CUF iko juu ya sheria Tanzania?

Tatizo la taifa letu ni kufanya mambo kiubaguzi, haiwezekani sheria moja ikatafsiriwa tofautitofauti. Pili kwa cuf inaonekana tayari mgombea wao ni lipumba na maalim seif, kama kawa demokrasia ndani ya cuf ni msamiati!

Mkuu wangu nilipohudhuria mkutano wao pale Jangwani baada ya kumtangaza Lipumba kama mgombea wao uchaguzi mkuu ujao na walipoanza tu kumuombea kura niliondoka kwa Aibu kubwa.Niliisikitikia demokrasia Tanzania.
 
Hivi huyu JOHN MREMA huko CDM makao makuu kazi yake ni nini hasa? Kila siku anashinda JF kumwaga fitna tu! ZZK wa CDM si katangaza hadharani kugombea urais mbona hamsemi?

Mods tafadhali huyu ashughulikiwe.
 
CUF wamejaribu kuiga M4C, lakini walichochemka ni kumwombea kura Lipumba. ninapata mashaka na uprofesa wa Lipumba, ama anajua wanaomwombea kura ni chakula cha wasomi (wajinga).

Kuna watu wenye nia mbaya wameanza kueneza mtindo huo wa kumwombea kura lipumba mpaka misikitini inasikitisha sana. hawana nia njema na cuf.

Mkuu wangu Nyerere alisema mtu yeyote anayetumia udini kujihalalisha amefilisika na kamwe hatafanikiwa.Kama ni kweli Lipumba anafanyiwa hivyo hatafika popote.
 
Mkuu sio kwamba inamwogopa isipokuwa Kikwete anamtumia Ponda, na Said mwema ni

sehemu ya hayo matumizi.

Mkuu wangu lakini wanachofanya CUF ni kubaka demmokrasia waziwazi.
 
ccm b hawawezi fanywa kitu, wapo kupunguza moto usiozimika wa cdm, afterall huyo sultani wa cuf hata afanyaje hatopata uraisi
 
ccm b hawawezi fanywa kitu, wapo kupunguza moto usiozimika wa cdm, afterall huyo sultani wa cuf hata afanyaje hatopata uraisi

Mkuu wangu uchaguzi mkuu uliopita Sultani Lipumba alipata kura laki 6 huku Dr Slaa wa CDM akipata kura zaidi ya milioni 2 tena baada ya kuchakachuliwa.
 
Hivi huyu JOHN MREMA huko CDM makao makuu kazi yake ni nini hasa? Kila siku anashinda JF kumwaga fitna tu! ZZK wa CDM si katangaza hadharani kugombea urais mbona hamsemi?

Jibu hoja wewe hayo ya John Mrema fungulia thread utapata vilaza wenzako watachangia
 
mbona chadema mmekuwa na mchecheto na CUF? hizi ni mvua za rasharasha masika 2015.

Mkuu

CUFU ya 1995, sio hii ya leo.

Jussa na Lipumba ndani ya Cuf moja wanamalengo tofauti, Mmoja anataka zanzibar huru na mwingine anautaka urai wa

Jamhuri ya muungano wa tanzania kuna malengo ya kichama kweli hapo?
 
Jibu hoja wewe hayo ya John Mrema fungulia thread utapata vilaza wenzako watachangia

Mkuu wangu huyo kilaza ameshikwa pabaya na Sultani wake Lipumba.Kama John Mrema anampelekesha sana amtafute aliko wmalizane.
 
Mkuu

CUFU ya 1995, sio hii ya leo.

Jussa na Lipumba ndani ya Cuf moja wanamalengo tofauti, Mmoja anataka zanzibar huru na mwingine anautaka urai wa

Jamhuri ya muungano wa tanzania kuna malengo ya kichama kweli hapo?

Mkuu wangu Adolay
Mpe somo huyo maana naona hana kumbukumbu.
 
Hivi huyu JOHN MREMA huko CDM makao makuu kazi yake ni nini hasa? Kila siku anashinda JF kumwaga fitna tu! ZZK wa CDM si katangaza hadharani kugombea urais mbona hamsemi?
kutangaza kugombea sio kosa hata wewe unaruhusiwa kutangaza nia, tatizo ni kutumia majukwaa kusema chagua fulani na ndo kosa la cuf!
 
Mkuu wangu lakini wanachofanya CUF ni kubaka demmokrasia waziwazi.

Mkuu Malemo

Pamoja na kuibaka Demokrasia lakini wamedhofika sana, tena Ndoa yao imewaharibia kabisa maana wamesahau hata

majukumu yao ya kuikosoa serikali iliyomadarakani ya ccm kwa faida na maendeleo ya watanzania.
 
Mkuu Adolay
Mkutano wao wa Arusha umewavua nguo.Kitendo cha kutoa watu 500 Dar kwenda kuwahutubia Arusha ni aibu kubwa katika historia ya siasa duniani.
 
Mkuu kampeni za urais haijatangazwa bado. Ingelikuwa ni chadema wanafanya hivyo ungemsikia msajili wa vyama vya siasa kada wa ccm John Tendwa akiropoka kutishia kukifuta usajili.
Wenye mamlaka ya kutangaza kuanza kwa kampeni ni tume ya uchaguzi, si mwingi awaye yote.
CDM ni mtoto wa kambo, CUF ni bi mdogo na Tendwa ni Mshenga
 
CUF wako kwenye ndoa na mahaba Yao CCM ni makubwa wacha wawe juu ya sheria
 
Back
Top Bottom