KERO Halmashauri ya Jiji Dar ina mpango gani na Soko la Ilala Boma? Lina mazingira hatarishi kiafya

KERO Halmashauri ya Jiji Dar ina mpango gani na Soko la Ilala Boma? Lina mazingira hatarishi kiafya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimekuwa nikitembelea Soko la Ilala Boma kununua bidhaa za ndani kwa ajili biashara ya genge, sasa ni takribani miaka minne imepita. Kusema ukweli, soko hilo lipo katika hali mbaya licha ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
photo_2026-04-29_00-31-44.jpg

photo_2026-04-29_00-31-42.jpg
Katika kipindi hiki cha mvua, wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira yasiyo rafiki kutokana na matope yaliyotapakaa kila eneo. Changamoto hiyo pia inaaathiri hata sisi wanunuzi, ukitoka sokoni unakuwa hauna utofauti na mkulima aliyetoka kwenye jaruba la mpunga.

Mazingira ya soko hilo hayana miundombinu rafiki, jambo linalosababisha mvua zinaponyesha soko kujaa matope na maji machafu yaliyochanganyika na taka. Aidha, wafanyabiashara wengi hupanga bidhaa zao chini, hali ambayo ni hatarishi kwa afya za walaji.

Jambo la kushangaza ni kwamba Halmashauri hukusanya ushuru usiopungua Tsh 1,200 kila siku kutoka kwa kila mfanyabiashara anayepanga bidhaa zake katika soko hilo. Najiuliza fedha hizo zinaelekezwa wapi, ilhali miundombinu ya soko hilo imeendelea kuwa katika hali mbaya kwa miaka yote hiyo.

Nitoe wito kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuboresha miundombinu ya soko hilo ili liendane na hadhi ya jiji, ikizingatiwa kuwa soko hilo limekuwa lango muhimu kwa wafanyabiashara wanaochukua bidhaa kwa ajili ya kuuza katika masoko mengine kwa gharama nafuu.
photo_2026-04-29_00-31-32.jpg
photo_2026-04-29_00-31-39.jpg
photo_2026-04-29_00-31-36.jpg
 
Hahahaaa!! Hawana mpango kabisa kiongozi zaidi wanasema ombeni mvua zikate tu.Nguvu na akili ni kujenga ofisi za mkuu w mkoa kwa Billion 10+.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom