CUF bara waufyate tuu

CUF bara waufyate tuu

Naona fikra kiduchu ndizo zinazokuhangaisha. Kama ungekuwa na upeo thabiti ungaliona jinsi katiba inavyonyong'onywezwa na kufinyangwa. Mwanzoni mlinyanyasa sana Mzee James Mapalala mpaka akakata tamaa na akaamua kuondoka, lakini kwa huu mziki ulivyo mnene, HATOKI MTU!

Wanajipa moyo tu., kwisha habari yake, ndembe ndembe chaliii
 
Naona fikra kiduchu ndizo zinazokuhangaisha. Kama ungekuwa na upeo thabiti ungaliona jinsi katiba inavyonyong'onywezwa na kufinyangwa. Mwanzoni mlinyanyasa sana Mzee James Mapalala mpaka akakata tamaa na akaamua kuondoka, lakini kwa huu mziki ulivyo mnene, HATOKI MTU!
Mbona mnapata shida kubwa wakati adui mkubwa wa CUF Anajulikana ni nani? I mean adui mkubwa wa siasa za upinzani
Wanajipa moyo tu., kwisha habari yake, ndembe ndembe chaliii
 
Mbona mnapata shida kubwa wakati adui mkubwa wa CUF Anajulikana ni nani? I mean adui mkubwa wa siasa za upinzani
Mpe jina huyo adui, manake siasa za bongo kila mtu aweza kuwa adui yako na angalizo ni kwamba katika siasa hakuna adui wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu
 
Safari unayofika salama salimia kwenye mabus yetu jua wazi kuna ushirikiano mkubwa wa dereva na kondakta
Lakini pia hata kwenye vyombo vya majini na angani ambako huko kondakta ni co-pilot
Ndani ya familia ni Vilevile lazima kuwe na maelewano kati ya baba na mama
Kwenye siasa kuna watu wawili muhimu sana mwenyekiti na katibu! Hawa lugha zikianza kupishana tuu lazima chama kiyumbe
Mwenyekiti wa CUF alijiuzuru wazifa wake katika kipindi ambacho chama kilikuwa kinamhitaji mno..yani ni sawa na dereva kumuachia kondakta gari kwenye mteremko ! Kujiuzulu kwake kwa barua rasmi ni haki yake ya kikatiba
Maalim Seif kwa uvumilivu mkubwa na umahiri pia kwa kushirikiana na viongozi wengine ndani na nje ya chama wakavuka salama japo wakiwa majeruhi wa majeraha yaliyosababishwa na mwenyekiti wa chama aliyejiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe
CUF mizizi yake iko visiwani na kule kimeendelea kuwa chama imara chini ya Maalim Seif ambaye amevumilia vishindo vingi vizito sana... Cuf Zanzibar ndio inaibeba Cuf bara
Kitendo cha Prof Lipumba Kujiuzulu kipindi kile cha uchaguzi kilichukuliwa kama ni usaliti kwa CUF visiwani na tangu hapo viongozi wengi wa bara hawakuaminika tena na wenzao wa visiwani
Mkakati wa Lipumba kutaka kurudi kwenye nafasi aliyejiuzulu kwa hiari ni kama pigo la mwisho la kutaka kuisambaratisha CUF kabisa
Maalim Seif ameshaliona hilo na kwa sasa inabidi achukue maamuzi ya kitemi ili kukinusuru chama, wabara inabidi wamsikilize Maalim kuliko Lipumba na genge lake ! Wakishupaza shingo chama kitasambaratika huku bara
chadema kutoka kupigania demokrasia hadi kukandamiza demokrasia...kisa tu hawa wabara wako tofauti na Sultani Seif?
 
chadema kutoka kupigania demokrasia hadi kukandamiza demokrasia...kisa tu hawa wabara wako tofauti na Sultani Seif?
Hivi kuna exit ngapi za kuingilia dar ? Mahitaji ya nyakati yamenisukuma niandike hiki nilichoandika
 
Kaamua kumtumikia shetani
Aisee tatizo la hivi vyama mbadala havitaki ufikiri tofauti na wanavyofikiri wao lazima wakuvue uanachama...ndo maana hii demokrasia wanayopigia kelele tunajua ni kutafuta kiki tu baada ya kuishiwa hoja ya maana
 
Ccm inajua wazi nguvu ya CUF visiwani na nguvu ya CHADEMA bara ! Kushamiri kwa hivi vyama kila upande kwa vyovyote vile sio habari njema kwa ccm
Tatizo kubwa ni kufikiri unavyotaka halafu kutuletea majibu bila kuyapima kama haya yanafaa kiliwa na member sijui umepatwa na ugonjwa gani....huu ugonjwa naona umewapata watu wengi sana mliokuwa mnasapoti mabadiliko ya kuzungusha mikono
 
CCM wanajua sana kuchezea siasa, sasa ili jambo sijui kama limetokea lenyewe hama walipanga....

Maalim yuko kwenye wakati mgumu mno hivi sasa, kupita vipindi vyote....
 
Lipumba pamoja kuwa mwanauchumi mwenzangu but simkubali on political arena . Nashauri apumzike apate muda WA kusoma thesis zake.

Dead and gone.
 
Tatizo kubwa ni kufikiri unavyotaka halafu kutuletea majibu bila kuyapima kama haya yanafaa kiliwa na member sijui umepatwa na ugonjwa gani....huu ugonjwa naona umewapata watu wengi sana mliokuwa mnasapoti mabadiliko ya kuzungusha mikono
Aisee...! Hivi huzioneagi huruma mb zako ?
 
Aisee tatizo la hivi vyama mbadala havitaki ufikiri tofauti na wanavyofikiri wao lazima wakuvue uanachama...ndo maana hii demokrasia wanayopigia kelele tunajua ni kutafuta kiki tu baada ya kuishiwa hoja ya maana
Ukiwa na mawazo tofauti na wenye chama jambo la haraka ni kukuvua uanachama. Hiyo turufu inawafanya wenye mawazo mbadala wawe na unafiki wa unyenyekevu.
 
Upeo wako ni mdogo., siku zote ni bora chama kuliko yooote hayo uliyoeleza, chama kibaki hai na salama kisiasa ndio kitu nyeti tunachoangalia.,

Tanzania ni kubwa, wasomi wapo wengi, there are so many Prof.Lipumba, hao kina Sekaya ndo kabisa, ni bora kujenga chama kikawa imara zaidi. Lipumba aanzishe chama chake na taasisi yake huko Bara, ukitaka kujuwa kilichomkuta HR Lipumba ni zaidi. HR alitarajiwa kuwa mrithi wa maalim seif leo Zanzibar ukimtaja HR hakuna anayemjuwa ni kwa sababu chama kilifanya maamuzi magumu na kuijenga CUF ya sasa.

CUF tokea imeanzishwa ni chama pekee cha upinzani Tz kilicho madhubuti na kinazidi kupiga hatua kila uchao. Katika taasisi hakuna mtu mkubwa zaidi kuliko taasisi, Lipumba alihisi CUF ni yeye na yeye ndo CUF. mwache ajifunze aendako. PUMBA TUPU UMEANDIKA
 
Nifahamishwe tu ikiwa katibu wa CUF anatoka Zanzibar ni lazima M/kiti atoke Bara?
 
ADAM KAMBAYA.jpg


NA ABDUL KAMBAYA

SIJAMBO GENI, HATA FIRAUN ALIPOSHINDWA KUJIBU HOJA ZA MUSSA ALITUMIA JESHI

Nimekua napigiwa simu nyingi toka kwa Wanachama wenzangu na Waandishi wa habari kuhusu Taarifa zilizozagaa kwenye Mitandao. Majibu yangu ya awali Kuhusu Taarifa hizo ni

1 Moja Baraza Kuu lina Mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na kwa kwa kufuata Katiba jinsi inavyoeleza kwenye hizo taratibu za kuchukua hatua za Kinidhamu.

2 Mimi na wenzangu tunaotajwa kwenye kadhia hiyo ikiwa ni Pamoja na Wabunge wa Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma) na Magdalena Sakaya Mbunge wa Jimbo la Kaliua na Diwani wa Kata ya Misima Wilayani Handeni,pamoja na wale ambao sikuwataja hatukuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa na Baraza Kuu lilofanyika jana Mjini Unguja katika Visiwa vya Zanzibar.

3 Baada ya kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu uliofanyika pale Ubungo Plaza Tarehe 21 /08 /2016 kutokana na Wajumbe 324 kutoridhishwa na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwa Wajumbe wasio halali kwenye Mkutano Mkuu, mimi ni miongoni mwa Wajumbe tuliojiorodhesha na kuandika barua ya Malalamiko na kupeleka Ofisi ya Msajili wa Vyama.

Kutokana na Mambo hayo Matatu, nawaomba Wanacuf msifadhahike na wala msihuzunike waliotufukuza kabla hata ya kutoa majibu ya hoja zetu tulizowasilisha kwa Msajili, bila shaka hawana Majibu ya sahihi ya hoja zetu. Na jambo hili sio geni kwa hapa Duaniani, Firaun aliposhindwa kuthibitisha kua yeye ndie Mungu, alitumia Jeshi lake (Baraza Kuu) kutaka kumuangamiza Mussa na Wafuasi wake waliokua wanaamini katika Haki na Mungu wa kweli.

Kilichoendelea Zanzibar ni Mfano wa Firaun na Jeshi lake dhidi ya Mussa na Wafuasi wake.

Kauli yangu ya Mwisho ni kwamba hatoki mtu kwenye Cuf hii kwakua sio ya Mtu bali ni ya watu, sijambo jema kujifananisha na Firaun, jibu hoja usitumie Jeshi kujibu hoja. Hakuna kukataa Tamaa wala kukimbia Cuf. Harakati za kutafuta Uhuru ndani ya Cuf kwa Watanganyika ndio kwanza umezifungulia Geti, sasa ni hoja za Makabwela dhidi ya Vibaraka wa Mabepari wa Tanganyika.
 
Hata ZZK alisema hatoki CHADEMA.
Mara zote shetani akikutumia ni wewe unayeishia to a very Miserable end
 
Back
Top Bottom