CUF: Unafiki wenu ndio anguko lenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Unafiki wenu ndio anguko lenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Mar 20, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawasalim WanaCUF,

  Bila kung'ata wala kumung'unya maneno ninyi ni wanafiki. Wanafiki sana.

  Kwa nini nawashutumu? Kwa sababu tabia ya unafiki haijifichi. Hata kama wengine wote hawaioni ila mwenye tabia anajua kwamba anachofanya ni unafiki.

  Mnawashutumu CDM kwamba ni kikwazo cha upinzani. Mnasema CDM wanadharau maamuzi ya ya wazanzibari kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.

  Mara mnakurupuka na kusema mnaenda kuwashtaki CCM kwa wananchi. Wananchi wapi? Watanzania Bara peke yake au pamoja na Visiwani?

  Hayo mnayoenda kuwashtakia kwa wananchi, i.e. Malipo ya dowans, bei za bidhaa, mgawo wa umeme, nk wananchi wanaishi nayo. Wanayajua. Pia CDM wameshawaambia.

  Lakini, kama CCM ndio chanzo, ni huku Bara peke yake? CCM wameshindwa Bara peke yake? Visiwani mnamshtaki nani?

  Hapa ndipo unafiki unapokuwa wazi. Hakuna asiyeuona unafiki wenu. Visiwani ninyi ni serikali. Matatizo ya wananchi mnatakiwa kuyatatua kama serikali. Hicho ndicho mlichokubaliana na CCM.

  Huku Bara ninyi ni upinzani mkishirikiana na TLP, NCCR na UDP. Mnapinga au kukosoa wanayofanya CCM. Mnajidai kutokuona tatizo hapo. Hata kama muungano una matatizo hii nchi bado ni moja. Hatuna serikali tatu.

  Tuna serikali mbili. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakilishwa kwenye Serikali ya Jamhuri. Kwa hiyo mpo kwenye Serikali.

  Je mnataka tuamini mnaenda kujishtaki au hamna uwezo wa kuleta mabadiliko mkiwa ndani ya serikali yenu? Mnataka kuwa serikali na upinzani kwa pamoja?

  Huwezi kula keki yako na kubaki nayo; you can not eat your cake and have it.

  CUF, you have made a political mistake and error. Rectify it. The train is moving. Acheni kuwa wanafiki. It will push this country further down the abyss.
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Beto CUF ilikufa siku nyingi, lete tamko la kikao au wewe huingi huko?
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  cuf ni giliba kwa wabara, kwa zanzibar-pemba saaaaaaaaafi. Ukombozi wa bara na tanzania (or tanganyika ) ya kweli ni kupitia CDM kwa hali ilivyo sasa!! Pengine upepo ubadilike baadae; lakini kwa sasa bado moto u CDM pekee!! Cuf wameonesha kujichanganya zaidi, na hasa wanapoanza kukosoa chama kingine cha upinzani hususan CDM na kuunga mkono ccm (ambao wanataka tena kuwashitaki kwa wananchi?????!!!!!)- lack of consistency!!
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu MsandoAlberto.

  Na mimi nakusalimia.

  Makala yako umeweka wazi unataka majibu kutoka kwa wa-CUF.

  Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Kwa hiyo haya ya ninyi CHADEMA na CUF kutupiana makombora na kuitana majina nawaachia wenyewe.

  Ila kuna kitu nimekiona katika post yako ambayo ningependa nichangie.
  Kwa maoni yangu naona hii dhana ya Tanzania ni nchi moja ni dhana potofu na haipaswi iwachwe iendelee. Kwa nini nasema hivi ?
  Tuanze kwenye jina lenyewe.Ni muunganisho wa majina mawili.Tanganyika na Zanzibar. Hizi ni nchi ngapi ? Jina Tanzania lilikuja miezi kadha baada ya Muungano.Muungano uliitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Usanii ni fani yetu.

  Haya kama hapo umepata jibu... safi sana.

  Pili, umepata kusikia wapi duniani nchi moja kuwa na serikali mbili ?

  Chukua mfano wa AU, EAC au EU..hizi ni umoja au muungano lakini hazina maana ya serikali moja au nchi moja.

  Lakini Mkuu wa serikali ya Tanganyika alitoa uwakala kwa serikali ya Muungano kufanya kazi pia za serikali ya Tanganyika.
  Mkuu wewe ni mwanasheria kitaaluma. Unapotoa uwakala huwa wewe ume-cease kuwepo kama entity ? Kwenye ule mkataba tunaombiwa ni wa Muungano kuna vipengele hivi.

  And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.
  (v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-
  (a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

  Mkuu huu mkataba halisi wa Muungano hata sijui umefichwa wapi. Basi hata copy ya Original hawataki kutuonesha. Sijui wanaficha nini hasa?

  Lakini Bwana MsandoAlberto, unaona hapo jina la nchi ambayo leo tunaiita "bara" au Tanzania bara? Kwa nini hatulitumii jina hili Tanganyika au wapi iliposemwa kuwa Tanganyika inabadilishwa jina na kuitwa "bara" au "Tanzania bara"?

  Juzi ulisema unaililia nchi ya babu na bibi zetu, halafu ukasema Tanzania.
  Unajitayarishaje kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi ya "Tanzania"?

  Mkuu..unafiki umekuwa ni sifa ya kila "mtanzania". Mambo yanafanya kinafiki. Siasa inaendeshwa kinafiki, hata fikra zetu zipo kinafiki kinafiki.

  Kwa hiyo huu utata wa Nchi ya Tanganyika na Zanzibar(Tanzania), utata wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania), Utata wa serikali ya Tanganyika kukasimu madaraka yake kwa Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Utata wa kuwepo serikali mbili katika nchi "moja"..Utata wa majina bara na visiwani.


  Utata wa kuwepo mamlaka tatu za sheria Tanzania. Utata wa kuwepo wizara za "bara" huku bara ambazo si wizara za Tanzania. Utata wa kuwepo kamati ya kero za Muungano ambayo ina wawakilishi wa upande wa Zanzibar na wa Tanzania huku wawakilishi wa Tanganyika wakikosekana.


  Sheria ya vyama vya siasa ambayo inataka kila chama kiwepo pande zote mbili za Muungano, yaani kiwepo Tanganyika na Zanzibar. Mkuu orodha ya unafiki wetu ni ndefu.


  Kwa hiyo hapa hakuna wa kumuoneshea mwenzake kidole!


  Mambo yamekorogeka mno kiasi ambacho tunashindwa kuchanganua nini ni nini. Hatuwezi tena kuwa rationale kwa sababu rationality haifanyi kazi tunapofanya mambo yetu badala yake ni unafiki tu na kuendelea kulikoroga.


  Tuhimizane tuache unafiki ili tutengeneze nchi zetu na umoja wetu au Muungano wetu. Wenzetu wanatucheka.


  Natumai nimekuchokoza kifikra.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,782
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  Nonda,

  ..nadhani kuna watu ama wameshindwa kuelewa hoja za CDM, au wameamua kuzipotosha.

  ..msimamo wa CDM unaeleweka kwamba wanataka serikali 3. huo pia ndiyo msimamo wa CUF.

  ..wanachodai CDM, and particularly Tundu Lissu, ni kwamba mabadiliko ya katiba yaliyotokea Zenj, yameongeza mkanganyiko/"unafiki" ktk suala zima la muungano wetu.

  ..Tundu Lisso alieleza wazi, nenda kasikilize hoja zake pale Nkrumah Hall, kwamba mabadiliko ya katiba Zanzibar yanaongeza nguvu kwa hoja kwamba TUNAHITAJI KATIBA MPYA, siyo kutia viraka.

  ..hoja ya CDM na Tundu Lissu ni kwamba muungano unaongozwa zaidi na "MAZOEA" badala ya kuongozwa na SHERIA na KATIBA.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Joka kuu.

  Nilipoandika mchango wangu hapo juu ilikuwa ni kumwambia Mkuu Msando kuwa "unafiki" unaonekana katika kila kitu tunachokifanya TZ katika broader meaning na mimi sikujikita katika siasa za vyama vya CDM na CUF.

  Katika siasa ya vyama mimi ningependa sana kuona CDM na CUF wanafanya kazi pamoja ili kuibwaga CCM iwe ni rahisi zaidi.
  Kwa hali ilivyo ni wazi CCM itaendelea kupigwa mweleka katika kila Uchaguzi Zanzibar na kama CDM wataibwaga CCM "bara" basi mchezo wa CCM utakuwa umekwisha.
  Chukua scenario ya CDM wameshinda Tanganyika na CUF wameshinda Zanzibar. Na CCM ikasita kuwa king'ang'anizi. Nini kitaendelea baada ya hapo?

  Kwa msisitizo wa MsandoAlbert Tanzania ni nchi moja sasa kwa nini CDM haioni ulazima au umuhimu wa kuwa na nguvu kule Zanzibar pia? Au ndio kuthibitisha kauli ya CUF kuwa CDM inawadharau wazanzibari?

  Mkuu nimesoma makala ya Lissu na ile ya Awadh pia. Hata bila ya Mabadiliko waliyofanya wazanzibari basi katiba mpya ilikuwa ni kitu cha muhimu na lazima kwa "amani na utulivu" na mustakabali mwema wa nchi. Ingependeza sana kama Lissu angekuwa na ujasiri pia wa kusema mabadiliko yaliyomuuondoshea Umakamo rais rais wa Zanzibar yalikwishavunja Muungano na haya mabadiliko waliyofanya wazenj ni kungongomelea msumari wa mwisho tu katika jeneza la Muungano ningemuelewa zaidi.

  Lakini Jokakuu tusiiteke mada ya watu…na sisi tusiendeleze "unafiki" tuwaache WanaCUF waje wajadiliane au walumbane na MsandoAlberto. Mimi nilitaka kumchokoza kifikra Msando tu katika "bara" = Tanganyika na hili la Tanzania ni nchi moja.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  cuf ni kenge katika msafara wa mamba. kuwajadili ni kupoteza muda.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,782
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  Nonda,

  ..nadhani CDM au vyama vya upinzani kutojitangaza Zanzibar is nothing but NUMBERS GAME.

  ..pia kuna suala la "historia" ambalo limejikita sana Zanzibar na kusababisha kuwa vigumu kwa chama kipya kujitangaza huko.

  ..kwa upande wa Tanganyika uwanja wa kisiasa uko more open, pia kuna idadi kubwa sana ya wapiga kura.

  ..sasa kwanini CUF haijitangazi huku Tanganyika kwa nguvu ileile inayotumika kule Zanzibar?

  ..hii hoja ya kutojitangaza upande wa pili wa muungano nadhani inawaelemea zaidi CUF kuliko chama chochote kile cha upinzani.

  ..binafsi ningependa CUF na CDM waache kushambuliana kwa wakati huu. mazingira hayo yatatoa nafasi ya wao kuweza kufanya kazi pamoja in the future.

  NB:

  ..wakati naelewa umuhimu wa kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kule Zanzibar, je CUF waliwafikiria wenzao wa Tanganyika wakati wanasaini makubaliano hayo?

  ..sasa hivi CUF-Bara wamekuwa kama yatima wa kisiasa. kuna wakati wanazungumza kama chama tawala, then ghafla wanageuka na kuzungumza kana kwamba ni wapinzani.
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nonda, umenena vizuri.

  Ila najua ulichofanya sio kunichokoza kifikra umetumia uwezo wako mkubwa kuniminya nitamke kile unachojua kiko moyoni mwangu.

  Mjadala wa muungano unakuwa wa kinafiki pia. Hatutaki kusema wazi kuna tatizo. Nakubaliana na yote ulioyasema. Kwa sababu nataka majibu ya wana cuf basi hili la muungano tulijadili tofauti. Ni vyema tukapasua jipu na kuweka wazi matatizo yalio wazi ya muungano. Tusing'ate maneno. Tuseme wazi wazi.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Arafat, mimi siingii humo. Nimeweka nadhiri kwamba nitabaki na Udiwani kwa kipindi chote na uongozi wa chama ubaki kwa wale ambao si viongozi wa wananchi. Naamini kwa hali hyo italeta ufanisi. Muda si mrefu tamko litawekwa jamvini
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CUF wamebaki jina tu na kuwajadili tutaonekana kama sisi hatuna akili
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu MsandoAlberto.
  Nia yangu ni kama nilivyoieleza; k ukuchokoza kifikra hakukuwa na ya zaidi ya hilo.

  Uwezo wangu ni mdogo sana mkuu, kama ule"mbu mbu mbu, mzungu wa reli"

  Shule kichwani ni shule ya kata. Lakini kwa changa moto uliyonipa hapa basi nitarudi shule ili kuongeza uwezo ili mminyo uwe mkali. LOL!

  Lakini umenidokolea hapa kuwa una mambo mengi unayoyafikiria juu ya jamii yetu. Si vyema kuyaweka moyoni pekee ni vyema uyatapike usije ukapata msongo wa mawazo. Wapo wajuzi wa mambo hapa JF watatusaidia katika mijadala.

  Inaonekana umewatisha CUF, siwaoni wakikujibu.Au pengine leo ni siku ya mapumziko watajitokeza kesho.
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nonda,

  Kama elimu yako ni ya kata basi shule zetu za kata zimefanikiwa na CCM ni wakupongezwa.

  Suala la muungano ni mojawapo ya mambo ambayo wengi wanaliongelea kwa kugusagusa. Hakuna anayetaka kuonekana anaupinga. Inabaki kusema ni 'mapungufu tu'.

  Ngoja nijipange nitoe kilicho moyoni kuhusu muungano.
   
 14. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  mkuu sijawahi kumwona mdau wa cuf humu jamvini
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  naona mjadala unaanza kunoga sasa wapaka upupu watakapotokea hata hatutaelewa

   
 17. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimependa thread yako ipo poa, CUF WANAFIKI SANA, Nashukuru vijana ambao ni taifa lakesho mmelitambua hilo, fitina zao na urafiki wao na Chama tawala ndio kitacho waponza!
   
 18. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hujui ulinenalo ni bora ukae kimya. Subiri moto wa baraza la wawakilishi ufike bungeni ndio utajua nini karata za CUF.
   
 19. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  professionally mie siyo mwanasheria kama bwana Msando, ila kwa kile kidogo ambacho na mimi nakifahamu kuhusu muunganao ni kwamba ule ilkuwa ni friendly contract kati ya Nyerere na Karume na karume was only forced due to historical background ya zanzibar mpka ikambidi akubali
  Nakumbuka kuna mdahalo wa kisiasa uliitishwa na REDET pale Nkurumah hole nafikiri Msando anakumbuka ,moja wapo wa watoa maada alikuwa ni Katibu mkuu wa ccm by then mzee Mangula aligawa paper zake akiwa anazungumzia historia ya zanzibar na pemba , lakini what was interested ni kwamba alisema KARUME aliuawa kwa idhini ya Nyerere na baada ya watu kusoma hiyo article walimuuliza maswali mengi naye akasema aliyeandika amekosea hakuwa na maana hiyo, kwa hiyo kuna uwezekano hata huo muunganao Mwanasheria wa Zanzibar from Nigeria by that time alimdanganya karume kuhusu muunganao kwa sababu kuna taarifa sizizo rasmi kuwa karume English ilikuwa ni issue sasa na hati ya Muungano imeandikwa kiingerza tena siyo normal English ila ni Kiingereza cha kwenye taalauma ya sheria, na ilkuwa ni muunganano wa kujaribu kwa miezi mitatu tu, ndiyo maana Maalimu Seif anasema alimsikia Karume kwa masikio yake akisema akiona muungano ni mzito anaweza akauvua kama koti,lakini baada ya kifo cha Karume waliobaki hakuna hata Mzanzibar mmoja aliyekuwa na uwezo wa kumuuliza Nyerere kuhusu Muungano na ndiyo maana alianzisha hata utaratibu wa kutafuta rais wa zanzibar kwa kupigiwa kura Dodoma wakati anaongoza visiwani.
   
 20. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kaka acha panic , CUF is a living dead political party now ,mtatiro is not a leader he is merely a primary teacher
   
Loading...