CUF bara waufyate tuu

CUF bara waufyate tuu

Na kwa kufanya hivyo kwa maoni yangu atafanikiwa kutimiza lengo la kuidhoofisha CUF na pia UKAWA. CHADEMA na CUF wasiotumika na maccm au ambao si mamluki watafanya jambo la maana sana kuamua kuungana na vyama vyote ndani ya UKAWA na hivyo kuunda chama kimoja chenye nguvu bila kuchelewa. Wakiweza kufanya hivyo lengo la Lipumba na waliomtumia ndani ya CCM litakuwa limeshindwa vibaya sana.

Kaamua kumtumikia shetani
 
Siasa za Tanzania zinachosha akili,usipokuwa makini utayumbishwa sana. Sasa viongozi wasio makini wanavyoyumbishwa,wanakubali kutumika na kuwasaliti wenzao kisa pesa kidogo. Sakaya ndio kaharibu sana.
 
Kwa hii fukuzafukuza Maalim amekurupuka, angetumia hekima na busara katika kuumaliza mgogoro. Na hapa badala ya kuutatua mgogoro ndio ameuchochea. Ametengeneza mgogoro na CUF Bara. Sipati picha jinsi Wabunge wa Bara na Visiwani watakavyoweza kuishi ndani ya Bunge. Sipati picha jinsi dhana ya UKAWA itakavyoweza kutekelezwa ndani ya Bunge wakati mshirika mwenza amejigawanya. Hapa kutakuwa na hali ya kutokuaminiana kati ya Wabunge wa Chama kimoja. Je CDM atashirikiana na CUF Zanzibar au CUF Bara? Ni ngumu kumeza! Kwa ujumla Maalim ametibua badala ya kujenga Umoja ndani ya CUF.
Kwa wana lumumba lazima mumchukie maalim
 
Na kwa kufanya hivyo kwa maoni yangu atafanikiwa kutimiza lengo la kuidhoofisha CUF na pia UKAWA. CHADEMA na CUF wasiotumika na maccm au ambao si mamluki watafanya jambo la maana sana kuamua kuungana na vyama vyote ndani ya UKAWA na hivyo kuunda chama kimoja chenye nguvu bila kuchelewa. Wakiweza kufanya hivyo lengo la Lipumba na waliomtumia ndani ya CCM litakuwa limeshindwa vibaya sana.
Na huo ndio muarobaini wa kushindana na siasa za maji taka kwani ccm watashindwa kujipenyeza kwenye huo muungano wa chama kimoja
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kweli hakika binadamu ni wanafiki hasa sisi waTanzania......yaani Lipumba huyu huyu....wadau walokuwa humu ndani wanajaribu kumshawishi Magufuli ampe kitengo cha ushauri wa masuala ya uchumi.....maana ni mwana Uchumi nguli leo hii ndio huyu anaambulia matusi..!!!??

Najua zile sifa na kila aina ya jina zuri ni kwa sababu alikuwa pamoja na UKAWA...pamoja na CHADEMA katika malengo yao ya kisiasa.....lakini baada kutokea kutokuelewa na viongozi wa UKAWA akajiengua kwenye muunganiko huo.....na hapo ndipo matusi yalipoanzia kwa huyu mtu tuliyewahi kuaminishwa ni nguli wa uchumi.......

Lakini hii haishangazi kwa vijana wa CHADEMA kwani walisha acha kutumia akili muda mrefu sana....na ndio maana hata uongozi unaweza ukakiiita kinyesi kuwa ni keki na wao japokuwa wanaona kuwa kile ni kinyesi lakini watashangilia kuwa ni keki.....hawa hawashangazi kwani ni watu ambao wameshapoteza udhibiti wa bongo zao na kuwakabidhi viongozi ambao wamejivika taswira za ukombozi katika macho ya vijana waliokata tamaa......

Si kwamba naegemea upande wowote ule la hasha.....bali ifikie kipindi watu waheshimu watu wengine.....mimi nadhani yale maamuzi ya Lipumba kutimka kwenye uongozi wake yalikuwa ni maamuzi yake nayo pia yalipaswa kuheshimiwa kwani ni haki yake.........

Watu wanaokimbilia kwenye hoja za kuwa alinunuliwa na CCM ndio hao hao wenye fikra fupi na finyu......kwani wanashindwa kujiuliza je tukio la Lowasa kuhama CCM na kutua CHADEMA tena katika wakati mzito wa uchaguzi ambao kila mtu ameliona vumbi lake.....je na wao walimnunua Lowasa....!!!??

Sasa kwanini maamuzi ya Lowasa kuhamia CDM ambapo alikuwa nembo yao ya ufisadi na kila sifa mbaya ya wizi yaheshimiwe na kupongezwa kuwa ya kishujaa huku maamuzi ya Lipumba kukataa kula matapishi yake na kuishi kwenye maneno yake....yaonekane kuwa ni kinafiki na yamenunuliwa......ni mpumbavu pekee ndio anayeweza kuukubali ujinga huu......!!!

Mimi nadhani kama ambavyo watu wanasifiwa kwa kutumia haki zao vyema za kikatiba kutoka vyama vingine na kuja CDM....basi vile vile haki hiyo hiyo iheshimiwe hata kwa wengine wanaotoka CDM na kuhamia vyama vingne.....na kumuita mtu msaliti na kuanza kumtusi.......

Kama Lipumba ana haki ya kuwania uongozi ndani ya chama chake na sifa anazo basi apambanishwe na hao wagombea wenzake.....na kama hakidhi vigezo basi abwagwe kwenye kinyanganyiro.....na sio kuleta majungu na matusi......

HASIRA na chuki dhidi ya CCM visitufanye kuwa vipofu hata tusione upande wa pili wa shilingi jinsi viongozi wetu wa upinzani wanavyotugeuza kama makatuni kwa maslahi yao katika taswira ukombozi na sisi kwa upumbavu wetu na mihemko tunayapokea bila ya kutumia japo robo ya akili zetu......huu ni uchizi wa kisiasa......
 
Kinachokiua Cuf bara ni ubaguzi wa Maalim Seif na Chadema wanachochea kwa kutaka wao ndio waonekane chama pekee cha upinzani chenye nguvu wameshakiua Nccr na sasa wanakishughulikia Cuf
Kwa hili napingana nawe kwa asilimia mia moja
 
Kwa wana lumumba lazima mumchukie maalim
Hii project nzima inadhaminiwa na kitengo kwa ujanja sana huku kikijitahidi kutaka kukipaka CHADEMA matope lakini mwisho wa siku ukweli utatamalaki kwakuwa siku zote kitu cha kupanga huacha alama za makosa zisizofutika
1472439572852.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Vijana wa Chadema wao wanaona wengine tu ndio wananunuliwa! Hapa naona Lipumba anapewa majina yote. Kwa nguvu ile iliyotengenezwa mwaka jana kama Dr Slaa alishindwa kuizuia angeweza Lipumba huku Maalim Seif akiwa amehakikishiwa kushinda Zanzibar na Ulipo tupo?
 
Kuna msemo unaosema ni heri mlevi wa visiwani kuliko Imamu/padre wa bara.. Huwa si watu wa kuaminika hata kidogo. Ushahidi huu hapa.
 
Kujiuzuru!!!
Hapa naona uzanzibar na ubara unaingia kwa kasi sana
 
Kuhusu Ubaguzi wa Maalim hiyo ni dhairi kabisa wala halihitaji tochi kwani hata hiyo Cuf kuwa bara ni kwa vile tu sheria ya usajili wa vyama vya siasa inalazimisha chama kuwa katika sura ya muungano maana hata kwenye uchaguzi nguvu kubwa imeelekezwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na bajeti kubwa inatengwa huko kuliko bara hivyo maalim Seif haoni hasara Cuf bara ikafa na hilo lingine ni jambo linafanywa kimkakati zaidi kijuu juu huwezi kuona
Siwezi kuliona lakini wewe umeliona! ishu ya CUF kuwa na nguvu kule haikwepeki kutokana na jiografia ya nchi hizi mbili...hata CDM haina nguvu kule kwasababu zile zile
Unajaribu kuinasua ccm kwenye hili jambo sijui kwanini....hivi kati ya ccm na Chadema ni nani ambaye anataka Cuf iwe distablelised? hili halihitaji kuumiza hata kichwa
 
CUF inahitaji mtu kama Maalim Seif siyo pr njaa, kuendesha upinzani Afrika siyo kazi nyepesi ati . Tatizo huwa chama tawala kuweka mapandikizi.Viva Seif, viva UKAWA.
 
CUF inahitaji mtu kama Maalim Seif siyo pr njaa, kuendesha upinzani Afrika siyo kazi nyepesi ati . Tatizo huwa chama tawala kuweka mapandikizi.Viva Seif, viva UKAWA.
Ccm inajua wazi nguvu ya CUF visiwani na nguvu ya CHADEMA bara ! Kushamiri kwa hivi vyama kila upande kwa vyovyote vile sio habari njema kwa ccm
 
Upeo wako ni mdogo., siku zote ni bora chama kuliko yooote hayo uliyoeleza, chama kibaki hai na salama kisiasa ndio kitu nyeti tunachoangalia.,

Tanzania ni kubwa, wasomi wapo wengi, there are so many Prof.Lipumba, hao kina Sekaya ndo kabisa, ni bora kujenga chama kikawa imara zaidi. Lipumba aanzishe chama chake na taasisi yake huko Bara, ukitaka kujuwa kilichomkuta HR Lipumba ni zaidi. HR alitarajiwa kuwa mrithi wa maalim seif leo Zanzibar ukimtaja HR hakuna anayemjuwa ni kwa sababu chama kilifanya maamuzi magumu na kuijenga CUF ya sasa.

CUF tokea imeanzishwa ni chama pekee cha upinzani Tz kilicho madhubuti na kinazidi kupiga hatua kila uchao. Katika taasisi hakuna mtu mkubwa zaidi kuliko taasisi, Lipumba alihisi CUF ni yeye na yeye ndo CUF. mwache ajifunze aendako.
Naona fikra kiduchu ndizo zinazokuhangaisha. Kama ungekuwa na upeo thabiti ungaliona jinsi katiba inavyonyong'onywezwa na kufinyangwa. Mwanzoni mlinyanyasa sana Mzee James Mapalala mpaka akakata tamaa na akaamua kuondoka, lakini kwa huu mziki ulivyo mnene, HATOKI MTU!
 
Back
Top Bottom