Corona: Tanzania yaingilia kati, madaktari wake wajitolea kwenda China kuidhibiti

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,238
Rafiki wa kweli ni wakati wa shida .

=====

SERIKALI ya China imeshukuru utayari wa Serikali ya Tanzania wa kutaka kuwapeleka madaktari nchini humo, kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid -19).

Aidha, imewatoa hofu Watanzania kuhusu changamoto za kibiashara na watalii kuingia nchini kutokana na kulipuka kwa virusi hivyo kuwa ni jambo la muda na vitaondoka muda si mrefu, hivyo kuwataka wafanyabiashara kuwa watulivu huku wakiwasiliana na wadau wao waliopo China.

Hatua hiyo imetokana na Rais John Magufuli, kumpa pole Balozi wa China nchini, Wang Ke kutokana na ugonjwa huo kuathiri kwa kiasi kikubwa nchi hiyo na kumueleza kuwa serikali iko tayari wakati wowote kupeleka madaktari kusaidia matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo, Balozi Ke alisema mbali na serikali kuwa tayari kupeleka madaktari, pia baadhi ya madaktari binafsi, waliandika barua kwa Balozi huyo, kuonesha nia na utayari wa kutaka kwenda kusaidia kutoa matibabu. Baada ya kuonesha utayari huo, aliwasiliana na serikali yake, waliopokea hatua hiyo kwa furaha na kueleza kwa wakati huu kuna madaktari wa kutosha 40,000 wa kutoa huduma, huku maambukizi ya virusi hivyo yakiendelea kupungua.

“Niliguswa sana pale Rais John Magufuli aliponiambia ‘kwa kuwa ndugu zetu wana uhitaji, tutapeleka madaktari kusaidia kupambana na virusi hivyo China wakati wowote’,”alisema.

Alieleza kuwa hatua hiyo ilionesha jinsi nchi hizo mbli, zilivyo na ushirikiano wa kudumu. Alisema kwa niaba ya serikali ya China, anashukuru utayari wa Tanzania kusaidia kupambana na ugonjwa huo.

Alisema kwamba nchi mbalimbali, zimekuwa pamoja na China kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo. Balozi Ke alisema kuna nchi zimewapatia misaada ya kifedha, kuwapatia barakoa (mask) na nguo kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa huo na vifaa mbalimbali. Alibainisha kuwa mpaka sasa, bado sababu za virusi hivyo, hazijagundulika kwani wanasubiri utafiti wa kisayansi.

Alitaka wafanyabiashara wa Kariakoo, wanaolalamikia mizigo yao kuzuiliwa nchini China kuwa wanatakiwa kutulia wakati tatizo hilo linaendelea kupungua na baadhi ya viwanda vya nchi hiyo kuanza uzalishaji, hivyo waendelee kuwasiliana na waliopo nje ya nchi.

Kuhusu usalama wa wananfunzi 400 waliopo katika jimbo la Wuhan, lililoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo, alisema kuwa wako salama na serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini China na vyuo wanavyosoma, wanaendelea kuwapatia huduma stahiki.

Alishauri kuwa ni salama, kuendelea kubaki katika jimbo hilo. Ke alitaja jitihada zilizosaidia kutokomeza virusi hivyo vipya duniani ni: Uongozi bora wa serikali, uliofanikisha kutoa taarifa za uwazi kwa ngazi zote, kujitoa kwa raia hususan wanasayansi na madaktari ambao 20 tayari wamepoteza maisha, njia za kisayansi kudhibiti ugonjwa huo na uwazi katika kupeleka taarifa.

Alishukuru jumuia za kimataifa kwa kusaidia kupambana na ugonjwa huo hatari. Alieleza kuwa hivi sasa China imeanza kudhibiti ugonjwa huo. Alitaka nchi za Afrika, kuungana kukabiliana na ugonjwa huo, unaosambaa kwa kasi duniani.
Wagonjwa wengine wamebainika katika hatua za mwisho kwa kutoonesha dalili. Alibainisha kuwa hivi sasa ushirikiano wa China na Tanzania, unaendelea kwenye miradi na uwekezaji, licha ya kuwepo changamoto katika biashara na utalii kutokana na ugonjwa huo.

“Matokeo haya mabaya ni ya muda. Tunaamini kuwa ugonjwa huu unazidi kupungua na uzalishaji utaendelea kama kawaida. Ushirikiano na urafiki kati ya watu wa nchi hizi mbili utaimarika zaidi,”alisema.

Daktari Mkuu Mshiriki katika Hospitali ya Nanjing China, Dk Li Ping alibainisha kuwa mpaka jana maambukizi ya watu 12,000 yamedhibitiwa nchini China huku kukiwa na vifo 3,051. Waliopona ni 52,109 na wengi wa waliokufa ni wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea.

Alibainisha kuwa watoto hawaathiriki. “Makundi yanayoathirika zaidi ni wazee wa kuanzia miaka 60 na walio na magonjwa sugu. Watoto wanaambukizwa kwa nadra, lakini dalili za ugonjwa kuchelewa kuonekana ndizo zinasababisha maambukizi kwa kiwango kikubwa,”alisisitiza.

Alipinga uvumi mbalimbali unaohusishwa na ugonjwa huo. Kwa mfano kuwa wako wanaosema “Unywaji wa maji moto huua virusi hivyo, kula vitamini C, kuvaa barakoa nyingi kuzuia ugonjwa, kutumia dawa za bakteria kuzuia maambukizi hayo au suala la wanyama wafugwao kueneza virusi”.

Alisema dalili za ugonjwa huo ni homa, kikohozi kikavu, uchovu, kiwango kidogo cha makohozi, ugumu wa kupumua, maumivu ya koo, pua kuziba na pua kutoa majimaji. Dalili hizo huonekana siku tano mpaka sita.

Alitaka wananchi kujikinga na ugonjwa huo, kwa kuosha mikono kwa kemikali au sabuni. Alisema kufanya hivyo kutapunguza athari. Alisema kugusa shavu baada ya kugusa sehemu ya maambukizi, husababisha kupata maambukizi.
Alitaja mbinu zingine za kujikinga kuwa ni:Kuacha madirisha wazi kupata hewa iingie na kutumia dawa kusafisha vitu vya ndani kama meza, viti na dawati. Mtu anapokohoa au kupiga chafya, ajifunike na kitambaa au karatasi na kisha kunawa mikono.

Alisema kutokana na virusi hivyo, kuambukizwa kwa njia ya matone ni vema kuwa mbali na watu kwa mita moja. Ikitokea una maambukizi, ni vema kuvaa barakoa unapotoka nje.

Chanzo: HabariLeo
 
Charity start at home!! Huku Lingusenguse hakuna Doctor hata mmoja tuna Med.Asst.tu ,please njooni kwanza huku,kueni kwenye border post hasa za aple namanga,tunduma, na nilitegemea watanzania hasa walioko kwenye lile jimbo la Wuhan watarudishwa nyumbani na kuwekwa chini ya uangalizi maalum for 21days kabla ya ku apply mind ya kuwaachia, na sijasikia kama tumeshaandaa isolations centres ndani ya nchi yetu kwa ajili ya kukabiliana na swala hii, kwangu mimi hii habari iliyochukua nafasi ya kwanza kwenye gazeti hili pendwa (!!!!) ni siasa zaidi kuliko reality.
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota nimeugua Corona acha watu wawe wananikimbia nikakumbuka ile video ilivuma sana ya "Ebolaaaa, ebolaaaa" 😂😂
 
Hongera sana wizara na wadau endapo litafanikiwa hili.Madaktari wasio na ajira ni fursa muhimu kwao, kwani kule wataliowa posho na mahitaji yote muhimu. Pia ni akiba nzuri kidiplomasia kesho yakitusibu tupate mkono wa karibu wa Mchina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom