CUF: Tunainyima usingizi CHADEMA, heshima yetu haiwezi kumalizwa na CHADEMA wala CCM

Mtatiro kasema kweli...kuwa wanajiandaa kurudisha heshima ya CUF iliyopotea... ukisoma hapa maana yake hata kuanza kurudisha hawajaanza, bado wanajiandaa, na hii kujiandaa wataendelea kujiandaa mpaka 2015. Ni ukweli kabisa na namsifu Mtatiro kwa hili kuwa amekuwa muwazi kuwa CUF imepoteza heshima kwa wananchi kwa kukubali ndoa ya mkeka na CCM na ambayo hata mahari haina!!!!
 
ah ah ah!nafurahi sana,naona wameanza kugeuza maneno,sasa CUF ndio wanaoshambuliwa na CDM na sio CDM kuishambulia CUF
nawashukuru sana viongozi wa CDM kutowajibu,kaeni kimya hivyo hivyo,msiwajibu hata kidogo......wtz tunaona tu
CDM inaua ndege wawili kwa jiwe moja

Maskini Mtatiro kijana mwenzangu,dah!sijui ni lini utakubali kujisahihisha kwamba uliteleza,sijui utagombea tena ubungo 2015??
Tutakupiga nyama chini tu kama kawaida,nenda kagombee pemba na chama chako cha mabahasha!!!!!!
 
CDM ndiyo ingepaswa kusema inapinzana na CCM & CUF baada ya wao kuungana. Sasa huyu haijui hii ndoa ya nje ambayo ni halali kabisa, au labda anaupinga MUAFAKA aka Umoja wa Kitaifa kupitia vyama viwili tu toka upande mmoja wa nchi.
 
naibu katibu mkuu wa cuf,julius mtatiro amezungumzia mikakati ya chama chake kurejesha heshima yake,
Akizungumzia mikakati ya CUF katika kujijenga na kurejesha heshima yake ya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania bara, Mtatiro anasema “ Heshima ya CUF iko palepale. Haijakwisha wala haiwezi kumalizwa na CCM wala Chadema.

Sisi bado ni chama cha upinzani chenye nguvu na ndio maana unaona sasa tuna maadui wengi zaidi”
Anaongeza “zamani tulikuwa tuna mpinzani mmoja tu yaani CCM, sasa wameongezeka Chadema naye ni mpinzani wetu na ndio maana kila mara utasikia akitushambulia kwa kauli zisizo na maana, hii ni kutokana na hofu waliyo nayo juu ya CUF ambacho ndicho chama makini na chenye wafuasi wa kuaminika” anasema

Anasema mashambulizi yanayofanywa na Chadema dhidi ya CUF ni ishara kuwa ndicho chama kinachowanyima usingizi na kutamba kuwa hiyo inatokana na uimara wake na mafanikio kilicho nacho katika siasa nchini.

Mtatiro anasema CCM na Chadema vimekuwa vikieneza propaganda zenye nia ya kukichafua chama hicho kutokana na kukihofia na kujigamba kuwa hata hivyo juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwa kuwa wananchi wanajua mbivu na mbichi na kamwe hawawezi kudanganyika.

Anasema watanzania ni wenye kuelewa na kuwa wamevishtukia vyama hivyo vinavyotafuta umaarufu kwa kukichafua CUF na kusema uchaguzi mkuu ujao ndio utakaomaliza ubishi wa kipi kati ya chama chao na vyama hivyo kinafanya siasa safi na zenye kukubalika na Watanzania.


Hapo kwenye RED kuna upungufu wa kufikiri. Hauwezi kurejesha Heshima ya kitu kama bado kipo. Utaweza kurejesha heshima ya kitu kama kimepotea
 
Ng'wanangwa,
Thanks. Angalau ametambua kuwa wamepoteza heshima. Nadhani anahitaji kwenda mbele zaidi, angejua nani amewang'oa kuwa chama kikuu cha upinzani. Chadema hakihusiki kabisa bali wenye nchi yao, yani wapiga kura. Kuna tofauti kubwa sana. Pamoja na uchakachuaji wote, wtazame idadi ya kura hivyo hawana sababu ya kutusema Chadema. Isitoshe tuwaache wao wahangaike na kurudisha heshima yao.Chadema inasonga mbele kutetea haki za watanzania.Maslahi ya nchi mbele kuliko ya Chadema.as katika utekelezsaji wa majukumu yetu kwa wananchi wataona tunastahili kupata heshima watatupa kwa ridhaa yao, lakini, kuzunguka nchi kutafuta "heshima" sioni kama ina tija yeyote kwa mtanzania ambaye ana kero na matatizo kibao



angalau sasa anatambua chama chao kimepoteza hashima kama yeye alivyopoteza hashima miongoni mwa vijana wasomi wa Tanzania.
 
CUF na CCM si waneungana jamani! sasa CCM watakuwaje maadui wa CUF!!!!
Alafu Mtatiro bwana nae kaanza kumwiga Lipumba kuongea kwa kupanuapanua limdomo loote!!!...henhee!! Kweli mabosi wanaigwa hata kwa ujinga wao!
 
ah ah ah!nafurahi sana,naona wameanza kugeuza maneno,sasa CUF ndio wanaoshambuliwa na CDM na sio CDM kuishambulia CUF
nawashukuru sana viongozi wa CDM kutowajibu,kaeni kimya hivyo hivyo,msiwajibu hata kidogo......wtz tunaona tu
CDM inaua ndege wawili kwa jiwe moja

Maskini Mtatiro kijana mwenzangu,dah!sijui ni lini utakubali kujisahihisha kwamba uliteleza,sijui utagombea tena ubungo 2015??
Tutakupiga nyama chini tu kama kawaida,nenda kagombee pemba na chama chako cha mabahasha!!!!!!
mkubwa wangu hapo umeniacha stendi
 
Hatuhitaji kutukana kwawanao tutukana ! lakini tunahitaji kushangaa na kucheka pale wachekeshaji wanapo kuwa kazini maana bila kufanya hivyo tutakuwa hatuja heshimu kazi ya wenzetu.CuF sasa wamegeuka kuwa wa chekeshaji na kukosa kuwa chama cha siasa. Hili linathitishwa na umakini wao na uwezo wa naibu katibu mkuu wa chama hiki anaposimama mbele ya umati wawatu kueleza waziwazi kuwa chama chao kina mikakati ya kurudisha heshima yake na hatimaye kuwa chama kikuu cha upinzani.

Hakika haiingii akilini kabisa kuwa hiki nichama cha siasa kwa maana ukimwuliza mwenyekiti au katibu mkuu wa CCK mikakati yake inalenga nini atakuambia kukamata dora hili ndio lengo la chama cha siasa.Wakati huo CUF mikakati yao inalenga kurudisha heshima ambayo kwa mtazamo wangu hawastahili kurudishiwa kama waliwahi kuwa nayo kwasababu wamekosa mwelekeo wa chama cha siasa.

Naibu katibu Mkuu CUF anashindwa kujenga hoja kama chama cha siasa wanasimamia nini badala yake anasema CDM wanakosa usingizi, hivi watanzania wanamda wa kupoteza kukiunga mkono chama ambacho hakisimamii mambo ya msingi yanayo wahusu ila kuwakosesha usingizi CDM.

Naibu katibu mkuu CUF anasubiri uchaguzi 2015 ili aonekane nachama chake wako juu bila kufanya jitihada zozote za kuwatetea wananchi wanaotaabika na maisha magumu kilasiku na wala haonyishi misimamo yoyote katika kupambana na ufisadi unao watesa wananchi. Huu utakuwa muujiza kwa mtanzania kukubaliana na hawa wa chekeshaji.

CUF kwa mtazamo huu mnakosa sifa za kuungwa mkono kama chama chasiasa......
 
Nilifikiri CUF watakuwa na mkakati wa kuwa chama tawala, kumbe wana mkakati wa kuwa chama kikuu cha upinzani ! Hii ajabu kabisa!

Mimi sijaona source ya hii post lakini nimeshangazwa sana na kauli ya Mtatiro; very mediocre, badala ya kufikiri kuchukua dola wanajijenga kuwa chama cha upinzani kikuu. Kweli siamini kama Mtatiro ndo kasema hiyo pumba!
 
Back
Top Bottom