Katika hali ya kushangaza V4C iliyozinduliwa na CUF imejulikana lengo lake kubwa ni kufanya kampeni za Urais kwa ajili ya mgombea wa kudumu wa chama hicho Prof Ibrahim Lipumba.
Katika mkutano uliofanyika jangwani wapambe karibu wote walikuwa wanamuombea kura Lipumba za mwaka 2015.Hayo hayo yamejirudia kwenye mkutano wao waliofanya kule Arusha.
Tunapenda kuiuliza tume ya uchaguzi ni lini imetangaza nafasi ya Urais iko wazi? Je hiki ni kipindi rasmi cha uchaguzi?
Je ingekuwa CDM ndiyo inazunguka mikoani na kumuombea kura Dr Slaa au Freeman Mbowe serikali ingekaa kimya? Si ingetangazwa wanachofanya CDM ni uhaini?
Tunamuuliza Msajili wa vyama vya siasa hili ni sawa? Au kwa vile linafanywa na mshirika wa CCM sio kosa?
Ikumbukwe msajili huyu huyu alisema hataki kuona M4C ya CDM kwa madai isubiri kipindi cha uchaguzi ufike.Lakini kwake ni sawa Lipumba akiombewa kura sasa za urais wa 2015.
Source:Tanzania daima Jumapili Makala.