CRDB wanavyotapeli Wanafunzi wa Vyuo Vikuu bila wao wenyewe kufahamu

Kumbuka hata hiyo statement ambayo ni halali yako kupata bure wamekuchaji hela. hapo ndio huwaga sielewagi hii nchi.
 
Bwana kiongoz pole Sana ndio Mana Mimi kwa miaka 5 nikiwa chuo najuta kutumia crdb Mana wameniibia pesa zangu balaa na nlipogundua skuwa na jins ya kubadil kutokana na kwamba akaunt yang ndyo ilkuwa linked had HELSB
 
Kama wadau walivyosema. Kuna mtu alivizia umeenda kuoga akachukua Cv..., Card number na exp. Tafuta mtu wako wakaribu anayetumia Iphone mtupe ndani.
 
Nakushauri usilaumu benk mojakwamoja. Fanya uchunguzi kuna mjanja anatumia credentials zako kufanya hiyo miamala
Kikulacho ki nguoni mwako
 
Itakuwa kuna mtu wako wa karibu kachukua kadi yako ya tembo card mastercard, kacopy namba za card na CVV, exp date, anajilipia tu online. Kuwa makini na kadi yako unless ina OTP kwamba mtu akitaka lipia kitu unapokea code kwenye msg au email ili uweke kukamilisha muamala kitu ambacho nadhan CRDB hawana.
 
Hili tatizo nishaona watu wanalalamika ila mimi situmii Crdb na sijajiunga Simbanking kwa ajili ya usalama zaidi. Sema hapa nimejua mengi
 
Ungemalizia kwa kusema "utanishuru baadaye" hapo kwenye I phone😄
 
Ahsanteni kwa muongozo wakuu.

Kupitia huu uzi nimejifunza mengi sana, nilikuwa siijui CVV nimeangalia hapa kwenye kadi yangu nimeona ipo baada ya kupata muongozo huu.

Kumbe kuacha wazi kadi ya bank kimasihara ni risk hivi.....
Siyo risk ndogo
 
Niko Standard Chartered, nako ni hivyo hivyo. Sijui pa kwenda. NMB nako hivyo hivyo. Hata kuangalia salio ni makato! Zamani pesa za wazee wetu zikiongozeka benki. Siku hizi haizongezeki. Zinapungua!
maana haya mabenki yetu ya nyumbani ni KERO, yanapenda janjajanja sana,
 
Kimsingi kwa akaunti za wanafunzi hawatakiwi waweke makato na kama yatakuwepo inatakiwa yawe kidogo sana, kwa sababu hiyo akaunti siyo ya mfanyakazi au mfanyabiashara ambao wana vyanzo vya mapato.......kama umegundua kuna makato makubwa, tafuta benki ambayo ina operate student accounts, unaweza kujaribu NMB au Equity na unapofungua wataarifu kwamba unafungua akaunti ya mwanafunzi, wanaweza kukwambia upeleke barua ya utambulisho kutoka chuoni au vinginevyo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…