Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,810
- 831,001
Safari unayofika salama salimia kwenye mabus yetu jua wazi kuna ushirikiano mkubwa wa dereva na kondakta.
Lakini pia hata kwenye vyombo vya majini na angani ambako huko kondakta ni co-pilot.
Ndani ya familia ni Vilevile lazima kuwe na maelewano kati ya baba na mama
Kwenye siasa kuna watu wawili muhimu sana mwenyekiti na katibu! Hawa lugha zikianza kupishana tuu lazima chama kiyumbe.
Mwenyekiti wa CUF alijiuzuru wazifa wake katika kipindi ambacho chama kilikuwa kinamhitaji mno..yani ni sawa na dereva kumuachia kondakta gari kwenye mteremko!
Kujiuzulu kwake kwa barua rasmi ni haki yake ya kikatiba.
Maalim Seif kwa uvumilivu mkubwa na umahiri pia kwa kushirikiana na viongozi wengine ndani na nje ya chama wakavuka salama japo wakiwa majeruhi wa majeraha yaliyosababishwa na mwenyekiti wa chama aliyejiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe.
CUF mizizi yake iko visiwani na kule kimeendelea kuwa chama imara chini ya Maalim Seif ambaye amevumilia vishindo vingi vizito sana... Cuf Zanzibar ndio inaibeba Cuf bara.
Kitendo cha Prof Lipumba Kujiuzulu kipindi kile cha uchaguzi kilichukuliwa kama ni usaliti kwa CUF visiwani na tangu hapo viongozi wengi wa bara hawakuaminika tena na wenzao wa visiwani.
Mkakati wa Lipumba kutaka kurudi kwenye nafasi aliyejiuzulu kwa hiari ni kama pigo la mwisho la kutaka kuisambaratisha CUF kabisa.
Maalim Seif ameshaliona hilo na kwa sasa inabidi achukue maamuzi ya kitemi ili kukinusuru chama, wabara inabidi wamsikilize Maalim kuliko Lipumba na genge lake.
Wakishupaza shingo chama kitasambaratika huku bara.