CRISTIANO RONALDO For Ballon D'Or 2013

CRISTIANO RONALDO For Ballon D'Or 2013

Wanaopinga Ronaldo kuchukua hiyo tuzo ni either,
1).Hawajui soka/hawafuatilii soka

2).Hawako objective na wanaleta ushabiki tu.

Mimi pia ni mpenz sana wa L.Messi ila Ronaldo anastahili kabisa hii tuzo this time around.Period.
 
FIFA wamemsahau kabisa.Maradona....Badala yake wanamtukuza Pele...

Chifu, hiyo tuzo ndio kwa mara ya kwanza...naamini siyo Maradona tu, hata greats wengine ambao hawajawahi kushinda tuzo ya Ballon d'Or watakuwa wakipewa hiyo tuzo ya heshima....

Ila kwa upande mwingine chifu, unajua wenzetu wanapenda watu ambao watakuwa na mfano mzuri kwa watoto wao, watu ambao watoto wao wakiwaangalia, wanatamani kuwa kama wao.....sasa huyu bwana Maradona na ujunkie wake, nani kweli atapenda awe idol kwa mtoto wake? Mi naamini hilo la ujunkie limemwaribia sana Maradona, otherwise nakumbuka kwenye lile shindano la nani bora kati yake na Pele (katika karne ya 20), kura zilitoka droo, na hivyo kupelekea FIFA kuwapa wote....
 
Mmoja mmoja, Messi hana wa kufanana nae kati yao, ila kwa vigezo vinavyomfanya mchezaji kuwa bora wa Dunia, Ribery ana vigezo vyote kwa mwaka 2013 in fact Ronaldo hakutakiwa hata kuwepo kwenye tatu bora because he won nothing in 2013
Nadhani huo ni mtizamo wako mkuu....

Kwa mmoja mmoja mwingine atasema Ronaldo hana wa kufanana nae....Mwingine atasema Messi hana wa kufanana nae...Mwingine atasema Ribery hana wa kufanana nae.....

Una uhakika kwamba kigezo cha kuchukua Ballon D'Or ni mpaka mchezaji awe amechukua Kombe la aina yoyote?...

Hebu tupe vigezo rasmi vya mchezaji kushinda Ballon D'Or mkuu....

The FIFA Ballon d'Or (French pronunciation: ​[balɔ̃ dɔʁ], "Golden Ball") is an association football award given annually to the player who is considered to have performed the best in the previous year. It is awarded based on votes by coaches and captains of international teams, as well as journalists from around the world.
The award started in 2010 after France Football's Ballon d'Or and the men's FIFA World Player of the Year award were merged. The winner of the inaugural 2010 FIFA Ballon d'Or was Lionel Messi who then went on to reclaim the title the following two years. After the merger, the FIFA World Player of the Year award became a women-only award.
 
Chifu, hiyo tuzo ndio kwa mara ya kwanza...naamini siyo Maradona tu, hata greats wengine ambao hawajawahi kushinda tuzo ya Ballon d'Or watakuwa wakipewa hiyo tuzo ya heshima....

Ila kwa upande mwingine chifu, unajua wenzetu wanapenda watu ambao watakuwa na mfano mzuri kwa watoto wao, watu ambao watoto wao wakiwaangalia, wanatamani kuwa kama wao.....sasa huyu bwana Maradona na ujunkie wake, nani kweli atapenda awe idol kwa mtoto wake? Mi naamini hilo la ujunkie limemwaribia sana Maradona, otherwise nakumbuka kwenye lile shindano la nani bora kati yake na Pele (katika karne ya 20), kura zilitoka droo, na hivyo kupelekea FIFA kuwapa wote....
Nimekusoma Chifu.....

Maana yangu ilikuwa ni kwamba FIFA wanamtenga sana Diego kwenye events zao....Hasa Ballon D'Or
 
CR7.jpg
 
Nadhani huo ni mtizamo wako mkuu....

Kwa mmoja mmoja mwingine atasema Ronaldo hana wa kufanana nae....Mwingine atasema Messi hana wa kufanana nae...Mwingine atasema Ribery hana wa kufanana nae.....

Una uhakika kwamba kigezo cha kuchukua Ballon D'Or ni mpaka mchezaji awe amechukua Kombe la aina yoyote?...

Hebu tupe vigezo rasmi vya mchezaji kushinda Ballon D'Or mkuu....

The FIFA Ballon d'Or (French pronunciation: ​[balɔ̃ dɔʁ], "Golden Ball") is an association football award given annually to the player who is considered to have performed the best in the previous year. It is awarded based on votes by coaches and captains of international teams, as well as journalists from around the world.
The award started in 2010 after France Football's Ballon d'Or and the men's FIFA World Player of the Year award were merged. The winner of the inaugural 2010 FIFA Ballon d'Or was Lionel Messi who then went on to reclaim the title the following two years. After the merger, the FIFA World Player of the Year award became a women-only award.

Inawezekana me sijui kuwa vigezo vimekuwa vipya na kwamba hii zawadi ilianza mwaka 2010 ndio maana sijui hivyo vigezo vipya vilivyoanzishwa mwaka 2010
 
Hakika Ronaldo alistahili hii tuzo kwa mwaka 2013. Messi ni mchezaji mzuri sana lakini mwaka huu haukuwa mzuri kwake. Ribery angalau kwakua amechukua makombe mengi lakini hicho nacho si kigezo conclusive!!! Ronaldo alithibiti kama jeshi la mtu mmoja kweli, alipokosekana uwanjani madrid walitetereka, amefunga magoli muhimu katika mechi zote muhimu za madrid na Portugal...tukumbuke mashabiki wa Madrid walimzodoa special1 kwa Madrid kumtegemea sana cr7. Timu ya Munich ilikua vizuri sana msimu huu. Karibu kila mchezaji alikua kwenye peak ya carier yake. Hii imesababisha mchango wa Ribery kutokua wazi compared to cr7 ambaye madrid ilikua inasuasua!! Hakuna uchakachuaji kama watu wengine wanavyosema hapa. Ronaldo hajashinda kwa kura 100% ila wengi waliona yeye anafaa. Wengi wape. Congrats cr7. Tuthibitishie tena 2014
 
YAAN Kama CR 7 akibeba leo.... nitaamini kuwa hizi tuzo si za ubora ni za siasa.... Yaan watu hawapimi mafanikio yake ila wanataka achukue kwa sababu tu ajilinganishe na MESSI.....

Ribery akikosa nachana bendera ya FIFA kwa hasira zangu.... Maana kwa vigezo huyu jamaa anastahili mwaka huuu si Ronaldo wala MESSI.... tena bora hata MESSI arudie tena kuliko CR maana hana kombe lolote alilobeba...

Watu mna mahaba popo kweli.. MFUKUZI
Mwaka 2010, Iniaesta,Xavi,Casilas walibeba kombe la dunia kwa kandanda safi,Messi na Algentina ya Maradona walikula kichambo cha mabao manne nunge kwa mkoloni Germany,
Haya,Champions League Morinho aliibeba na Intermilan,na Mtaalam snejder akiwa kwenye Form,na Snejder alifika final world cup,
bado Ballon d'or alipewa Messi,leo mnaongea nini@
cc: Mourinho, Gang Chomba, #teammahabapopo ...
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana me sijui kuwa vigezo vimekuwa vipya na kwamba hii zawadi ilianza mwaka 2010 ndio maana sijui hivyo vigezo vipya vilivyoanzishwa mwaka 2010
Mkuu naomba utuwekee hata vigezo vya zamani....Maana vinavyotumika ni vilevile vya 'FIFA Player of the year award' vilivyotumika mpaka 2009.....Kilichofanyika ni kuunganisha tu ile tuzo ya Ballon D'Or na 'FIFA Player of the year award' ...
 
Watu mna mahaba popo kweli.. MFUKUZI
Mwaka 2010, Iniaesta,Xavi,Casilas walibeba kombe la dunia kwa kandanda safi,Messi na Algentina ya Maradona walikula kichambo cha mabao manne nunge kwa mkoloni Germany,
Haya,Champions League Morinho aliibeba na Intermilan,na Mtaalam snejder akiwa kwenye Form,na Snejder alifika final world cup,
bado Ballon d'or alipewa Messi,leo mnaongea nini@
cc: Mourinho, Gang Chomba, #teammahabapopo ...

Kuna mtu alitetea huo uozo? Kwa hiyo kwa sababu FIFA walifanya uozo wakampa zawadi asiyestahili kwa hiyo na leo tukubali kuwa fifa wamefanya uozo na kumpa Ronaldo zawadi ya Ribery?

Two wrongs don't make it right
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naomba utuwekee hata vigezo vya zamani....Maana vinavyotumika ni vilevile vya 'FIFA Player of the year award' vilivyotumika mpaka 2009.....Kilichofanyika ni kuunganisha tu ile tuzo ya Ballon D'Or na 'FIFA Player of the year award' ...

Ni rahisi sana Mkuu, kabla ya kina Blatter kuchakachua hivyo vigezo, ni mchezaji gani prio to 2009 alipewa zawadi ya mchezaji bora wa Dunia bila kushinda chochote katika ngazi ya club au Taifa
 
http://www.fifa.com/mm/document/bal...2/26/02/68/fboaward_menplayer2013_neutral.pdf

Hiyo link ina file la pdf inaonesha jinsi kura zilivyopigwa

Tanzania (Captain -Juma Kaseja)
5 points-ronaldo
3points-messi
1point-van persie

Coach Tanzania Poulsen Kim
Messi Lionel
Cristiano Ronaldo
Ribéry Franck

Media Tanzania Wambura Boniface
Cristiano Ronaldo
Messi Lionel
Van Persie Robin

naona kura ya afisa habari wa tff na ya nahodha zilifanana.
hii ni hatua nzuri ya fifa kuondoa kelele za uchakachuaji kama za mwaka uliopita
 
Ni rahisi sana Mkuu, kabla ya kina Blatter kuchakachua hivyo vigezo, ni mchezaji gani prio to 2009 alipewa zawadi ya mchezaji bora wa Dunia bila kushinda chochote katika ngazi ya club au Taifa

Roberto Baggio mwaka 1993...

Binafsi si muumini wa hizi tuzo...

Mfano ni mwaka 2006 alipewa Cannavaro kisa tu alikuwa Nahodha wa Italy..WC winners
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom