Coronapocalypse

Coronapocalypse

Sasa Ulaya baadhi ya supermarkets wameamua kufungua saa moja kabla ili kuruhusu wazee tu kufanya shopping
Maana wanaonewa sana kwa kweli
Kweli hawa watu wako mbele kwa kila kitu
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
halafu hii panic nahisi ni sisi wa mjini tu ambapo kwasasa kila mtu ni korona korona ilimradi kaongea, ila ndugu zangu wa vijijin uko wao habar wameskia lakini maisha yanaendelea bila panic yoyote
kwa mfano ivi wamasai ndani uko wanaweza kujadili hii kitu kwa ata lisaa😊😊😊
 
Wanao recover wanakuwa na 30% reduced lung function na wana gasp for breath hasa wanapotembea kwa kasi
Je! Hali Yao inaweza kurejea Kama ilivyokua awali?, Maana uingereza tumeona baadhi ya wanamichezo Kama vile Odoi na Kocha wa Arsenal vipi imekaaje hio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana corona imekuzwa na kutangazwa sana kulinganisha na Ebola ambayo ni hatari zaidi. Ila Ebola imebaki kama ugonjwa wa Africa. Ma celebrity wengi wamepata corona, ingekuwa hao ma celebrity wamepata Ebola sijui ingekuwaje !!!
 
Gumzo la dunia hivi sasa ni kirusi cha Corona.

Kirusi hiki kimeleta kizaizai na sokomoko kila pembe ya dunia.

Nchini Marekani kuna sintofahamu kubwa.

Hakuna ajuaye mwisho wa huyu kirusi.

Hali hiyo imepelekea kutokea kitu kinachoitwa ‘panic buying’.

Sasa hivi ukienda kwenye maduka-masoko [supermarket] mengi kuna baadhi ya bidhaa kuzipta ni mbinde.

Bidhaa hizo ni kama karatasi za chooni, taulo za karatasi, jeli za kusafishia mikono, na kadhalika.

Rafu za maduka-masoko mengi zipo tupu. Hiyo ni kwa sababu watu wengi wanazinunua hizo bidhaa kwa wingi kuliko ilivyo kawaida. Jambo linalopelekea kuwepo na uhaba wa hizo bidhaa kwa sasa.

Hebu ona hizo rafu hapo chini. Ni kutoka duka-soko la Publix.

View attachment 1388155View attachment 1388157View attachment 1388158View attachment 1388159

Sielewi kwa nini watu wanakimbilia sana kuzinunua hizo bidhaa na kuzihodhi majumbani mwao.

Kwangu jambo lenye mantiki zaidi na bora ni kujiwekea akiba ya pesa kuliko kutumia pesa na kununua vitu ambavyo kama itatokea umeugua na hicho kirusi, havitakusaidia kupata nafuu.

Badala ya kununua dawa, watu wananua makaratasi ya chooni!

Halafu Wamarekani wana tabia ya ku-panic sana.

Corona siyo kiama. Lakini jinsi watu wanavyofanya mambo hivi sasa, utadhani kiama ndo kimefika.

Sielewi. Na wala siogopi.

I ain’t never scared
Deal done wazungu washenz sana

kilicho akilini kitumie
 
Je! Hali Yao inaweza kurejea Kama ilivyokua awali?, Maana uingereza tumeona baadhi ya wanamichezo Kama vile Odoi na Kocha wa Arsenal vipi imekaaje hio.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mtihani, kwa sababu korona inaathiri hadi mapafu mbali na mafua ambayo yanasababisha upper respiratory symptoms.
 
Back
Top Bottom