CUF: Tunainyima usingizi CHADEMA, heshima yetu haiwezi kumalizwa na CHADEMA wala CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Tunainyima usingizi CHADEMA, heshima yetu haiwezi kumalizwa na CHADEMA wala CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by itahwa, Mar 24, 2011.

 1. i

  itahwa Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naibu katibu mkuu wa cuf,julius mtatiro amezungumzia mikakati ya chama chake kurejesha heshima yake,
  Akizungumzia mikakati ya CUF katika kujijenga na kurejesha heshima yake ya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania bara, Mtatiro anasema “ Heshima ya CUF iko palepale. Haijakwisha wala haiwezi kumalizwa na CCM wala Chadema.

  Sisi bado ni chama cha upinzani chenye nguvu na ndio maana unaona sasa tuna maadui wengi zaidi”
  Anaongeza “zamani tulikuwa tuna mpinzani mmoja tu yaani CCM, sasa wameongezeka Chadema naye ni mpinzani wetu na ndio maana kila mara utasikia akitushambulia kwa kauli zisizo na maana, hii ni kutokana na hofu waliyo nayo juu ya CUF ambacho ndicho chama makini na chenye wafuasi wa kuaminika” anasema

  Anasema mashambulizi yanayofanywa na Chadema dhidi ya CUF ni ishara kuwa ndicho chama kinachowanyima usingizi na kutamba kuwa hiyo inatokana na uimara wake na mafanikio kilicho nacho katika siasa nchini.

  Mtatiro anasema CCM na Chadema vimekuwa vikieneza propaganda zenye nia ya kukichafua chama hicho kutokana na kukihofia na kujigamba kuwa hata hivyo juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwa kuwa wananchi wanajua mbivu na mbichi na kamwe hawawezi kudanganyika.

  Anasema watanzania ni wenye kuelewa na kuwa wamevishtukia vyama hivyo vinavyotafuta umaarufu kwa kukichafua CUF na kusema uchaguzi mkuu ujao ndio utakaomaliza ubishi wa kipi kati ya chama chao na vyama hivyo kinafanya siasa safi na zenye kukubalika na Watanzania.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mke wa nje hawezi kuwa na heshima hata siku moja ......!
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri CUF watakuwa na mkakati wa kuwa chama tawala, kumbe wana mkakati wa kuwa chama kikuu cha upinzani ! Hii ajabu kabisa!
   
 4. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama kweli chama chake kiko makini mbona kinawabunge 2 tu huku bara? CUF kwishney
   
 5. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ukiwa umejifungia chumbani kwako tuuu utaona dunia ni hapo ulipo tu.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Maneno ya mkosaji. Ni maneno ya kivita hayo, hata kama unashindwa vitani huwezi kusimama na kuukubali ukweli!
   
 7. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanajua chama tawala 2015 ni Cdm,wananga'ng'ania kuwa chama kikuu cha upinzani,kwa 7bu Ccm haitakuwepo tena,na hata ikiwepo nguvu yake itakuwa kama ya Tadea
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HAMAD RASHID NA CCM MJUE USALAMA WA NCHI UNAYUMBISHWA NA 'MUAFAKA WA MASLAHI BINAFSI' YA VYEO NA KUJIUNGA KULE NA NGURUWE KULA
  MABUA NA UFISADI ULIOKITHIRI NCHINI


  Jamani kuna uwezekano Wa-Tanzania tukawa na tofauti nyingi tu nchini zikiwemo zile za kitamaduni, kiimani, kijinsia na kadhalika lakini matatizo yanayotuhatarishia amani nchini, Wakristo kwa Waislmu na kote Bara na Visiwani ni zile zile!!

  Nasema matatizo ya kusisitizwa tu AMANI na kufichwa kule kwa HAKI kwa raia ni chanzo cha matatizo kibao yanayotukaba kila siku nchini kama vile: (1) UFISADI uliokithiri ndani ya serikali ya CCM yatuathiri sote, (2) Muafaka wa CUF kujiunga na CCM kula mabua kwa pamoja na kuwaacha wananchi solemba kwenye umasikini wa kutupwa ni letu sote, (3) Utaratibu wa Serikali ya Muungano usiona tija, na fursa sawa wa moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida, (4) ukosefu wa ajira, (5) elimu duni, (6) Maisha kupanda gharama kila kukicha ni letu sote hivyo kwa hali ya kawaida kabisa Mtanzania hahitaji KAMPENI ZA KUTIANA HOFU pale tunapojiunga kama taifa kujikomboa kwa kudai haki zaidi na Katiba Mpya nchini!!!

  ... hatuwe kujua vizuri; wenzetu wa CCM na CUF waulizwe vizuri juu ya hilo jambo wanaloliona peke yao tu hapa nchini kuhusu usalama kutetereshwa ambalo sisi wengine hatulion.

  Lakini kama kudai HAKI SAWA NA MASLAHI KWA UMMA wa Tanzania ndicho hasa kile kinachowakosesha amani wale MAFISADI walioko serikalini na kuitwa KUHATARISHA USALAMA WA NCHI na basi CHADEMA kazeni mwendo mdundo kwa sana tu.

  Wa-Tanzania tunaakili sana kote Bara na Visiwani na pia tunafahamu fika kwamba wale wanaoingia muafakaka na serikali ya CCM gizani kwa maslahi binafsi ya kupata vyeo, mijumba, na mashamba ndio hasa wanaoHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU.

  Ndugu zetu akina Hamad Rashid, CUF-Maslahi na CCM-Ufisadi, acheni mara moja kuchezea akili za Mtanzania wa leo kote Bara na Visiwani tunasema kwamba Hatudanganyiki wala Hatugawanyiki kwenye Kutafuta Maslahi yetu kama Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 9. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  Naona hawa jamaa hawana nia ya kushika dola. Halafu huyu Mtatiro haijui CUF, wenzake wako kimya hawaishambulii CCM kutokana na ndoa waliyofunga, yeye anataka kuwaharibia.
   
 10. s

  seniorita JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CUF is not a political party.......
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  angalau sasa anatambua chama chao kimepoteza hashima kama yeye alivyopoteza hashima miongoni mwa vijana wasomi wa Tanzania.
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi mtatiro alisoma UDSM kweli?
  Mbona ana tuaibisha na ana aibisha wakurya mjinga huyu,....kuwa mwanachama wa CUF sasa ni ugonjwa!
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Namwonea huruma Mtatiro! Mwenzake Seif amepewa umakamu wa rais akasahau kila kitu! Wamebaki Mtatiro na Hamad wanaweweseka. Na wataweweseka hadi waanguke maana hakuna namna na wao watapata cheo kwavile uchaguzi ujao wataendelea kushinda Pemba na chadema itakomba viti vyote bara! Namuhakikishia kuwa adui yao sio chadema ila wao ndio maadui wa chadema!
   
 14. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ONE: Hivi ni nani anamshambulia mwenzie CUF anu CDM?
  TWO: CDM wanakosa usingizi kwa lipi ambalo CUF wamefanya? Sasa hivi Prof Pumba na Hamad siRashid wanazunguka kote kuisemea CCM badala ya kujenga chama chao. Nani hapo kakosa usingizi?
  THREE: Uchaguzi mkuu ujao utamaliza ubishi ... Si wamwaambie JK aitishe huo uchaguzi hata sasa halafu waone joto lake! Mtaji pekee alionao JK sasa ni huo mchakato wa katiba mpya. Ambao hata hivyo ana wasiwasi kama utakinufaisha chama au utampa wala heshima kidogo akiwa ameondoka.
   
 15. k

  kiche JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  cuf wanasumbuliwa na ndoa ya mkeka,na bado!,wataropoka sana maana hawatakiwi kumshambulia 'bwana' yao ccm sasa maneno ya kuongea watayatoa wapi!?,ni ajabu mtu mzima kusema kuwa wao wanajiandaa kuwa chama kikuu cha upinzani!ni bora hata wasiwepo.

  Kauli hii inadhihirisha makubaliano yao na ccm mpaka cuf wakatema urais wa zanzibar licha ya kushinda,wanajua wazi kuwa hata wakishinda kwa mujibu wa ndoa yao ccm lazima watangazwe washindi,hapo kunafaida ya kuwa na cuf?

  Seif amewauza na wao wameshindwa wafanye lipi,nawashauri wageuke jumuia ya ccm kama walivyo uvccm kwani naona hawana tofauti tena afadhali kidogo uvccm wanaweza wakaropoka kidogo kama wanavyofanya sasa.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TATIZO MTATIRO KAFICHIWA MAFAILI KULE PEMBA JUU YA SURA HALISI YA CUF-MASLAHI

  Ndio alisoma pale sana tu lakini tatizo kubwa na huyu Ndugu Juliasi ambalo wengi mmegoma kulitambua ni kwa FAILI NYINGI NA NYETI juu ya CUF-Maslahi na 'kule kujiunga na nguruwe' ili wale pamoja, huyu bwana wameficha faili hizo kwani zote ziko kuleee kwa Maalim Seif Chake Chake - Pemba.

  Kwa zaidi mjue CUF-Maslahi kiliweza kuingia ndoa au muafaka na CCM-Ufisadi baada ya mazungumzo ya faragha na mshenga Yussuf Makamba akimtongozesha Maalim Seif kwa jina lake (CUF baadaye) na pingu za maisha zikafungwa kwenye ndoa ya mkeka tu kiasi cha Pro Lipumba kufanya kutaarifiwa tu bila kushirikishwa kwenye kila hatua.

  Kwa nini unashangaa Maalim Seif ndio yule kuleee chumbani kwa CCM anakula kuku kwa nafasi; akina Hamad Rashid makombo ya uenyekiti wa Kamati ya Bunge yakagoma, Mwanasiasa machachari nchini Duni Haji Duni ndio huyo anakufa anagugumia tu usaliti wote wa CUF kwa juhudi zake zile zote kuwekwa kando.

  Naye Prof Safari ndio hivo majuzi uzalendo wa kinafiki ukamshinda, na Abrahamu mwenyewe w Kigoma a.k.a CUF Career Presidential Candidate (CCPC) naye wasingemfanyia tu ka-mshahara ka mwezi mara baada ya fungu zito la kupiga bendeji mdomo basi leo moto mkubwa ungekua unawaka mle!!
   
 17. majata

  majata JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45

  Mtatiro mbumbumbu walausijishughulishe naye, anafikili siasa ni sawa na uongozi wa daruso.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,654
  Likes Received: 1,438
  Trophy Points: 280
  hivi anayemshambulia mwenzake ni nani?:smash:
   
 19. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu Julias mtatiro; unaposema 'MNAJIANDAA KURUDISHA HESHIMA" ipi hiyo? at least pia unakubali kuwa cuf hamheshimiki tena. Unasema mnajiandaa kuwa chama kikuu cha "upinzani" so hamna ndoto za kutawala. Kweli mmekwisha kaka
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi CHADEMA Inanyimwa Usingizi na CUF? Labda Zanzibar ambacho ni chama Tawala
   
Loading...