CRDB wanavyotapeli Wanafunzi wa Vyuo Vikuu bila wao wenyewe kufahamu

Igande

Member
Jun 10, 2021
41
60
Habari za wakati huu Great thinkers!

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Ni kawaida kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa pesa kutoka katika account zao za benki kidogo kidogo.

Huo ndio mwanya wanaotumia CRDB kuwatapeli fedha zao, kivipi?

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS). Mara nyingi, kama ilivyo kwa wanafunzi wengi, natoa pesa kidogo kidogo. Hilo hupunguza hata risk ya kuibiwa, natoa pesa ambayo nina matumizi nayo tu!

Tangu naanza kupokea Boom la kwanza, nilikuwa na wasiwasi kwamba pesa yangu inapungua. Lakini pasipo kufuatilia na pasipo kujua nika'assume' kwamba itakuwa nyingine inaishia kwenye makato!

Lakini ile hali ya kwamba pesa inapungua haikunipa amani kabisa!

Baada ya Boom la mwisho kwa mwaka huu ambapo kwa MUHAS tunapokea Takribani Tsh 665,000/= nikatoa laki 3 kwa ajili ya kulipa madeni na matumizi mengine.

Nilipokuja kutoa tena kiasi cha fedha elfu 50, nikashangaa kuona imebaki 190,000/=!! Hata kama ni Makato yanakuwaje makubwa hivi?

Nikaenda kuwauliza CRDB Kariakoo Branch wakasema hawawezi kunisaidia labda niende kwenye Bank niliyosajilia bank account yangu. Hivyo basi nikaenda Azikiwe branch na baada ya mvutano mrefu mwisho wakaniambia niombe bank statement.

Nikaomba ya June na July, nilichokikuta ndio hicho hapo chini! Hizo sehemu zenye duara ni malipo madogo madogo ambayo sija yafanya na wanadai nimeyafanya.

Ikumbukwe kwamba sijalipia premium kwenye App au sehemu nyingine yoyote na wala sifanyi manunuzi ya mtandaoni.

Itoshe kusema kwamba, CRDB ni wezi! Na huenda ikawa wanaibia wengi kwa staili hii hii bila wao wenyewe kujua. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wanafunzi wengi sio wafuatiliaji.

Na je, hivi ni kweli hizi Tembo card zinaweza kutumika kwenye kulipia malipo ya mtandaoni? (iTunes)

Nimelileta hili jukwaani, ili watu walitambue. Binafsi nitaangalia namna ya kuwahama japo ni process ndefu kwa mujibu wa taarifa nilizopewa. Lakini je, huko kwingine vipi?

Inauma sana!
 
St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,661
11,051
Hio bank statements haioneshi yote nilikuwa nataka kuangalia muda wa kutoa(matumizi) ili ujuwe huo muda ulikuwa shule? Kazini? Namaanisha mazingira ya wewe kuwa huwezi kufanya muamala bali kuna mwizi ndio aliefanya huo muamala.

Jengine la kufanya jaribu kuificha debit card yako inawezekana kuna chali kishakopi na kuitumia kama yake.

Lunatic
 
B I N A M U

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
1,500
2,316
Iyo ni scam kiongozi wala hata sio CRDB ndio maana benki kama DTB card zao hazifanyi online payments ukitaka kufanya online payments inabidi upate mastercard ambayo ni kama wallet wala haihitaj uwe na account. Pole sana aise
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
5,194
6,600
Ila ukiomba foottage za siku ambazo sio wewe uliyetoa ATM si utamuona aliyetoa au haiwezekaniki hiyo Mkuu?
 
Igande

Member
Jun 10, 2021
41
60
Pia itune uwa inatabia ya kufanya automatic subscription na hapo kwenye statement yako naona transactions zako ulizozungushia karibu zote ni bills za itune
Mkuu, subscription inaweza kufanyika hata kama sijatoa taarifa zangu za bank? Na hata hiyo Application ya iTunes sina kwenye simu yangu, hilo linawezekana vipi?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Igande

Member
Jun 10, 2021
41
60
Hio bank statements haioneshi yote nilikuwa nataka kuangalia muda wa kutoa(matumizi) ili ujuwe huo muda ulikuwa shule? Kazini? Namaanisha mazingira ya wewe kuwa huwezi kufanya muamala bali kuna mwizi ndio aliefanya huo muamala.

Jengine la kufanya jaribu kuificha debit card yako inawezekana kuna chali kishakopi na kuitumia kama yake.

Lunatic
Daaah ila anaweza vipi kuitumia kama hajui namba ya siri?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,044
6,834
Habari za wakati huu Great thinkers!

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada...
Wala sio uongo, mimi sio mwanachuo ila nime experience wizi kwa staili ya kutoa pesa kidogo kidogo.

Huwa natoa yote na afadhari nitunze kwenye simu kwenye makato makubwa nakuwa na amani na mchanganuo wa makato kuliko wizi wanaoufanya watu wa benki. Ni wapumbavu sana hao.
 
Igande

Member
Jun 10, 2021
41
60
Iyo ni scam kiongozi wala hata sio CRDB ndio maana benki kama DTB card zao hazifanyi online payments ukitaka kufanya online payments inabidi upate mastercard ambayo ni kama wallet wala haihitaj uwe na account. Pole sana aise
Asante mkuu. Ila bado mimi nawaza ni hawa hawa CRDB ndio wezi wangu

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,307
8,056
Asante mkuu. Ila bado mimi nawaza ni hawa hawa CRDB ndio wezi wangu

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Wala sio uongo ,mimi sio mwanachuo ila nime experience wizi kwa staili ya kutoa pesa kidogo kidogo.

Huwa natoa yote na afadhari nitunze kwenye simu kwenye makato makubwa nakuwa na amani na mchanganuo wa makato kuliko wizi wanaoufanya watu wa benki.Ni wapumbavu Sana hao.
Kwenye simu huku si salama pia ni rahisi kupigwa
 
spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,154
4,397
Habari za wakati huu Great thinkers!

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Ni kawaida kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa pesa kutoka katika account zao za benki kidogo kidogo.

Huo ndio mwanya wanaotumia CRDB kuwatapeli fedha zao, kivipi?

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS). Mara nyingi, kama ilivyo kwa wanafunzi wengi, natoa pesa kidogo kidogo. Hilo hupunguza hata risk ya kuibiwa, natoa pesa ambayo nina matumizi nayo tu!

Tangu naanza kupokea Boom la kwanza, nilikuwa na wasiwasi kwamba pesa yangu inapungua. Lakini pasipo kufuatilia na pasipo kujua nika'assume' kwamba itakuwa nyingine inaishia kwenye makato!

Lakini ile hali ya kwamba pesa inapungua haikunipa amani kabisa!

Baada ya Boom la mwisho kwa mwaka huu ambapo kwa MUHAS tunapokea Takribani Tsh 665,000/= nikatoa laki 3 kwa ajili ya kulipa madeni na matumizi mengine.

Nilipokuja kutoa tena kiasi cha fedha elfu 50, nikashangaa kuona imebaki 190,000/=!! Hata kama ni Makato yanakuwaje makubwa hivi?

Nikaenda kuwauliza CRDB Kariakoo Branch wakasema hawawezi kunisaidia labda niende kwenye Bank niliyosajilia bank account yangu. Hivyo basi nikaenda Azikiwe branch na baada ya mvutano mrefu mwisho wakaniambia niombe bank statement.

Nikaomba ya June na July, nilichokikuta ndio hicho hapo chini! Hizo sehemu zenye duara ni malipo madogo madogo ambayo sija yafanya na wanadai nimeyafanya.

Ikumbukwe kwamba sijalipia premium kwenye App au sehemu nyingine yoyote na wala sifanyi manunuzi ya mtandaoni.

Itoshe kusema kwamba, CRDB ni wezi! Na huenda ikawa wanaibia wengi kwa staili hii hii bila wao wenyewe kujua. Hiyo ni kutoakana wanafunzi wengi sio wafuatiliaji.

Na je, hivi ni kweli hizi Tembo card zinaweza kutumika kwenye kulipia malipo ya mtandaoni? (iTunes)

Nimelileta hili jukwaani, ili watu walitambue. Binafsi ntaangalia namna ya kuwahama japo ni process ndefu kwa mujibu wa taarifa nilizopewa. Lakini je, huko kwingine vipi?

Inauma sana!

View attachment 1871552
Mkuu bila kujari,twende kidogo kidogo pande zote mbili,huenda tukapata jibu tu....,

umeshawahi kutumia bidhaa yeyote ya Iphone/Apple toka umeanza kumiliki hio card?

Kuna swali pia umeuliza kuhus tembo card.....Jibu lake.
Tembo card iloyounganishwa na Visa/Mastercard inaweza kufanya malipo ya mtandaoni ikiwa tu imeunganishwa na banki kufanya huduma hiyo.

Naomba nikuulize swali la pili?
Kadi yako ya benki ina nembo ya Via card /Master card?
NOTE
Haya maswali mawili yatasaidia kutatua tatizo lako,kwa kuanzia
 
miamia100

Senior Member
Nov 13, 2019
139
101
Nilikuwa nina taratibu ya kupokea fedha kutoka ughaibun kwa kipindi kirefu cha ajabu zilikuwa zinaisha tu bila utaratibu nikagundua naibiwa mpaka nimehamia wordremit CRDB wabaya sana
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
7,661
9,479
Mkuu

Kama ulijiunga na Internet Banking na ukaruhusu malipo ya online ni rahisi sana kuibiwa

Kufanya malipo online mtu anahitaji namba ya Visa/Mastercard na CVV [Card Verification Code], ile number inakuwa na digits 3 nyuma ya kadi. Mtu akiona tu kadi yako na akachukua hizo details anafanya malipo bila ya kuwa na password yako.

1627473211869.png
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Top Bottom