soko unaofanya kazi kwa ufanisi ni sharti muhimu la kuchochea ukuaji wa uchumi unaoongeza ajira. Bei ya bidhaa na mishahara ya nguvu kazi iambatane na upatikanaji wake.

Uongozi wenye dira na uliyo tayari kujifunza na serikali madhubuti ndiyo msingi wa kujenga uchumi unaoongeza ajira. Changamoto ya ziada kwa Watanzania ni kupata uongozi wenye dira na serikali madhubuti kwa njia za kidemokrasia ili tuweze kujenga uchumi utakaoleta neema kwa Watanzania wote.

Katika mahusiano yetu ya biashara na uwekezaji ni muhimu kwa Tanzania kuwa na sera na mpango madhubuti ya uwekezaji wa miundo mbinu na kuusimamia ipasavyo. Misaada ya China itusaidie kutekeleza mpango wetu. Tatizo ni udhaifu mkubwa wa mipango yetu. Serikali imekuwa na mipango mingi isiyo tekelezwa au kutekelezeka.

Kuna Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ambayo inalenga kuwa Tanzania iwe ni nchi yenye kiwango cha kati cha mapato (middle income country) na hali bora ya maisha kwa wananchi. Mpango Maalum wa Kuharakisha Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Mini Tiger Plan 2020) ambao haijulikani umeishia wapi.

Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania – MKUKUTA I na MKUKUTA II na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2010-15. MKUKUTA I na MKUKUTA II hazikufanyiwa makadirio ya gharama za utekelezaji wake. Gharama za mpango wa miaka mitano ni kubwa mno na serikali haina fedha ya kuugharamia. Serikali imevamia mkakati mwingine wa Big Results Now.

Lazima tuwe na mkakati wetu wa kujenga viwanda. Tanzania isiwe chanzo cha malighafi tu za kuuza China. Gharama za uzalishaji viwandani katika nchi ya China zinaongezeka na ajira ya watu milioni 90 inategemewa kuhamia nchi nyingine. Ni vyema Tanzania ikajipanga kuwa nchi itakayoweza kuongeza ajira kwa wingi kwa shughuli za uzalishaji viwandani zinazohama toka China.

Tunapaswa kutenga eneo kubwa la kilomita za mraba 100- 200 karibu na bandari ya Tanga na Mtwara na kwa kushirikiana na sekta binafsi kulisheheni miundombinu na kulifanya kuwa eneo maalum la kuendeleza viwanda vya kuuza bidhaa nch za nje. Wawekezaji wa ndani na nje wajengewe mazingira mazuri yanayovutia kuwekeza na kuongeza ajira. Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.

China ni taifa kubwa litakalokuwa na uchumi mkubwa kuliko nchi zote duniani katika miaka 20 ijayo. Tanzania tujipange vizuri kuwa na mahusiano ya kiuchumi na China yatakayokuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba

Mwenyekiti wa Taifa

Kweli kabisa prof umenena! Tatizo la hili ni kwamba kabla hajafika walishapanga kila kitu na watu walishapanga jinsi ya kunufaika.

Si kweli watanzania hawana sifa bali sifa wanazo hila china ndio inapanga hitatoaje ajira pamoja na kuwepo sheria sidhani kama zinafuatwa katika kuajiri.
 
Good point Profesa Lipumba... Uko kimya sana mchumi kulikoni? Hawa maCCM hawajui hata vitu vidogo kama hivyo halafu wanasimama majukwaani na kusema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka
 
Tatizo hatujui mikataba inasema nini. Kama mikataba inasema waChina wana haki ya kutafuta human resource sehemu yoyote duniani na wakuu wa nchi washamwagika wino. Hapa si tutakua tunapiga kelele tu.
 
Prof amenena ila tatizo letu watanzania ni ubinafsi wakati wakuingia kwenye mikataba ya kimataifa. Matokeo yake miradi ya maendeleo haiwi na manufaa kwa jamii ila kwa watu wachache.
 
Analysis nzuri

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Tarehe 24 Machi 2013, Rais Xi Jiping atazuru nchi yetu. Tanzania itakuwa nchi ya pili baada ya Urusi kwa Rais Xi kutembelea tangu achaguliwe rasmi na Bunge la Jamhuri ya Watu wa China kuwa Rais wa nchi hiyo tarehe 14 Machi 2013. Kuteuliwa kwake kuwa Rais wa China kunafuatia uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu wa China na kuwa Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Majeshi ya China (na kwa hiyo kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la China) Novemba 2012 katika mkutano mkuu wa 18 wa chama hicho. Utaratibu wa kuwa na uongozi wa juu wa Chama na Serikali wa muda wa miaka 10 na viongozi wasizidi umri wa miaka 70 uliasisiwa na Deng aliyeleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini China kuanzia mwaka 1978. Uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu. China waliunga mkono mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 1964. Mwalimu Nyerere alitembelea China mwaka 1965 na alivutiwa sana na sera za Ujamaa za Mwenyekiti Mao. Katika uhai wake kabla na baada ya kun'gatuka wadhifa wa Urais, Mwalimu alitembelea China mara 13.

Katika nyanja za uhusiano wa kimataifa Dr. Salim Ahmed Salim aliyekuwa balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York alisimamia kidete kukubaliwa kwa China kujiunga katika Umoja wa Mataifa na kuchukua kiti kilichokuwa kinakaliwa na Taiwan tarehe 25 Novemba 1971. Sherehe aliyofanya Balozi Salim katika ukumbi wa Umoja Mataifa tarehe 25 Oktoba 1971, wakati Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha azimio la kuifukuza Taiwan na kuikaribisha China, ulimuudhi sana George W. H. Bush ambaye alikuwa balozi wa Marekani wa wakati huo na hatimaye akawa Rais wa Marekani 1988 – 92.
Ushirikiano na China katika miaka ya 1960 na 1970 ulifanikisha miradi kama vile Kiwanda cha nguo cha Urafiki, kiwanda cha zana za kilimo cha Ubungo na mradi mkubwa wa reli ya TAZARA. Kwa sababu ya udhaifu wa kiutendaji miradi hii imekuwa siyo endelevu. Kiwanda cha zana za kilimo kimekufa. Hata baada ya kubinafsishwa kiwanda cha Urafiki kinasuasua. Reli ya Tazara haifanyi kazi kwa kiwango chake. Mwaka 2002 ilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani elfu 677 lakini mwaka 2011 kiwango hicho kilipungua na kufikia tani elfu 248.
Katika Mkutano wa Tano wa Mawaziri kuhusu ushirikiano wa China na Afrika uliofanyika Beijing Julai 18-20 2012, Rais Hu Jintao wa China aliahidi nchi za Kiafrika mikopo ya riba nafuu ya dola bilioni 20 katika kipindi cha miaka 3 ijayo.Hili ni ongezeko la mara mbili ya msaada uliotolewa wa dola bilioni 10 katika mkutano kama huu mwaka 2009.
Mikopo itakayotolewa na China itasaidia ujenzi wa barabara, reli na miundombinu mingine, kilimo, viwanda na shughuli za uzalishaji na biashara ndogo na kati. Katika miaka 12 iliyopita biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa kasi kubwa. Mwaka 2011 thamani ya biashara yote kati ya China na Afrika ilikuwa dola bilioni 166.
Afrika iliuza China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 93. Bidhaa hizo zilikuwa malighafi hasa mafuta ghafi ya petroli, madini megine kama vile shaba na chuma. Afrika iliagiza toka China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 73 nyingi kati ya hizo zikiwa ni bidhaa za viwandani. Katika nchi nyingi za kiafrika kuna manun'guniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika. Makampuni ya China yanawekeza katika nchi za kiafrika hasa katika sekta ya madini na yanashiriki katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara.
Wafanya biashara ndogo ndogo toka China wamejitokeza katika nchi nyingi na kuzua mjadala kuwa wanachukua fursa zinazopaswa kuachiwa Waafrika wenyewe. Baada ya kifo cha Mwenyekiti Mao mwaka 1976, Deng Xiaoping alishika uongozi wa China 1978 na kuanza kubadilisha sera za Mao hatua kwa hatua. Kwanza alianza kwa kuachana na mashamba ya ujamaa na badala yake akawapa fursa familia za wakulima kulima mashamba kwa mkataba wa kuuza sehemu ya mazao yao kwenye vyombo vya dola kwa bei zilizopangwa na ziada kuuza kwenye soko huria ambako bei ilikua juu.
Wakulima wakawa na shauku ya kupata ziada kubwa ya mazao ili kuyauza kwenye soko huria na kuongeza kipato chao. Mabadiliko ya sera kutoka mashamba ya ujamaa na kwenda kwenye mashamba yanayomilikiwa na familia yaliongeza kasi ya ukuaji wa pato la sekta ya kilimo na kusaidia kupunguza umaskini.
Wakati China imeanza mabadiliko ya sera za uchumi mwaka 1978, pato la wastani la Mchina lilikuwa dola za Marekani 190 chini ya wastani wa pato la taifa la Mtanzania. Mabadiliko ya uchumi yamefanikisha ukuaji wa pato la taifa kwa kasi ya juu ya wastani wa asilimia 10 kwa mwaka kwa muda wa miaka 34. Katika historia ya dunia hakuna nchi iliyofanikiwa kukuza uchumi kwa muda mrefu na kwa kasi ya juu kama China ilivyofanya. Katika kipindi hiki biashara na nchi za nje ilikua kwa kasi ya wastani wa asilimia 16.3 kwa mwaka.
China yenye watu bilioni 1.34 hivi sasa ina wastani wa pato la taifa la dola 4930 wakati Tanzania ina wastani wa pato la taifa la dola 530. Ukuaji wa uchumi umepunguza umaskini wa kipato. Inakadiriwa Wachina zaidi ya milioni 600 wameondokana na umaskini wa kipato katika kipidi cha miaka 30. Mwaka 1979 asilimia 86 ya wananchi wa China walikuwa maskini wakiishi kwa kutumia chini ya dola 1 kwa siku. Kwa sababu ya ukuaji wa kilimo, asilimia ya watu maskini ilipungua na kufikia 54 mwaka 1987 na asilimia 36 mwaka 1996.
Ukuaji wa uchumi kwa wastan wa asilimia 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 30 umepunguza sana umaskini na kufikia asilimia 13 mwaka 2008 kwa kutumia kigezo cha kimataifa cha mtu mzima kutumia dola 1 kwa siku. Maendeleo ya viwanda yaliongezeka kwa kasi kwa serikali kuruhusu uongozi wa vijiji kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ambavyo viliwanufaisha wafanyakazi na mameneja wa viwanda hivyo ambavyo havikuwa mali ya serikali kuu. Mwaka 1980 China ilifungua eneo moja la Shenzen kilichokuwa kijiji kidogo cha wavuvi na kukifanya eneo maalum la uchumi ambapo wawekezaji kutoka nje waliruhusiwa kuanzisha viwanda.
Eneo la Shenzen lilikuwa na wakazi laki 3 mwaka 1980. Sasa limekuwa jiji kubwa la watu zaidi ya milioni 10 na maarufu kwa uzalishaji wa kila aina ya bidhaa za viwandani. Sera ya kufungua maeneo na kukaribisha wawekezaji toka nje imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uzalishaji za bidhaa za viwandani na umeifanya China kuwa karakana ya dunia. Kwa nini China ilifanikiwa kukuza uchumi wake kwa kasi ya juu baada ya mabadiliko ya sera.
Ukuaji wa uchumi unaambatana na mabadiliko ya mfumo wa uchumi kutoka kutegemea sana kilimo na kuelekea kwenye ongezeko la ajira viwandani, kutoka nguvu kazi inayoishi vijijini kuelekea nguvu kazi inayoishi mijini. Mabadiliko ya mfumo wa uchumi husababishwa na ushindani wa soko.
Serikali ya China ilikuza uchumi kwa kuruhusu ushindani wa soko na kuyapa fursa makampuni mapya yenye tija kuanza na makampuni yanayopata hasara kufilisika. Soko la ajira ukiacha mashirika ya umma liliruhusu makampuni mapya kuajiri wafanya kazi na makampuni yanayopata hasara kupunguza wafanyakazi. Sheria za kazi zilijikita katika kurahisisha uanzishwaji wa ajira. Ni vizuri kuwa na utaratibu wa hifadhi za jamii kwa wafanya kazi wanaopoteza ajira ili kupunguza makali na kuwepo kwa soko la ajira linalonyumbulika.
Wanaopoteza ajira wapate kipato cha kuwawezesha kuishi wakati wakitafuta ajira mpya. Katika kipindi cha mabadiliko ya mfumo wa uchumi, China haikuwa na mfumo mzuri wa hifadhi za jamii. Wafanyakazi wengi wanaotoka vijijini hawakuwa na huduma za jamii na vibali vya kuishi katika miji walioenda kufanya kazi. Kwa sababu ya ukosefu wa hifadhi za jamii, familia ziliwajibika kuweka akiba itakayowasaidia watakapougua na pia kuwaelimisha watoto wao.
Nchi yeyote haiwezi kuondokana na umaskini bila kukuza uchumi unaoongeza ajira. Katika suala la kukuza uchumi hakuna miujiza. Uchumi unakua kwa kuongeza elimu, ujuzi na utaalamu wa wafanyakazi, ongezeko la raslimali na vitendea kazi, na kuongezeka kwa ufanisi na tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma. Maendeleo ya teknolojia ndiyo yanayochea ukuaji wa uchumi. Kabla ya mapinduzi ya viwanda ya karne ya 18, maendeleo ya teknolojia yalitokana na uzoefu wa wakulima kwenye mashamba yao na mafundi kwenye karakana zao.
Baada ya mapinduzi ya viwanda maendeleo ya teknolojia na uvumbuzi ulitokana na majaribio ya maksudi na badae uliimarishwa na matumizi ya sayansi katika majaribio. Ukuaji wa uchumi wa nchi ambazo ziko mstari wa mbele wa maendeleo na matumizi ya teknolojia uvumbuzi wa teknolojia mpya au oboreshaji wa teknolojia ya zamani. Kasi ya uvumbuzi wa teknolojia mpya unategemea uwekezaji katika elimu ya sayansi, teknolojia na utafiti. Nchi ambazo ziko nyuma katika maendeleo ya uchumi na matumizi ya teknolojia zina fursa ya kutumia teknolojia ambayo tayari imeisha gunduliwa.
Kinachohitajika ni kutumia teknolojia iliyopo ukizingatia raslimali ulizonazo, nguvukazi yako na elimu na ujuzi wake na mazingira ya nchi yako. Wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Mao, mkakati wa maendeleo ya uchumi ulijikita katika kuwekeza kwenye viwanda vizito na kujitosheleza bila kushiriki sana katika biashara za nchi za nje. Taratibu za uchumi wa soko hazikukubaliwa.
Lengo ilikuwa kujenga jamii mpya ya kikomunisti ambapo kila mtu alitegemewa achangie katika jamii kwa kuchapa kazi kwa kadri ya uwezo wake na jamii imuwezeshe kupata mahitaji yake muhimu sawa na wananchi wengine. Matumizi ya bei za soko na motisha kwa wafanyakazi vilionekana kuwa nyenzo za kibepari. Sera nyingine kama za Hatua Kubwa Mbele (The Great Leap Forward) na Mapinduzi makubwa ya utamaduni (The Great Cultural Revolution) yalileta vurugu na kusababisha kuanguka kwa uzalishaji.
Baada ya kufanikisha mapinduzi ya kikomunisti mwaka 1949 na kuanzia mwaka 1953 China ilianza kutekeleza mipango ya maendeleo ya miaka mitano. Mipango hii ilikuwa na lengo la kujenga viwanda vizito na kutumia utaratibu wa kiutawala wa kugawa raslimali, malighafi na nguvu kazi katika sekta za uchumi. Pamoja na upungufu wa tija katika uzalishaji, jambo moja ambalo China ilifanikiwa ni kuboresha huduma za afya na hasa huduma za kinga ya maradhi na kusambaza elimu ya msingi kwa wananchi wote.
Katika uongozi wa Deng Xiaoping, China ililegeza masharti ya biashara na ikaanza kuagiza bidhaa na teknolojia kutoka nje ili kusaidia kuleta maendeleo ya haraka ya uzalishaji viwandani. Ilianza kutumia vizuri fursa za kuwa nyuma na kuzalisha bidhaa katika viwanda vilivyoajiri watu wengi kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu, vifaa vya umeme na elektronoki.
Sehemu kubwa ya bidhaa za viwanda hivi viliuzwa nchi za nje. Ukuaji wa uzalishaji viwandani ulisaidiwa na ujenzi wa miundombinu imara ya kufua na kusambaza umeme, ujenzi wa njia za usafirishaji hasa barabara, reli na viwanja vya ndege. Sera za thamani ya sarafu ya China zilihakikisha kuwa bidhaa za China zinakuwa na ushindani mkubwa katika soko la dunia.
China haikusita kupunguza thamani ya sarafu yake ili kuongeza ushindani wa bidhaa zake katika soko la dunia. Thamani ya sarafu ya China ilishuka toka yuan 1.5 mwaka 1980 na kufikia yuan 8.6 mwaka 1994 kwa dola moja ya Marekani. Baada ya 1994 sarafu ya China ilikongomewa kwenye dola ya Marekani, yuan 8.3 zikiwa sawa na dola 1. Ushindani wa bidhaa za China katika soko la dunia uliongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa tija na ufanisi uliopunguza gharama za uzalishaji za China ukilinganisha na nchi nyingine.
Sera za China zimehamasisha uwekaji wa akiba na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi. Sehemu ya pato la taifa linalowekwa kama akiba limeongezeka toka wastani wa asilimia 37 katika kipndi cha miaka 1982 – 92 mpaka kufikia asilimia 50 katika miaka ya 2003 – 2010. Uwekaji mkubwa wa akiba umeiwezesha China kugharamia uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi mkubwa sana uliofikia wastani wa asilimia 42 kwa mwaka katika kipindi 2003 – 2011. Katika miaka 10 iliyopita ukuaji wa uchumi wa China umechochewa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi ndani ya China.
Kwa kuwa China inauza bidhaa nyingi nchi za nje kuliko inazoagiza, imekuwa na ziada katika urari wa malipo ya nchi za nje na kwa hiyo kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni. Akiba ya fedha za kigeni ya China inazidi dola trilioni 3.2 sehemu kubwa ikiwa imewekwa Marekani. Tangu mwaka 2002, Marekani imekuwa inategemea akiba ya China kuziba pengo la nakisi ya bajeti ya serikali. Hivi sasa China inashinikizwa ibadilishe sera, iongeze thamani ya sarafu yake na kuongeza matumizi ya kawaida ndani ya nchi na kupunguza uwekaji mkubwa wa akiba ili inunue bidhaa nyingi kutoka nje na ipunguze uuzaji wa bidhaa zake nchi za nje.
Sera ya Ujamaa ya Tanzania ilishawishiwa sana na ujamaa wa China. China ilipoanza kubadili sera mwaka 1978, Tanzania iliendelea kusisitiza msimamo mkali wa ujamaa kama ulivyoainishwa katika Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981. Mabadiliko ya sera Tanzania yalishinikizwa na mashirika ya kimataifa hususani IMF na Benki ya Dunia na wahisani wa nchi za magharibi baada ya uchumi luporomoka mwanzoni wa miaka ya 1980. Mabadiliko ya sera nchini China ulitokana na mapambano ya kisiasa na fikra ndani ya China yenyewe.
Deng alitumia ushauri hasa wa Lee Kuan Yew, Waziri Mkuu wa Singapore na wataalam wa Benki ya Dunia lakini Wachina wenyewe ndiyo walioendesha usukani wa mabadiliko. Utekelezaji wa sera za mabadiliko nchini Chinaulifanywa kwa majaribio. Mabadiliko ya sera za kilimo yalijaribiwa katika eneo dogo. Yalipoonekana kuwa na mafanikio yalisambazwa maeneo mengine. Ukaribishaji wa wawekezaji viwandani kutoka nje ulianza Shenzen eneo lilioko karibu na Hongkong na ulipofanikiwa maeneo mengine yaliruhusu uwekezaji toka nje.
China haikubinafsisha mashirika ya umma, bali hatua kwa hatua waliruhusu makampuni binafsi kuanzishwa na kushindana na mashirika ya umma. Sekta ya fedha na mabenki bado inashikiliwa na dola. Serikali ya China iliweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu na kwa hiyo kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa vitega uchumi katika sekta ya viwanda. Mambo muhimu tunayoweza kujifunza kutoka China.
Kwanza Watanzania wenyewe ndiyo tuendeshe usukani wa mabadiliko. Tujifunze toka uzoefu wa nchi nyingine lakini tusiendeshwe na wengine. Katika utekelezaji wa sera mpya serikali inapaswa kufanya majaribio eneo dogo, kujifunza kama sera ina mafanikio itekelezwa katika maeneo mengine. Kama haifai iachwe. Kwa mfano sera ya maeneo maalum ya uchumi itekelezwe vizuri katika eneo moja na kuona matunda yake badala ya kuanza maeneo mengi madogo madogo yasiyokuwa na miundombinu ya kutosha kama ilivyo hivi sasa.
Serikali ya China imeweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu. Kila inapowezekana China inatumia utaratibu wa wale wanaonufaika na huduma za miundombinu walipie huduma hizo. Tanzania inaweza kujifunza toka China kwa kukamilisha miradi ya miundombinu inayoanzishwa kabla ya kuanza mingine na kuwa na mipango ya ujenzi wa miundimbinu inayotekelezeka.
Sera za sarafu zinazohakikisha ushindani wa kibiashara ni muhimu katika maendeleo ya viwanda. Hata hivyo izingatiwe kuwa ongezeko la tija na ufanisi katika uzalishaji liambatane na sera ya sarafu inayohakikisha ushindani wa kibiashara. Tanzania inaweza kutumia fursa zilizopo katika kuwa nyuma katika maendeleo ya uchumi na teknolojia. Ikiwa tutajipanga na kutumia teknolojia iliyopo tunaweza kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji kama walivyofanya Wachina. Mfumo wa soko unaofanya kazi kwa ufanisi ni sharti muhimu la kuchochea ukuaji wa uchumi unaoongeza ajira. Bei ya bidhaa na mishahara ya nguvu kazi iambatane na upatikanaji wake.
Uongozi wenye dira na uliyo tayari kujifunza na serikali madhubuti ndiyo msingi wa kujenga uchumi unaoongeza ajira. Changamoto ya ziada kwa Watanzania ni kupata uongozi wenye dira na serikali madhubuti kwa njia za kidemokrasia ili tuweze kujenga uchumi utakaoleta neema kwa Watanzania wote.
Katika mahusiano yetu ya biashara na uwekezaji ni muhimu kwa Tanzania kuwa na sera na mpango madhubuti ya uwekezaji wa miundo mbinu na kuusimamia ipasavyo. Misaada ya China itusaidie kutekeleza mpango wetu. Tatizo ni udhaifu mkubwa wa mipango yetu. Serikali imekuwa na mipango mingi isiyo tekelezwa au kutekelezeka.
Kuna Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ambayo inalenga kuwa Tanzania iwe ni nchi yenye kiwango cha kati cha mapato (middle income country) na hali bora ya maisha kwa wananchi. Mpango Maalum wa Kuharakisha Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Mini Tiger Plan 2020) ambao haijulikani umeishia wapi.
Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania – MKUKUTA I na MKUKUTA II na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2010-15. MKUKUTA I na MKUKUTA II hazikufanyiwa makadirio ya gharama za utekelezaji wake. Gharama za mpango wa miaka mitano ni kubwa mno na serikali haina fedha ya kuugharamia. Serikali imevamia mkakati mwingine wa Big Results Now.
Lazima tuwe na mkakati wetu wa kujenga viwanda. Tanzania isiwe chanzo cha malighafi tu za kuuza China. Gharama za uzalishaji viwandani katika nchi ya China zinaongezeka na ajira ya watu milioni 90 inategemewa kuhamia nchi nyingine. Ni vyema Tanzania ikajipanga kuwa nchi itakayoweza kuongeza ajira kwa wingi kwa shughuli za uzalishaji viwandani zinazohama toka China.
Tunapaswa kutenga eneo kubwa la kilomita za mraba 100- 200 karibu na bandari ya Tanga na Mtwara na kwa kushirikiana na sekta binafsi kulisheheni miundombinu na kulifanya kuwa eneo maalum la kuendeleza viwanda vya kuuza bidhaa nch za nje. Wawekezaji wa ndani na nje wajengewe mazingira mazuri yanayovutia kuwekeza na kuongeza ajira. Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.
Serikali iwe makini na kuhakikisha hatuleti Wawekezaji matapeli kama muwekezaji wa Ujenzi wa Terminal ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Ulinzi wa mazingira uzingatiwe katika uwekezaji wa viwandani na katika uvunaji wa maliasili yakiwemo madini.
China ni taifa kubwa litakalokuwa na uchumi mkubwa kuliko nchi zote duniani katika miaka 20 ijayo. Tanzania tujipange vizuri kuwa na mahusiano ya kiuchumi na China yatakayokuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
 
Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.

Serikali iwe makini na kuhakikisha hatuleti Wawekezaji matapeli kama muwekezaji wa Ujenzi wa Terminal ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Ulinzi wa mazingira uzingatiwe katika uwekezaji wa viwandani na katika uvunaji wa maliasili yakiwemo madini.

TUMKARIBISHE RAIS XI JINPING LAKINI TUWE NA MIPANGO MADHUBUTI ILI TUNUFAIKE NA USHIRIKIANO NA CHINA

Kesho Tarehe 24 Machi 2013, Rais Xi Jiping atazuru nchi yetu. Tanzania itakuwa nchi ya pili baada ya Urusi kwa Rais Xi kutembelea tangu achaguliwe rasmi na Bunge la Jamhuri ya Watu wa China kuwa Rais wa nchi hiyo tarehe 14 Machi 2013. Kuteuliwa kwake kuwa Rais wa China kunafuatia uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu wa China na kuwa Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Majeshi ya China (na kwa hiyo kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la China) Novemba 2012 katika mkutano mkuu wa 18 wa chama hicho. Utaratibu wa kuwa na uongozi wa juu wa Chama na Serikali wa muda wa miaka 10 na viongozi wasizidi umri wa miaka 70 uliasisiwa na Deng aliyeleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini China kuanzia mwaka 1978. Uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu. China waliunga mkono mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 1964. Mwalimu Nyerere alitembelea China mwaka 1965 na alivutiwa sana na sera za Ujamaa za Mwenyekiti Mao. Katika uhai wake kabla na baada ya kun'gatuka wadhifa wa Urais, Mwalimu alitembelea China mara 13.

Katika nyanja za uhusiano wa kimataifa Dr. Salim Ahmed Salim aliyekuwa balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York alisimamia kidete kukubaliwa kwa China kujiunga katika Umoja wa Mataifa na kuchukua kiti kilichokuwa kinakaliwa na Taiwan tarehe 25 Novemba 1971. Sherehe aliyofanya Balozi Salim katika ukumbi wa Umoja Mataifa tarehe 25 Oktoba 1971, wakati Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha azimio la kuifukuza Taiwan na kuikaribisha China, ulimuudhi sana George W. H. Bush ambaye alikuwa balozi wa Marekani wa wakati huo na hatimaye akawa Rais wa Marekani 1988 – 92.

Ushirikiano na China katika miaka ya 1960 na 1970 ulifanikisha miradi kama vile Kiwanda cha nguo cha Urafiki, kiwanda cha zana za kilimo cha Ubungo na mradi mkubwa wa reli ya TAZARA. Kwa sababu ya udhaifu wa kiutendaji miradi hii imekuwa siyo endelevu. Kiwanda cha zana za kilimo kimekufa. Hata baada ya kubinafsishwa kiwanda cha Urafiki kinasuasua. Reli ya Tazara haifanyi kazi kwa kiwango chake. Mwaka 2002 ilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani elfu 677 lakini mwaka 2011 kiwango hicho kilipungua na kufikia tani elfu 248.

Katika Mkutano wa Tano wa Mawaziri kuhusu ushirikiano wa China na Afrika uliofanyika Beijing Julai 18-20 2012, Rais Hu Jintao wa China aliahidi nchi za Kiafrika mikopo ya riba nafuu ya dola bilioni 20 katika kipindi cha miaka 3 ijayo.Hili ni ongezeko la mara mbili ya msaada uliotolewa wa dola bilioni 10 katika mkutano kama huu mwaka 2009.

Mikopo itakayotolewa na China itasaidia ujenzi wa barabara, reli na miundombinu mingine, kilimo, viwanda na shughuli za uzalishaji na biashara ndogo na kati. Katika miaka 12 iliyopita biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa kasi kubwa. Mwaka 2011 thamani ya biashara yote kati ya China na Afrika ilikuwa dola bilioni 166.

Afrika iliuza China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 93. Bidhaa hizo zilikuwa malighafi hasa mafuta ghafi ya petroli, madini megine kama vile shaba na chuma. Afrika iliagiza toka China bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 73 nyingi kati ya hizo zikiwa ni bidhaa za viwandani. Katika nchi nyingi za kiafrika kuna manun'guniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika. Makampuni ya China yanawekeza katika nchi za kiafrika hasa katika sekta ya madini na yanashiriki katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara.

Wafanya biashara ndogo ndogo toka China wamejitokeza katika nchi nyingi na kuzua mjadala kuwa wanachukua fursa zinazopaswa kuachiwa Waafrika wenyewe. Baada ya kifo cha Mwenyekiti Mao mwaka 1976, Deng Xiaoping alishika uongozi wa China 1978 na kuanza kubadilisha sera za Mao hatua kwa hatua. Kwanza alianza kwa kuachana na mashamba ya ujamaa na badala yake akawapa fursa familia za wakulima kulima mashamba kwa mkataba wa kuuza sehemu ya mazao yao kwenye vyombo vya dola kwa bei zilizopangwa na ziada kuuza kwenye soko huria ambako bei ilikua juu.

Wakulima wakawa na shauku ya kupata ziada kubwa ya mazao ili kuyauza kwenye soko huria na kuongeza kipato chao. Mabadiliko ya sera kutoka mashamba ya ujamaa na kwenda kwenye mashamba yanayomilikiwa na familia yaliongeza kasi ya ukuaji wa pato la sekta ya kilimo na kusaidia kupunguza umaskini.

Wakati China imeanza mabadiliko ya sera za uchumi mwaka 1978, pato la wastani la Mchina lilikuwa dola za Marekani 190 chini ya wastani wa pato la taifa la Mtanzania. Mabadiliko ya uchumi yamefanikisha ukuaji wa pato la taifa kwa kasi ya juu ya wastani wa asilimia 10 kwa mwaka kwa muda wa miaka 34. Katika historia ya dunia hakuna nchi iliyofanikiwa kukuza uchumi kwa muda mrefu na kwa kasi ya juu kama China ilivyofanya. Katika kipindi hiki biashara na nchi za nje ilikua kwa kasi ya wastani wa asilimia 16.3 kwa mwaka.

China yenye watu bilioni 1.34 hivi sasa ina wastani wa pato la taifa la dola 4930 wakati Tanzania ina wastani wa pato la taifa la dola 530. Ukuaji wa uchumi umepunguza umaskini wa kipato. Inakadiriwa Wachina zaidi ya milioni 600 wameondokana na umaskini wa kipato katika kipidi cha miaka 30. Mwaka 1979 asilimia 86 ya wananchi wa China walikuwa maskini wakiishi kwa kutumia chini ya dola 1 kwa siku. Kwa sababu ya ukuaji wa kilimo, asilimia ya watu maskini ilipungua na kufikia 54 mwaka 1987 na asilimia 36 mwaka 1996.

Ukuaji wa uchumi kwa wastan wa asilimia 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 30 umepunguza sana umaskini na kufikia asilimia 13 mwaka 2008 kwa kutumia kigezo cha kimataifa cha mtu mzima kutumia dola 1 kwa siku. Maendeleo ya viwanda yaliongezeka kwa kasi kwa serikali kuruhusu uongozi wa vijiji kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ambavyo viliwanufaisha wafanyakazi na mameneja wa viwanda hivyo ambavyo havikuwa mali ya serikali kuu. Mwaka 1980 China ilifungua eneo moja la Shenzen kilichokuwa kijiji kidogo cha wavuvi na kukifanya eneo maalum la uchumi ambapo wawekezaji kutoka nje waliruhusiwa kuanzisha viwanda.

Eneo la Shenzen lilikuwa na wakazi laki 3 mwaka 1980. Sasa limekuwa jiji kubwa la watu zaidi ya milioni 10 na maarufu kwa uzalishaji wa kila aina ya bidhaa za viwandani. Sera ya kufungua maeneo na kukaribisha wawekezaji toka nje imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uzalishaji za bidhaa za viwandani na umeifanya China kuwa karakana ya dunia. Kwa nini China ilifanikiwa kukuza uchumi wake kwa kasi ya juu baada ya mabadiliko ya sera.

Ukuaji wa uchumi unaambatana na mabadiliko ya mfumo wa uchumi kutoka kutegemea sana kilimo na kuelekea kwenye ongezeko la ajira viwandani, kutoka nguvu kazi inayoishi vijijini kuelekea nguvu kazi inayoishi mijini. Mabadiliko ya mfumo wa uchumi husababishwa na ushindani wa soko.

Serikali ya China ilikuza uchumi kwa kuruhusu ushindani wa soko na kuyapa fursa makampuni mapya yenye tija kuanza na makampuni yanayopata hasara kufilisika. Soko la ajira ukiacha mashirika ya umma liliruhusu makampuni mapya kuajiri wafanya kazi na makampuni yanayopata hasara kupunguza wafanyakazi. Sheria za kazi zilijikita katika kurahisisha uanzishwaji wa ajira. Ni vizuri kuwa na utaratibu wa hifadhi za jamii kwa wafanya kazi wanaopoteza ajira ili kupunguza makali na kuwepo kwa soko la ajira linalonyumbulika.

Wanaopoteza ajira wapate kipato cha kuwawezesha kuishi wakati wakitafuta ajira mpya. Katika kipindi cha mabadiliko ya mfumo wa uchumi, China haikuwa na mfumo mzuri wa hifadhi za jamii. Wafanyakazi wengi wanaotoka vijijini hawakuwa na huduma za jamii na vibali vya kuishi katika miji walioenda kufanya kazi. Kwa sababu ya ukosefu wa hifadhi za jamii, familia ziliwajibika kuweka akiba itakayowasaidia watakapougua na pia kuwaelimisha watoto wao.

Nchi yeyote haiwezi kuondokana na umaskini bila kukuza uchumi unaoongeza ajira. Katika suala la kukuza uchumi hakuna miujiza. Uchumi unakua kwa kuongeza elimu, ujuzi na utaalamu wa wafanyakazi, ongezeko la raslimali na vitendea kazi, na kuongezeka kwa ufanisi na tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma. Maendeleo ya teknolojia ndiyo yanayochea ukuaji wa uchumi. Kabla ya mapinduzi ya viwanda ya karne ya 18, maendeleo ya teknolojia yalitokana na uzoefu wa wakulima kwenye mashamba yao na mafundi kwenye karakana zao.

Baada ya mapinduzi ya viwanda maendeleo ya teknolojia na uvumbuzi ulitokana na majaribio ya maksudi na badae uliimarishwa na matumizi ya sayansi katika majaribio. Ukuaji wa uchumi wa nchi ambazo ziko mstari wa mbele wa maendeleo na matumizi ya teknolojia uvumbuzi wa teknolojia mpya au oboreshaji wa teknolojia ya zamani. Kasi ya uvumbuzi wa teknolojia mpya unategemea uwekezaji katika elimu ya sayansi, teknolojia na utafiti. Nchi ambazo ziko nyuma katika maendeleo ya uchumi na matumizi ya teknolojia zina fursa ya kutumia teknolojia ambayo tayari imeisha gunduliwa.

Kinachohitajika ni kutumia teknolojia iliyopo ukizingatia raslimali ulizonazo, nguvukazi yako na elimu na ujuzi wake na mazingira ya nchi yako. Wakati wa uongozi wa Mwenyekiti Mao, mkakati wa maendeleo ya uchumi ulijikita katika kuwekeza kwenye viwanda vizito na kujitosheleza bila kushiriki sana katika biashara za nchi za nje. Taratibu za uchumi wa soko hazikukubaliwa.

Lengo ilikuwa kujenga jamii mpya ya kikomunisti ambapo kila mtu alitegemewa achangie katika jamii kwa kuchapa kazi kwa kadri ya uwezo wake na jamii imuwezeshe kupata mahitaji yake muhimu sawa na wananchi wengine. Matumizi ya bei za soko na motisha kwa wafanyakazi vilionekana kuwa nyenzo za kibepari. Sera nyingine kama za Hatua Kubwa Mbele (The Great Leap Forward) na Mapinduzi makubwa ya utamaduni (The Great Cultural Revolution) yalileta vurugu na kusababisha kuanguka kwa uzalishaji.

Baada ya kufanikisha mapinduzi ya kikomunisti mwaka 1949 na kuanzia mwaka 1953 China ilianza kutekeleza mipango ya maendeleo ya miaka mitano. Mipango hii ilikuwa na lengo la kujenga viwanda vizito na kutumia utaratibu wa kiutawala wa kugawa raslimali, malighafi na nguvu kazi katika sekta za uchumi. Pamoja na upungufu wa tija katika uzalishaji, jambo moja ambalo China ilifanikiwa ni kuboresha huduma za afya na hasa huduma za kinga ya maradhi na kusambaza elimu ya msingi kwa wananchi wote.

Katika uongozi wa Deng Xiaoping, China ililegeza masharti ya biashara na ikaanza kuagiza bidhaa na teknolojia kutoka nje ili kusaidia kuleta maendeleo ya haraka ya uzalishaji viwandani. Ilianza kutumia vizuri fursa za kuwa nyuma na kuzalisha bidhaa katika viwanda vilivyoajiri watu wengi kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu, vifaa vya umeme na elektronoki.

Sehemu kubwa ya bidhaa za viwanda hivi viliuzwa nchi za nje. Ukuaji wa uzalishaji viwandani ulisaidiwa na ujenzi wa miundombinu imara ya kufua na kusambaza umeme, ujenzi wa njia za usafirishaji hasa barabara, reli na viwanja vya ndege. Sera za thamani ya sarafu ya China zilihakikisha kuwa bidhaa za China zinakuwa na ushindani mkubwa katika soko la dunia.

China haikusita kupunguza thamani ya sarafu yake ili kuongeza ushindani wa bidhaa zake katika soko la dunia. Thamani ya sarafu ya China ilishuka toka yuan 1.5 mwaka 1980 na kufikia yuan 8.6 mwaka 1994 kwa dola moja ya Marekani. Baada ya 1994 sarafu ya China ilikongomewa kwenye dola ya Marekani, yuan 8.3 zikiwa sawa na dola 1. Ushindani wa bidhaa za China katika soko la dunia uliongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa tija na ufanisi uliopunguza gharama za uzalishaji za China ukilinganisha na nchi nyingine.

Sera za China zimehamasisha uwekaji wa akiba na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi. Sehemu ya pato la taifa linalowekwa kama akiba limeongezeka toka wastani wa asilimia 37 katika kipndi cha miaka 1982 – 92 mpaka kufikia asilimia 50 katika miaka ya 2003 – 2010. Uwekaji mkubwa wa akiba umeiwezesha China kugharamia uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi mkubwa sana uliofikia wastani wa asilimia 42 kwa mwaka katika kipindi 2003 - 2011. Katika miaka 10 iliyopita ukuaji wa uchumi wa China umechochewa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje na uwekezaji wa raslimali na vitega uchumi ndani ya China.

Kwa kuwa China inauza bidhaa nyingi nchi za nje kuliko inazoagiza, imekuwa na ziada katika urari wa malipo ya nchi za nje na kwa hiyo kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni. Akiba ya fedha za kigeni ya China inazidi dola trilioni 3.2 sehemu kubwa ikiwa imewekwa Marekani. Tangu mwaka 2002, Marekani imekuwa inategemea akiba ya China kuziba pengo la nakisi ya bajeti ya serikali. Hivi sasa China inashinikizwa ibadilishe sera, iongeze thamani ya sarafu yake na kuongeza matumizi ya kawaida ndani ya nchi na kupunguza uwekaji mkubwa wa akiba ili inunue bidhaa nyingi kutoka nje na ipunguze uuzaji wa bidhaa zake nchi za nje.

Sera ya Ujamaa ya Tanzania ilishawishiwa sana na ujamaa wa China. China ilipoanza kubadili sera mwaka 1978, Tanzania iliendelea kusisitiza msimamo mkali wa ujamaa kama ulivyoainishwa katika Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981. Mabadiliko ya sera Tanzania yalishinikizwa na mashirika ya kimataifa hususani IMF na Benki ya Dunia na wahisani wa nchi za magharibi baada ya uchumi luporomoka mwanzoni wa miaka ya 1980. Mabadiliko ya sera nchini China ulitokana na mapambano ya kisiasa na fikra ndani ya China yenyewe.

Deng alitumia ushauri hasa wa Lee Kuan Yew, Waziri Mkuu wa Singapore na wataalam wa Benki ya Dunia lakini Wachina wenyewe ndiyo walioendesha usukani wa mabadiliko. Utekelezaji wa sera za mabadiliko nchini Chinaulifanywa kwa majaribio. Mabadiliko ya sera za kilimo yalijaribiwa katika eneo dogo. Yalipoonekana kuwa na mafanikio yalisambazwa maeneo mengine. Ukaribishaji wa wawekezaji viwandani kutoka nje ulianza Shenzen eneo lilioko karibu na Hongkong na ulipofanikiwa maeneo mengine yaliruhusu uwekezaji toka nje.

China haikubinafsisha mashirika ya umma, bali hatua kwa hatua waliruhusu makampuni binafsi kuanzishwa na kushindana na mashirika ya umma. Sekta ya fedha na mabenki bado inashikiliwa na dola. Serikali ya China iliweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu na kwa hiyo kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa vitega uchumi katika sekta ya viwanda. Mambo muhimu tunayoweza kujifunza kutoka China.

Kwanza Watanzania wenyewe ndiyo tuendeshe usukani wa mabadiliko. Tujifunze toka uzoefu wa nchi nyingine lakini tusiendeshwe na wengine. Katika utekelezaji wa sera mpya serikali inapaswa kufanya majaribio eneo dogo, kujifunza kama sera ina mafanikio itekelezwa katika maeneo mengine. Kama haifai iachwe. Kwa mfano sera ya maeneo maalum ya uchumi itekelezwe vizuri katika eneo moja na kuona matunda yake badala ya kuanza maeneo mengi madogo madogo yasiyokuwa na miundombinu ya kutosha kama ilivyo hivi sasa.

Serikali ya China imeweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu. Kila inapowezekana China inatumia utaratibu wa wale wanaonufaika na huduma za miundombinu walipie huduma hizo. Tanzania inaweza kujifunza toka China kwa kukamilisha miradi ya miundombinu inayoanzishwa kabla ya kuanza mingine na kuwa na mipango ya ujenzi wa miundimbinu inayotekelezeka.

Sera za sarafu zinazohakikisha ushindani wa kibiashara ni muhimu katika maendeleo ya viwanda. Hata hivyo izingatiwe kuwa ongezeko la tija na ufanisi katika uzalishaji liambatane na sera ya sarafu inayohakikisha ushindani wa kibiashara. Tanzania inaweza kutumia fursa zilizopo katika kuwa nyuma katika maendeleo ya uchumi na teknolojia. Ikiwa tutajipanga na kutumia teknolojia iliyopo tunaweza kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji kama walivyofanya Wachina. Mfumo wa soko unaofanya kazi kwa ufanisi ni sharti muhimu la kuchochea ukuaji wa uchumi unaoongeza ajira. Bei ya bidhaa na mishahara ya nguvu kazi iambatane na upatikanaji wake.

Uongozi wenye dira na uliyo tayari kujifunza na serikali madhubuti ndiyo msingi wa kujenga uchumi unaoongeza ajira. Changamoto ya ziada kwa Watanzania ni kupata uongozi wenye dira na serikali madhubuti kwa njia za kidemokrasia ili tuweze kujenga uchumi utakaoleta neema kwa Watanzania wote.

Katika mahusiano yetu ya biashara na uwekezaji ni muhimu kwa Tanzania kuwa na sera na mpango madhubuti ya uwekezaji wa miundo mbinu na kuusimamia ipasavyo. Misaada ya China itusaidie kutekeleza mpango wetu. Tatizo ni udhaifu mkubwa wa mipango yetu. Serikali imekuwa na mipango mingi isiyo tekelezwa au kutekelezeka.

Kuna Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ambayo inalenga kuwa Tanzania iwe ni nchi yenye kiwango cha kati cha mapato (middle income country) na hali bora ya maisha kwa wananchi. Mpango Maalum wa Kuharakisha Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Mini Tiger Plan 2020) ambao haijulikani umeishia wapi.

Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania – MKUKUTA I na MKUKUTA II na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2010-15. MKUKUTA I na MKUKUTA II hazikufanyiwa makadirio ya gharama za utekelezaji wake. Gharama za mpango wa miaka mitano ni kubwa mno na serikali haina fedha ya kuugharamia. Serikali imevamia mkakati mwingine wa Big Results Now.

Lazima tuwe na mkakati wetu wa kujenga viwanda. Tanzania isiwe chanzo cha malighafi tu za kuuza China. Gharama za uzalishaji viwandani katika nchi ya China zinaongezeka na ajira ya watu milioni 90 inategemewa kuhamia nchi nyingine. Ni vyema Tanzania ikajipanga kuwa nchi itakayoweza kuongeza ajira kwa wingi kwa shughuli za uzalishaji viwandani zinazohama toka China.

Tunapaswa kutenga eneo kubwa la kilomita za mraba 100- 200 karibu na bandari ya Tanga na Mtwara na kwa kushirikiana na sekta binafsi kulisheheni miundombinu na kulifanya kuwa eneo maalum la kuendeleza viwanda vya kuuza bidhaa nch za nje. Wawekezaji wa ndani na nje wajengewe mazingira mazuri yanayovutia kuwekeza na kuongeza ajira. Wawekezaji toka China watumie wafanyakazi wa Tanzania na siyo kuleta wafanyakazi toka China kwa shughuli zinazowezwa kufanywa na Watanzania.

Serikali iwe makini na kuhakikisha hatuleti Wawekezaji matapeli kama muwekezaji wa Ujenzi wa Terminal ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Ulinzi wa mazingira uzingatiwe katika uwekezaji wa viwandani na katika uvunaji wa maliasili yakiwemo madini.

China ni taifa kubwa litakalokuwa na uchumi mkubwa kuliko nchi zote duniani katika miaka 20 ijayo. Tanzania tujipange vizuri kuwa na mahusiano ya kiuchumi na China yatakayokuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba

Mwenyekiti wa Taifa

Prof. mbona anaji dhalilisha!!?? Mikataba mbona ilisha sainiwa siku nyingi leo ndio anapiga kelele kwamba tunufaike!!! Jamaa amekuja kuona kile walicho saini kwamba utekelezaji wake umefikia wapi. Si mlisha ona bomba la gas na mambo ya Kinyerezi? Ndiyo imesha kula kwetu hiyo. Si watu walisha enda China siku nyingi tu!! Mtashangaa na macho yenu.
 
JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:51 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ameonya tabia ya kuingia mikataba yenye mazingira ya siri na makampuni kutoka nchini China, kuwa inaweza kuendelea kulitia aibu Taifa.

Alitolea mfano aibu iliyoikumba nchi kutokana na usiri huo huo kuwa ni mkataba kati Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya China Communications Construction Company (CCCC).

Kwa mujibu wa Lipumba, aibu hiyo ilimfanya Rais Jakaya Kikwete, alazimike kuvunja Baraza la Mawaziri kutokana na kashfa iliyokuwa ikiwakabili mawaziri wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu ujio wa Rais wa China, Xi Jinping, anayewasili leo, Prof. Lipumba ambaye pia ni Mtaalamu wa Uchumi, alisema ni wazi Tanzania imekuwa ikijikuta katika aibu kutokana na usiri huo wa mikataba ya miradi ya maendeleo inayoiingia na wawekezaji wa makampuni kutoka China.

Profesa Lipumba, alisema ziara hiyo ya Rais wa China inatakiwa kutumiwa kama fursa ya pekee kwa Taifa na isiwe majuto kwa Watanzania ambao kila siku wamekuwa wakiwashangilia wawekezaji ambao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

“Ukweli ulio wazi katika nchi nyingi za Afrika kumekuwa na manung’uniko makubwa kuwa bidhaa kutoka China zinaua viwanda vya Afrika, ikiwemo makampuni kutoka China, yanayowekeza katika katika sekta ya madini na yale yanayoshiriki katika ujenzi wa miundombinu, hasa ya barabara.

“Hivi karibuni nchi yetu ilishuhudia aibu kwa waliokuwa waziri wa Uchukuzi na Naibu wake kulumbana hadharani kuhusu ujenzi wa gati namba 3. Ni wazi ziara hii ya Rais Xi Jinping tunajua kuna mikataba zaidi ya 17 ambayo itasainiwa mbele yake pamoja na Rais Jakaya Kikwete,” alisema Profesa Lipumba.

Kwa mwenendo huo pamoja na malalamiko ya Watanzania, Prof. Lipumba alisema ni muhimu kwa mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje, kufanya uhakiki wa kina kuhusu kampuni zinazopewa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aksante Mwenyekiti Mchumi... tunahitaji TRANSPARENCY Kwanini kila kitu na CHINA ni USIRI SIRI??? Lazima CHAMA TAWALA - CCM wawe WAJIBIKAJI... na Wasijisahau; Watafuatwa Mpaka Makaburini Mifano IKO MINGI DUNIANI... Mali ya Wananchi Masikini sio rahisi kuibiwa...
 
Nina imani wataalamu watakuwa wamepitia vipengele vyote vya mikataba yote utakayosainiwa ili kuepuka ulaghai kama avyopelekwa kabaaang chief Mangungo!!
 
Sultan Mangungu of Burger-heart is a joker himself, equally surrounded by jokers and fraudulent vulture ambao wanajali zaidi matumbo yao, when it comes Tanzanian interest, you can count more on some faction of the mzunguz (ref. Sakata la rada, ambapo mpaka leo hii, serikali ya Sultan huyu haija-acknowledge kwamba kuna kosa limetendeka achilia mbali kumchukulia hatua za kisheria yeyote) than this pompous comical excuse of a 'president'.

Furthermore, ni vigumu kujua mikataba ni fwamba kwa sababu ya ukihiyo au rushwa za suti au vyote kwa pamoja..yetu macho/
 
Hivi huu U-Prof maana yake ni nini? Mbona Mikataba ilisha tiwa sahihi siku nyingi!! Au hapo Kinyerezi kwa ajili ya Gas vilivyo anza kujengwa mkataba wake ni wa nchi gani?

Na kule watu walipo safiri usiku kwa usiku mikataba yake ilikuwa ni ya nchi gani? Ngoja tugeuzwe mazuzu, tukija zinduka wenzetu walisha kimbilia Uswizi kula penshini zao.
 
Only in Tanzania.... mikataba inasigniwa sasahv usk saa3 kasoro mikataba 17....why usk? kesho hawa mawaziri watakuwa wanafanya nn? maana marais wako wanatizama tu....
 
viwanda kibao sana vitakufa hapa kwetu maana ushindani kati yetu na china gap kubwa sana na bidhaa zao zaingia sana hapa kwetu
 
Hivi hiyo mikataba wamepata muda wa kuisoma kweli hawa mburula wa kitanzania?
 
Back
Top Bottom