CUF: Unafiki wenu ndio anguko lenu

Chadema ni chama cha kanisa tu muna wasi wasi na ccm kuweka raisi muislamu ndio hasira zote muna ona maslahi ya kanisa yanahatarishwa.
kwani kuna ushahidi majimbo mengine mulishirikiana na ccm kuchakachuwa matokeo ili cuf isishinde

Kwa hiyo ni chama kipi ni cha msikiti tu? Unadhani CCM wataweka mgombea U-Raisi Muislam?

Hayo majimbo ambayo CCM ilishirikiana na CDM ili CUF isishinde ni ni yapi?

Na je Zanzibar CDM imeshirikiana na CCM pia?

Naweza nikawa natumia nguvu nyingi ya kufikiri kujadiliana na mtu ambaye haelewi anachokisema na hajui anachokiandika....niondoe wasiwasi kwa kunieleza 'muna' 'muna' ni kiswahili cha wapi?
 
Nawasalim WanaCUF,
Bila kung'ata wala kumung'unya maneno ninyi ni wanafiki. Wanafiki sana.
Kwa nini nawashutumu? Kwa sababu tabia ya unafiki haijifichi. Hata kama wengine wote hawaioni ila mwenye tabia anajua kwamba anachofanya ni unafiki.Mnawashutumu CDM kwamba ni kikwazo cha upinzani. Mnasema CDM wanadharau maamuzi ya ya wazanzibari kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.Mara mnakurupuka na kusema mnaenda kuwashtaki CCM kwa wananchi. Wananchi wapi? Watanzania Bara peke yake au pamoja na Visiwani?Hayo mnayoenda kuwashtakia kwa wananchi, i.e. Malipo ya dowans, bei za bidhaa, mgawo wa umeme, nk wananchi wanaishi nayo. Wanayajua. Pia CDM wameshawaambia. Lakini, kama CCM ndio chanzo, ni huku Bara peke yake? CCM wameshindwa Bara peke yake? Visiwani mnamshtaki nani?Hapa ndipo unafiki unapokuwa wazi. Hakuna asiyeuona unafiki wenu. Visiwani ninyi ni serikali. Matatizo ya wananchi mnatakiwa kuyatatua kama serikali. Hicho ndicho mlichokubaliana na CCM. Huku Bara ninyi ni upinzani mkishirikiana na TLP, NCCR na UDP. Mnapinga au kukosoa wanayofanya CCM. Mnajidai kutokuona tatizo hapo.Hata kama muungano una matatizo hii nchi bado ni moja. Hatuna serikali tatu.Tuna serikali mbili. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakilishwa kwenye Serikali ya Jamhuri. Kwa hiyo mpo kwenye Serikali.Je mnataka tuamini mnaenda kujishtaki au hamna uwezo wa kuleta mabadiliko mkiwa ndani ya serikali yenu? Mnataka kuwa serikali na upinzani kwa pamoja?Huwezi kula keki yako na kubaki nayo; you can not eat your cake and have it.CUF, you have made a political mistake and error. Rectify it. The train is moving. Acheni kuwa wanafiki. It will push this country further down the abyss.

CDM Wanapogoma Kushirikiana na CUF, CUF wanaona wanaonewa...lakini mimi sijui kwa nini Lipumba anaendelea kuwa Kiongozi wa CUF ya Bara na Visiwani. Kwa Muundo wa Serikali ya Nchi yetu HAIKUTAKIWA KABISA CUF KUSHIRIKIANA NA CCM kwa Upande mmoja na iendelee Kuipinga CCM Kwa Upande mwingine. CUF Imejiondolea Sifa ya Kuwa Chama cha Upinzani kwa Kuwa kinazikubali sera za CCM Huko Zanzibar ambazo ndo sera hizohizo za Muungano....But Siwalaumu sana Kwa Kuwa Maalimu SEIF Siku Hizi kaanza Kupendeza...Njaa Ilimchosha saana na ndevu zilikuwa zimeanza Kunyonyoka! Thank God kwa Sasa anakula Vizuri na labda Lipumba pia Mwaka 2015 Attajiunga na CCM akiona mwenzake kamzidi kula! Any way MNAFIKI NI MNAFIKI TU!
 
Kwa hiyo ni chama kipi ni cha msikiti tu? Unadhani CCM wataweka mgombea U-Raisi Muislam?

Hayo majimbo ambayo CCM ilishirikiana na CDM ili CUF isishinde ni ni yapi?

Na je Zanzibar CDM imeshirikiana na CCM pia?

Naweza nikawa natumia nguvu nyingi ya kufikiri kujadiliana na mtu ambaye haelewi anachokisema na hajui anachokiandika....niondoe wasiwasi kwa kunieleza 'muna' 'muna' ni kiswahili cha wapi?
Mkuu.
kama nilivyosema mwanzoni.malumbano na kuitana majina ni yenu CHADEMA na CUF.
Hilo la Kiswahili ndio nitajaribu kutoa mchango.

Mimi nina wasiwasi. ....sisi tuna wasiwasi ............mimi ninaona
Wewe una wasiwasi. ninyi, nyinyi muna wasiwasi. .........ninyi munaona
yeye ana wasiwasi. ....wao wana wasiwasi.

Kama ni mtumia muna basi imo katika kiswahili sanifu.
Kama umeona inatumika visivyo basi ni vyema umueleweshe huyo mtumiaji, mwandishi.

Mkuu..nimefurahi kuona bila ya kuuma maneno umeanza kuitamka Tanganyika.
We all should do the same!
 
NONE CAN EXPLAIN IT MORE CLEARLY THAN THIS!!
Watanzania (Tanganyika na Zanzibar) tu wanafiki na unafiki wetu ndio umetufikisha hapa na hatutanasuka hata nusu hatua moja mbele ikiwa hatutawacha kuwa wanafiki.
 
nimeona madiwani wa cuf mwanza, nimeona madiwani wa cuf musoma ( mara), nimeona madiwani kagera, kumbe wapemba wengi. hapo kwenye red tufahamishe vizuri wewe chadema-kata

Hao madiwani wa cuf hawako Mwanza nzima, wala Mara nzima wala Kagera nzima ni kwa baadhi tu ya maeneo ya mikoa hiyo. Ingekuwa vizuri ungetaja idadi ya madiwani kwa kila mkoa kati ya hiyo uliyoitaja kuwa ina madiwani wa cuf. Kwa mantiki hiyo hayo maeneo machache "yenye madiwani wa cuf" ina maana yana wapemba wengi.

Kama si hivyo mbona hutaji suala la ubunge? Kwa nini cuf haina wabunge katika maeneo hayo uliyoyataja? Au wabunge sio viongozi?
Samahani kwa kuwaingilia mjadala wenu.
 
CCM walibobanwa mbavu na CUF wakawategea mtego mdogo wa kuwaonjesha utamu wa madaraka, waliwatega hivyo kwa sababu wanajua kuwa viongozi wengi wa CUF walikuwa viongozi serikalini hivyo wanajua utamu wa madaraka ukoje, Jamaa hawakufanya uamuzi kwa kuzingatia kizazi cha sasa na kijacho wao waliona wameteseka sana kupambana na CCM sasa wakikataa hata offer ndogo waliopewa wanaweza kukusa kabisa wakakubali. Matokeo yake wamekuwa sehemu ya serikali hivyo wao ni chama tawala, hawawezi kujikosoa, na wakiangalia madaraka matamu hivyo wameona bora kumtumikia kafir wapate mradi wao.
Je 2015 SEIF na CUF yake watasema CCM hawaletea wananchi maendeleo au? maana wao ni serikali ndio maana wenzao CDM wanasema maisha magumu ghafla wamekuwa watetezi kuwa eti hiyo ni hali ya dunia. wenzao wakiandamana wao wanasema wahaini sababu maslahi ya CCM yakiporwa yameporwa ya CUF pia.

CUF mlitegwa nanyi mkanasa hivyo mmeshakuwa watumwa wa CCM kila ngoma watakayo piga nyinyi lazima mcheze, watoto wa mjini wanasema imekula kwenu
 
Mkuu.
kama nilivyosema mwanzoni.malumbano na kuitana majina ni yenu CHADEMA na CUF.
Hilo la Kiswahili ndio nitajaribu kutoa mchango.

Mimi nina wasiwasi. ....sisi tuna wasiwasi ............mimi ninaona
Wewe una wasiwasi. ninyi, nyinyi muna wasiwasi. .........ninyi munaona
yeye ana wasiwasi. ....wao wana wasiwasi.

Kama ni mtumia muna basi imo katika kiswahili sanifu.
Kama umeona inatumika visivyo basi ni vyema umueleweshe huyo mtumiaji, mwandishi.

Mkuu..nimefurahi kuona bila ya kuuma maneno umeanza kuitamka Tanganyika.
We all should do the same!

Nonda, nakumbuka the post uliyoweka hapa ambayo kwa kiasi fulani imechagia sana kunifanya nifikirie kwanini jina Taganyika 'lilikufa' na Zanzibar likabaki. Nagundua kwamba ingawaje lengo lilikuwa Tanganyika isiwepo kwa jina lakini nchi ilibaki.

Najua unafahamu tafsiri ya nchi ni nini. Turudi kwenye tafsiri hiyo.
 
Hao madiwani wa cuf hawako Mwanza nzima, wala Mara nzima wala Kagera nzima ni kwa baadhi tu ya maeneo ya mikoa hiyo. Ingekuwa vizuri ungetaja idadi ya madiwani kwa kila mkoa kati ya hiyo uliyoitaja kuwa ina madiwani wa cuf. Kwa mantiki hiyo hayo maeneo machache "yenye madiwani wa cuf" ina maana yana wapemba wengi.

Kama si hivyo mbona hutaji suala la ubunge? Kwa nini cuf haina wabunge katika maeneo hayo uliyoyataja? Au wabunge sio viongozi?
Samahani kwa kuwaingilia mjadala wenu.

Mkeshaji,

Hujaingilia mjadala. Mawazo yako ni muhimu katika lolote linalozungumzwa. Usikae pembeni, pale ambapo unaona yeyote kati yetu ameruka mstari changia.
 
Kuna watu wana taka taka za akili na huyu Msando Alberto ni mmoja wao.
Nani mnafiki kati ya chadema na CUF? hebu jiulize:

Kwa vipi chadema wanashikilia kuwa CUF kufanya serikali ya umoja wa kitaifa na CCM imekuwa si chama cha upinzani (hawajuwi kama ni mnyama au ndege), leo hao hao chadema wanasema wanataka na Tanzania bara iundwe serikali ya umoja wa kitaifa, wanamaanisha nini na kama si unafiki kitu gani?

Leo chadema wanasema hawamtambuwi rais Kikwete kama rais halali, na alipoingia bungeni kuhutubia walitoka wote, lakini hao hao wakarudi kuchangia hotuba yake ile ile ambayo waliigomea kuisikiliza, kama huu si unafiki na uzandiki ni kitu gani?
 
Nawasalim WanaCUF,

Bila kung'ata wala kumung'unya maneno ninyi ni wanafiki. Wanafiki sana.

Kwa nini nawashutumu? Kwa sababu tabia ya unafiki haijifichi. Hata kama wengine wote hawaioni ila mwenye tabia anajua kwamba anachofanya ni unafiki.

Mnawashutumu CDM kwamba ni kikwazo cha upinzani. Mnasema CDM wanadharau maamuzi ya ya wazanzibari kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.

Mara mnakurupuka na kusema mnaenda kuwashtaki CCM kwa wananchi. Wananchi wapi? Watanzania Bara peke yake au pamoja na Visiwani?

Hayo mnayoenda kuwashtakia kwa wananchi, i.e. Malipo ya dowans, bei za bidhaa, mgawo wa umeme, nk wananchi wanaishi nayo. Wanayajua. Pia CDM wameshawaambia.

Lakini, kama CCM ndio chanzo, ni huku Bara peke yake? CCM wameshindwa Bara peke yake? Visiwani mnamshtaki nani?

Hapa ndipo unafiki unapokuwa wazi. Hakuna asiyeuona unafiki wenu. Visiwani ninyi ni serikali. Matatizo ya wananchi mnatakiwa kuyatatua kama serikali. Hicho ndicho mlichokubaliana na CCM.

Huku Bara ninyi ni upinzani mkishirikiana na TLP, NCCR na UDP. Mnapinga au kukosoa wanayofanya CCM. Mnajidai kutokuona tatizo hapo. Hata kama muungano una matatizo hii nchi bado ni moja. Hatuna serikali tatu.

Tuna serikali mbili. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakilishwa kwenye Serikali ya Jamhuri. Kwa hiyo mpo kwenye Serikali.

Je mnataka tuamini mnaenda kujishtaki au hamna uwezo wa kuleta mabadiliko mkiwa ndani ya serikali yenu? Mnataka kuwa serikali na upinzani kwa pamoja?

Huwezi kula keki yako na kubaki nayo; you can not eat your cake and have it.

CUF, you have made a political mistake and error. Rectify it. The train is moving. Acheni kuwa wanafiki. It will push this country further down the abyss.

cuf ni wanafiki wameshachoka hawana jipya uliwahi kuona wapi uhaini unafanyika kwenye mikutano ya hadhara watafute cha kufanya bara siasa imeshawashinda:gossip:
 
Nonda, nakumbuka the post uliyoweka hapa ambayo kwa kiasi fulani imechagia sana kunifanya nifikirie kwanini jina Taganyika 'lilikufa' na Zanzibar likabaki. Nagundua kwamba ingawaje lengo lilikuwa Tanganyika isiwepo kwa jina lakini nchi ilibaki.

Alichofanya Nyerere ni kama mbinu alizotumia mama mmoja wa kambo aliyekuwa na mtoto wake mmoja (dhana ya Tanganyika) na watoto wawili wa mume wake (dhana ya Tanzania na Zanzibar). Alichofanya ni kuonesha kuwapenda sana watoto wa kambo, kiasi kwamba alikuwa anawapa chungwa moja kila mmoja kwa mfano, na kuwaambia wamgawie ndugu yao nusu. Hatimaye mwanawe akawa anaambulia 1/2+1/2 =1, wakati wale wa kambo wanabakia na 1/2 tu kila mmoja.
 
Ndio maana huwa nawalaumu waandishi wetu wa habari na watangazaji wa TV zetu. Wangekuwa na uwezo (academically I guess) wangetusaidia kutengeza ajenda ya kitaifa kwa kuuliza hawa wanasiasa maswali magumu na ku-run polls za maana. Sina hakika sana viongozi wangapi wa CUF wanaingia humu lakini Prof Lipumba angeulizwa maswali magumu na follow up questions, mithili ya yale yaulizwayo katika 'Hard Talk' ya BBC kuhusu msimamo wa CUF katika maswala ya maandamano ya CDM na msimamo wa CDM juu ya CUF kuungana na CCM na tena kutaka kuungana na CDM. Msando ndugu yangu maswali yako, kama yetu wengine, hayatapata majibu, sana sana watababaisha na kudanganya watu tu bure.
 
chatu dume "nimeona madiwani wa cuf mwanza, nimeona madiwani wa cuf musoma ( mara), nimeona madiwani kagera, kumbe wapemba wengi. hapo kwenye red tufahamishe vizuri wewe chadema-kata"

Njoo mwanza CUF wana diwani mmoja wa kata ya Mirongo ambayo iko kati kati ya jiji la mwanza na mitaa inayounda hiyo kata ni Unguja, rufiji, Uhuru nk, ana angalia wakazi wengi wa mitaa hiyo ni watu gani maana majina tu ya mitaa yanakutambulisha , my brother dont shout as if you have never been to school, CDM alaways huwa hatuongei kama hatuna ushahidi, ni sera na ipo kwenye katiba ya CDM, tofauti na nyinyi CCM,CCMb ambao Umakamba na Umatatiro umewajaa ( uropokaji na ukurupukaji)
 
Junius,

Inawezekana mimi ni mmoja wa wenye akili takataka kama wewe. Lakini angalau naweza kukushangaa kwamba hoja yako ni 'nani mnafiki zaidi kati ya CDM na CUF'.

Hata kama ningekuwa nakubaliana na wewe nisingefika huko. Ni sawa useme umuulize rafiki yako 'mimi na wewe na mjinga zaidi wakati wote wajinga'.
 
Kwanza asante sana kwa hiki kiunganishi. Lakini mada hii ilikusudiwa kuwachonoa wana CUF watoe majibu. Kiunganishi ulichotuwekea ni cha Wazanzibari wanajadili katiba mpya, hivyo unaposema Hawa wameanza unakusudia nani? CUF au Wazanzibari? Ikiwa ni CUF, Wazanzibari wote ni CUF au CUF ni Wazanzibari?
Mkuu.
Hiyo link ilikusudiwa kwa MsandoAlberto...kama umesoma katika moja ya mchango wake alisema anajipanga aje na mada ya Muungano.Nilikutana na hiyo link niliyoiweka na nilitaka yeye achungulie huko, pia ilikuwa kumwambia kuwa kama yeye anajipanga basi watu wameanza kujadiliana na kulumbana katika hiyo link. yaani wanaJF waliochangia katika hiyo mada.
 
Nonda, nakumbuka the post uliyoweka hapa ambayo kwa kiasi fulani imechagia sana kunifanya nifikirie kwanini jina Taganyika 'lilikufa' na Zanzibar likabaki. Nagundua kwamba ingawaje lengo lilikuwa Tanganyika isiwepo kwa jina lakini nchi ilibaki.

Najua unafahamu tafsiri ya nchi ni nini. Turudi kwenye tafsiri hiyo.

Mkuu,
Kuna sehemu nilikutana na mada kuhusu muungano. Mzanzibari aliandika hiyo mada.Alisema kuwa kilichofanyika katika kuunda muungano ilikuwa ni Tanganyika kujiongezea eneo.(nikiiona tena nitarudi kukuwekea link)

Na hapa inaonesha unataka niamini hivyo. Hata hivyo nimependa kuwa umechukua muda kufikiri sana. Nahisi wanaJF wengine hawajakiona kitu hicho na ndio sababu wanawakejeli sana Wazenj wanapokuja na malalamiko yao.
Nafikiri pia ndio sababu CCM wameufanya Muungano kuwa ni taboo. Wengi wakijua kinachoendelea watabaki kimya kama CCM.
Lakini ,Msando kama umegundua hili basi nafikiri hatupaswi kubariki "unafiki".

Tuusemee na tuuoneshe kwa umma. Kwa sababu tumo kwenye mchakato wa EAC na sisi kama TZ hatutapenda kufanyiwa ujanja na nchi member katika nchi zinazounda EAC au vipi?

sasa vipi, bado unajipanga na utakuja na mada yako au joto limepungua? sio muhimu tena?
 
Hao madiwani wa cuf hawako Mwanza nzima, wala Mara nzima wala Kagera nzima ni kwa baadhi tu ya maeneo ya mikoa hiyo. Ingekuwa vizuri ungetaja idadi ya madiwani kwa kila mkoa kati ya hiyo uliyoitaja kuwa ina madiwani wa cuf. Kwa mantiki hiyo hayo maeneo machache "yenye madiwani wa cuf" ina maana yana wapemba wengi.

Kama si hivyo mbona hutaji suala la ubunge? Kwa nini cuf haina wabunge katika maeneo hayo uliyoyataja? Au wabunge sio viongozi?
Samahani kwa kuwaingilia mjadala wenu.

Mkuu naona umekurupuka ulikuwa umelala? nadhani ungemuuliza huyo Chadema-kata niliomjibu anasema sehemu yoyote kwenye madiwani wa CUF kuna wapemba, naomba umjibu mwenzio
 
chatu dume "nimeona madiwani wa cuf mwanza, nimeona madiwani wa cuf musoma ( mara), nimeona madiwani kagera, kumbe wapemba wengi. hapo kwenye red tufahamishe vizuri wewe chadema-kata"

Njoo mwanza CUF wana diwani mmoja wa kata ya Mirongo ambayo iko kati kati ya jiji la mwanza na mitaa inayounda hiyo kata ni Unguja, rufiji, Uhuru nk, ana angalia wakazi wengi wa mitaa hiyo ni watu gani maana majina tu ya mitaa yanakutambulisha , my brother dont shout as if you have never been to school, CDM alaways huwa hatuongei kama hatuna ushahidi, ni sera na ipo kwenye katiba ya CDM, tofauti na nyinyi CCM,CCMb ambao Umakamba na Umatatiro umewajaa ( uropokaji na ukurupukaji)

Mkuu Chadema-kata nashukuru kwa hoja zako murua, umetufumbua vichwa tunashukuru sana kwa hiyo Chadema ni chama rasmi cha Wakiristo tu? Mwanza hata mimi napajua vizuri sana, sasa wale Waislam waliopigia Chadema Kura, Waislam wa Kirumba, Nyegezi, Igogo, Mkuyuni, Nyamanoro, Rufiji, Nyakato, Pansiansi, Igoma, Uhuru, Mtakuja, Mbugani, Bugarika, Mabatini, wapo wengi sana leo wamekuwa wabaya? nyie ndio mnaichafua Chadema nadhani ata Dk Slaa akisoma posts zako lazima atapike, Unawafukuza Waislam Chadema, wewe Chadema-kata ni Jabber basi tena ni Insubstatial
 
HACHA KUKURUPUKA WEWE...CUF KUUNGANA NA CCM VISIWANI NI MAAMUZI YA W/NCHI NA SIO SHINIKIZO TOKA KWA MAALIM SEIF AU KARUME,KAMA HOJA YAKO NI KUBEZA MAAMUZI YA W/NCHI WA ZANZIBAR NJOO KWA hoJA HIYO NA SIO KURUKA RUKA NA KULETEA USHABIKI WA KISIASA HUSIO NA TIJA HATA KIDOGO.WA TZ TUPUNGUZE USHABIKI ZAIDI.....TUONGEE MAMBO YA MSINGI KUHUSU TAIFA LETU HUU USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA HAUNA MAANA YOYOTE...WEWE KAMA KIJANA TOA MITAZAMO YAKO JINSI TAIFA ILI LINAVYOTAKIWA KUONGOZWA NA TUFANYE NINI TUWE KAMA WENZETU WA NCHI ZA UGHAIBUNI.

BY METHOD
from UDOM
 
Back
Top Bottom