Gumzo la dunia hivi sasa ni kirusi cha Corona.
Kirusi hiki kimeleta kizaizai na sokomoko kila pembe ya dunia.
Nchini Marekani kuna sintofahamu kubwa.
Hakuna ajuaye mwisho wa huyu kirusi.
Hali hiyo imepelekea kutokea kitu kinachoitwa ‘panic buying’.
Sasa hivi ukienda kwenye maduka-masoko [supermarket] mengi kuna baadhi ya bidhaa kuzipta ni mbinde.
Bidhaa hizo ni kama karatasi za chooni, taulo za karatasi, jeli za kusafishia mikono, na kadhalika.
Rafu za maduka-masoko mengi zipo tupu. Hiyo ni kwa sababu watu wengi wanazinunua hizo bidhaa kwa wingi kuliko ilivyo kawaida. Jambo linalopelekea kuwepo na uhaba wa hizo bidhaa kwa sasa.
Hebu ona hizo rafu hapo chini. Ni kutoka duka-soko la Publix.
View attachment 1388155View attachment 1388157View attachment 1388158View attachment 1388159
Sielewi kwa nini watu wanakimbilia sana kuzinunua hizo bidhaa na kuzihodhi majumbani mwao.
Kwangu jambo lenye mantiki zaidi na bora ni kujiwekea akiba ya pesa kuliko kutumia pesa na kununua vitu ambavyo kama itatokea umeugua na hicho kirusi, havitakusaidia kupata nafuu.
Badala ya kununua dawa, watu wananua makaratasi ya chooni!
Halafu Wamarekani wana tabia ya ku-panic sana.
Corona siyo kiama. Lakini jinsi watu wanavyofanya mambo hivi sasa, utadhani kiama ndo kimefika.
Sielewi. Na wala siogopi.
I ain’t never scared 💪🏿