Ahsante sana Profesa Lipumba kwa kuzidi kuwaanika mafisadi,hii ya Chadema kuwa ni CCM B inajulikana zamani sana ,kwa ufupi CHADEMA ni wanafiki na waongo wakutupwa ni wao wanaowadanganya WaTz kwa ujanja mkubwa sana, CUF imeshindwa kuvumilia maana Chadema imeonysha haivumiliki wala haichukuliki.
Chadema imenaswa pabaya sana ,napenda kuwaonya WaTz kuwa wasiwe na Jazba wala wasiwe wenye kuzidi upande mmoja ,kama hapa JF kuna msemo au heading kuwa the Palace of Great Thinkers & ukiongezea ..We Dare to Talk Openly.
So Mheshimiwa Lipumba ametibua hoja kuwaambia WaTz kuwa hata CHADEMA nao ni mafisadi , na akwataja akina Bob Makani(aliewahi kuwepo CUF) na Edwin Mtei kuwa waliibia Benki na kama haitoshi wakaichoma moto ,Sasa waTz hii au hili sio jambo dogo na utawezaje kuwakabili CCM ikiwa ndani mwako wapo watu ambao nao wameiba na kuichoma moto benki ,hivi hapa kuna baya lipi ? Je hilo ni kosa ? Msiukimbie ukweli maana tunahitaji viongozi ambao ni wasafi ,iwe Chadema au CUF ,ni vizuri kama watu wa Chadema mpo hapa basi mlijadili hili ,ili kujisafisha ,kusema Profesa hana isipokuwa pumba huko mtakuwa mnakimbia vivuli vyenu wenyewe ,ila kwa mwenye akili ya kutaka kuijenga Tz yenye viongozi safi ,basi hana wajibu kumuunga mkono Mheshimiwa Lipumba na kuzifanyia kazi hoja zake ,nahisi Chadema wanahitaji kuzijibu hoja hizi ,lakini Lipumba amesema kwa ushahidi sasa kama huko Chadema mkifanya siri mjue ,siku hizi siri zinauzika au zinauzwa , ninachowaomba muwe makini na vyama vya upinzani sio mnafuata tu kwa kuwa Chadema inakuja na mabomu mengi huko bungeni ,inawezekana kabisa mabomu hayo ni kujikinga dhidi ya mashambulizi.
Inaonyesha kabisa kuwa kimya kirefu cha CUF katika mambo ya mafisadi ilikuwa ni kuwasoma wale wote wanaolipua mabomu ,na labda tuseme wananchi wwalikuwa wameshatekwa na watu hawa na kuwaona kuwa ..hawa ndio viongozi wanaoweza kutuletea maendeleo au sio na ikafikia kuwa kila mtu anaona waChadema ni viongozi makini kabisa ,sasa katika uono huo CUF imeweza kuwasoma na kuwakuta kuwa kumbe hata hawa wanaolipua mabomu pale bungeni ni maadui wa Taifa hili kwa msemo mwengine ni mafisadi.
......Viongozi hao wameeleza kwamba hata viongozi wa CHADEMA waliofuata wakina Freeman Mbowe, Dr Slaa na Zitto Kabwe wote wana tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazowakabili...!.
Jamani hizo ni tuhuma nzito sana ,tena sana sio mchezo ,hapo wametajwa viongozi wa juu kabisa wa CHADEMA ,kwa maana ingine tusiwe tunawapigia kelele wale wa EPA ,RIchmond ,Twin BOT buildings na mengine ,tukawaacha hawa kwa kuwa tu ni wa CHADEMA ,hilo litakuwa halikubaliki ,tuwe wenye kuwaongoza wananchi pale panapoonekana pana manufaa as a Jamii Forums na sio kuwakandia CCM peke yao ,lazima tuvikubali vile vyama ambavyo vinaoonyesha viongozi wake wapo katika mstari ulio sawa ,hawana madoa madoa ,tukumbuke harakati za uchaguzi wa Marekani ,kitu kidogo tu alichonacho mgombea kinaweza kabisa kuhatarisha uchaguliwaji wake ,sasa tujaribu kuiga yale mambo ambayo wenzetu huwa wanayafuata katika kumchagua kiongozi alie bora.
Tuacheni jazba na tujaribu kuutafuta ukweli ,na ukweli wa viongozi ambao tunategemea ipo siku watatuongoza , Sasa habari ndio hiyo ipo magazetini ,tuwajadili akina viongozi hawa wa CHADEMA ambao kama wengine mnavyoona kuwa wana nafasi ya kuwa viongozi au kushika madaraka ya nchi hii ,na hivyo kuwaelekeza wananchi pale ambapo patagunduliwa kuwa ni kweli ,aidha Chadema wanayo nafasi ya kuwasafisha viongozi hao ikiwa wanasafishika ,kwa maana ingine kuonyesha kuwa tuhuma walizopachikwa ni uongo ,na sio kusema uongo tu ,tunahitaji kuona CHADEMA inadai uthibitisho kutoka kwa CUF juu ya tuhuma hizo ,kukaa na kusema Lipumba au CUF ni wababaishaji ,wameishiwa ,hawana jipya ,sijui wamechemsha na menginetele ,kwa kweli hakutowasaidia CHADEMA ,aidha natarajia kuona viongozi wa CHADEMA wakikusanya vyombo vya habari na kupinga ,ila kama mambo hayo ni kweli basi watakuwa wamefwulia.