Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,413
- 31,402
Hapa kwetu kuna mabanda yalijengwa Muhimbili na Mloganzila, lakini kuna wakati tunakwenda NairobiRais Rajeolina mjanja sana. Yawezekana yeye hata kuionja hakuthubutu ila alijua wajinga wametamalaki miongoni mwetu na kweli kwa namna walivyoubugia huo ushombwe sina hamu. Kwa mbali nakumbuka kikombe cha babu na barabara ya kuelekea Loliondo ilivyochongwa haraka haraka ndani ya saa 24...masikini Wadanganyika, we never learn.
Rajoelina kauona ukweli kwa watu wake waliopoteza maisha sana na kwingine.
Hukusibiri ushuhuda kageuka nyuma na sasa kaiangukia WHO. Anataka chanjo.
Ni wakati sasa tupate chanjo. Makampuni ya dunia yametenga dozi milioni 400 kwa Afrika. Ni bure
Somalia na Al shabab wanatoa vaccine, sisi tunasubiri nini?
Mapapai hayafai wala mazoezi ya kukimbia si tiba! mvinyo wa NIMR hauna ithibati ni kama wa Madagascar
Tuukubali ukweli kwasababu umedhihiri, virus haihitaji mzaha malipo yake ni makubwa kwa watu wetu
Vaccine ililetwe wanaotaka wapate wasiotaka wasibughudhiwe