CRDB BANK si Bank ya kuiamini kabisa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB BANK si Bank ya kuiamini kabisa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by manuu, Feb 23, 2012.

 1. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Miezi kama sita iliyopita nili deposit shiling milion moja kwenye account yangu ya hapo CRDB jana nikaenda pale kutaka kuchukua kiasi fulani cha fedha nikaomba bank statement yangu,nikapewa balance inaoonyesha nina shilingi elfu kumi na mbili tu.

  Sikuamini nikamuuliza yule bwana mbona niliweka shilingi milion moja mwezi wa tisa na kwenye account nilikuwa na elfu ttemanini kabla sija deposit hiyo pesa? Jamaa akacheck akaniambia inaonekana hiyo pesa ilichukuliwa kwa njia ya ATM machine kataika awamu mbili tofauti.

  Nikamwabia aliechukua ni nani sababu mi sijawai kuja chukua hiyo pesa, nikamwambia si kwenye ATM machine kuna camera yenye uwezo wa ku track matukio yote ya hapo check ili tuone aliechukua hiyo pesa jamaa akachek baada ya mda akaja na kuniambia aliechukua inaonekana alikuwa amejitanda kitu kichwani na picha haipo clear.

  Nikamsisitiza anionyeshe hiyo picha kama ni mtu wa kwenye familia yangu nitmjua hata kwa umbo jamaa mara aingie ndani atoke bila majibu ya maana.Nikamwambia aniruhusu kama yeye ishu ameishindwa niende kwa meneja jamaa(bank teller) akaniambia nisubiri ila mpaka ikafika saa kumu na moja walikuwa hawajanipa jibu la nani kachukua pesa yangu.

  Akawa ameniambia leo nirudi pale bank tuweze kucheck tena. Kwa bahati mbaya leo nilikuwa nasafari ya siku kama saba ndio nitarejea hivyo sikuweza kwenda pale.

  Maswali mengi nilijiuliza sana je kuna mtu mwingine alishapatwa na shida kama hii? Na ni hatua gani ntaweza kuzichukua pindi nitakapo rudi kama hawatanipa majibu ya kutosha?
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kimei asipoangalia CRDB inakokwenda siko. Kama na gadgets walizo nazo wameshindwa kubaini mtu aliyeingia kwenye akaunti yako na kuchota hela basi security ya hela zetu hasa hizi za mishahara ya kutunzia familia iko hatarini mno.

  CRDB kuna uzembe mkubwa sana siku hizi haswa wa kukatika mitandao na nafikiri ktk wakati kama huu ndo huwa hizi hela zinachotwa sana.

  Hatujaamua kufuatilia kwa karibu fedha zoote tunazoweka kama hatuibiwi ila najua tukianza kufuatilia shs kwa shs tutakuta wizi unaofanywa au uzembe ni wa mamilioni
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Pole sana...

  Hiyo ndio bank ambayo karibu madili yote ya EPA yalipigiwa humo. Kuna sister mmoja aliwahi kupigwa chini kazi CRDB kwa kosa la kujikopesha hela za wateja bila wao kujua. Eti kama kuna mkwanja halafu hakuna activity muda mrefu wanadhani umekufa wanaanza kujikopesha huku wanaskilizia...
   
 4. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Unaweza ukailaumu bank wakati kosa ni la bank teller..mara nyingi hawa ma bank teller ndo wanaopiga deal zote...nakushauri kama una deposit slip ya ile cash 1million,na ile bank statement uliyopewa unayo then hakuna haja ya kumfuata bank teller tena nenda direct kwa Manager wa customer service wa tawi lako...yeye ataweza ku-track na pengine ukarudishiwa fedha zako..
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Somo lingine wakuu, kama una hela nyingi usiwe unatoa kwa ATM. Wafanyakazi wa benki wameanzaisha kamtindo ka kuiba hela kutoka kwenye akaunti zilizonona za wateja wakijua kuwa mhusika huwezi gundua wizi huo hasa kama una mazoea ya kwenda kutoatoa hela kwa ATM. Wajanja wanaenda kaunta unatoa hela ya kutosha kwa matumizi ya wiki 2 au 4 na unahakikisha una-note somewhere amount na siku uliyotoa hela.

  Wakigundua hutumii ATM kudroo hela huwa wanaogopa wanajua lazima utakuwa unatunza kumbukumbu tu!
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kimei asidhani issue ya EPA imekufa, lazima tuzae naye tu, labda afe kabla dogfathers wake hawajapoteza mamlaka
   
 7. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Waweza kuwa wizi kweli huo? Waache utani na milioni moja ya Bongo ya sasa...wakomalie wakupe chako
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Ina maana huyo Bank Teller siyo mfanyakazi wa CRDB? kiasi cha kumtenganisha na bank kama ulivyosema? Mi naona kama bank teller ni wa CRDB basi CRDB inahusika kwani ndiyo mwajiri wake na huwe separate hivi vitu. kama ni kuwajibika ni CRDB kama bank na siyo teller.
   
 9. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa hii insight mkuu na kama mambo yataendelea hivi basi tutarudi mwaka wa 40 kulipiwa mishahara madirishani na kuhifadhi fedha mvunguni na kwenye vyungu
   
 10. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani bankteller kaajiriwa na nani? Mimi ilishanitokea nikaishiwa kuonyeshwa picha ambazo mpaka leo nawatafuta wezi wangu maana wako watano tofauti
   
 11. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Ushauri Mzuri.
   
 12. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hata NBC, wife wangu alishalizwa 1m kwa njia hiyo hiyo ya ATM.picha wanasema haipo clear.jee wanazi install za nini?
   
 13. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Na hata mimi nilipata wasiwasi huo kwa sababu yule bank teller nilimwambia naenda kwa meneja akapata kigugumizi.
   
 14. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Ni balaa aisee,yaani imenipotezea concetration ya safari kabisa.
   
 15. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Inawezekana sana hii mtu usipo onekana mwezi tu wanajua ushagongwa na Toyo.
   
 16. m

  mob JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  mimi hawa jamaa wamenizinguaga zana nikaamua kwenda kuchukua hela zangu na kuzipeleka DTB na exim wana usumbufu then ukiwauliza wanacheka
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  exim weziiiiiii pambav
   
 18. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Jamani hili swala la watu kuchkua hela kwenye akaunt za wateja wa crdb kwa ss limekamata sasi 3 weeks ago kuna shemeji yangu kaibiwa laki8 kwenye akaunt yake through atm 2 weeks ago shangazi yangu anaishi kule lembeni kaibiwa pesa zake kwenye akaunt yake! Cha ajabu mwanae kufwatilia anaona zmeibiwa hapa dar through atm! Nadhani ni mpango wa ndani na ma it wa hapohapo crdb!
   
 19. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu mimi hili jambo nilistukia siku nyingi sana nilichofanya nilienda pale dar worth nikanunua safe yangu nikaanza kudroo pesa zangu mpaka zikabaki 5000/= nikaenda kuzifungia kwenye safe yangu na share zao ambazo nilinunua wakati wa IPO nikapeleka orbit security nikauza zooote kabisa nikachukua zile fedha nikaenda kununua kiwanja. hii nchi imefika pabaya unaibiwa unaenda polisi hakuna anayekusikiliza jamani amkeni.
   
 20. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hapana sijam-separate,ni mfanyakazi ndio ila kama ameonyesha kusuasua kwenye kutoa information ambazo mteja anataka na kwakuwa manager wa customer service yupo hapo hapo tatizo litatatulika kwa urahisi zaidi...kwa mfano,pengine hizo fedha haziku tolewa kwenye ATM ya hilo tawi bali ATM ya sehemu nyingine.Kila ATM ina numba kupitia Manager wa customer service,atasoma kwenye bank statement yake numba ya ATM iliyotoa hzo fedha..ata-consult branch husika au atawa-consult watu wa IT kujua ni ATM ya wapi....ikionekana kuna zengwe the benk itakuwa liable...
   
Loading...