Corona: Shule Afrika Kusini zafungwa tena

Corona: Shule Afrika Kusini zafungwa tena

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Moja kwa moja kwenye mada.

Afrika Kusini wamezifunga tena shule zote kwa mwezi mmoja wanapoendelea kupambana na ugonjwa huu.

Mapambano ni pamoja na tathmini ya wazi ya mirejesho pasipo na kujidanganya.

Korea kusini, China nk, nako wanapita katika hali kama hizo hizo.

Marekani ya Trump sasa kuvalia mabarakoa si hiari tena.

Antananarivo Madagascar hali si hali na mabarakoa sasa ni shuruti.

Tusimsubirie wa kumfunga paka kengele, lives of the people matter!

Hatumkomoi yeyote kwa kutozingatia masharti yaliyowazi ya kujikinga na kuwahami wengine na ugonjwa huu.

======

South Africa to Close Schools Again as Covid Infections Surge

Loni Prinsloo and Paul Vecchiatto

South Africa plans to shutter schools for a second time as the number of Covid-19 cases surges, according to two people familiar with the matter.

South African President Cyril Ramaphosa may announce the decision in a televised addressed at 8 p.m. in Pretoria on Thursday, the people said, asking not to be identified because the information isn’t public yet.

The closing of schools will be scheduled to coincide with an already planned break in early August, to reduce the impact of the shutdown on the academic year, the people said. Proposals put to the president include shuttering campuses for three weeks or longer, they said.

The number of confirmed coronavirus infections in South Africa doubled over the past 17 days to surpass 400,000. More than 13,000 cases were reported for a second consecutive day on Thursday, bringing the cumulative total to 408,052 -- the world’s fifth-highest. The government has forecast that the country is expected to reach its peak-infection rate in the coming weeks.

All schools were closed in March when the government introduced one of the world’s strictest lockdowns to curb the spread of the virus. Since they re-opened on June 1, teachers’ labor unions and some members of the public have urged the government to close them again.

While South Africa’s privately funded schools are well-resourced, there has been a concern around space in classrooms for physical distancing, and even water and sanitation in some of the nation’s public schools.

Source: Bloomberg
 
Kama sio rais wetu kuzuia misaada feki ya barakoa kutoka nje na sie nchi yetu ingekuwa na maambukizi ya juu sana
Hao Madagascar walivyojifanya kuwa wana dawa ya Corona, ndio wakapelekewa virus wa kufa mtu na dawa yao kimyaaaa

Corona imetengenezwa na imekuzwa ili watu wapige hela
 
Kwa mawazo ya kijima kama haya tutandelea kusikia taarifa za vifo vya ghafla visivyo na maelezo na kwa muda mrefu hadi nasi tutakapokuwa wahanga rasmi.

Hivi inachukua nini kuweka tahadhari au kuzuia?

Waliona mbali sana waliosema "usipoziba ufa utajenga ukuta."
 
Waje wajifunze Tanzania namna ya kuishinda Corona, hakika tumeishinda na maisha yanaendelea.. Wasione aibu waje tuwafundishe.
 
naomba kujua,unataka nchi hii ifanye nini kuhusu corona?,
pia,naomba kufahamu unapata faida gani kusema neno baya au lisilojenga juu ya nchi yako mwenyewe?,
itapendeza zaidi ukijibu bila jazba;

Mkuu sijui ni neno lipi baya au lisilojenga juu ya nchi yetu wenyewe unaolizungumzia wewe. Itapendeza kukusikia pasipo na jazba mkuu.

Kama nchi nini cha kufanya imeelezwa sana mkuu. Pasipo na kuyafanya maelezo hapa marefu mno. Kwa ufupi ni hivi:

"Kutambua kuwa huu ni ugonjwa tu kama ugonjwa mwingine (a health issue) ni suala la muhimu mno." Hakuna hujuma ya mtu wala taifa lolote dhidi yetu katika ugonjwa huu. Hili janga la mataifa yote. Haitusaidii kuishi in a state of denial.

Tukitambua hilo, kwamba tuna tatizo la kisayansi tuwaache sasa wenye taaluma zao watuongoze kushinda vita hivi, tutavishinda.

Kutokuwepo kwa jazba upande wako kutakuwa jambo la msingi sana mkuu kwani tunajenga nyumba moja.
 
Kwa mawazo ya kijima kama haya tutandelea kusikia taarifa za vifo vya ghafla visivyo na maelezo na kwa muda mrefu hadi nasi tutakapokuwa wahanga rasmi.

Hivi inachukua nini kuweka tahadhari au kuzuia?

Waliona mbali sana waliosema "usipoziba ufa utajenga ukuta."
Mkuu kwani wewe una corona mwanao je, mama ako au ndugu zako ? ukisikia kifo cha gafla hicho kilipangwa na Mungu mm najuan hamna corona kama ipo mashuleni watoto wangedondoka na kufa vyuoni , tuna ndugu zetru huko hamna hata aliye na mpango wa barakoa ila maisha yanaenda tu
 
Kwa mawazo yako unadhani tunaandika kutokea hewani?

Mkuu kwa hoja kama hizi nilileta uzi huu ili msome muelewe na muache kuuliza maswali kama haya:

Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

Hiyo ni kada moja tu. Unataka zote na za vigogo pia?

Waliopo kwenye orodha hiyo ni ndugu zetu, colleagues na marafiki zetu.

Unalo swali jingine?
 
Si mmoja, ni wengi. Wengi pia wamefariki.

Ni ajabu na kweli kuona nguvu kubwa inayowekwa kwenye kulazimisha kutokuwepo kwa tatizo ambalo walazimishaji wanajua kuwa lipo.

Tatizo haliondoki kwa jitihada za kulikataa.

Aliandika bwana mmoja (kiranga) hayo katika red (heshima kwake):

IMG_20200724_095942_863.jpg

Ni jambo la afya tu kujua mtanzania wa leo si wa jana na pia huwezi kuwadanganya watu wote siku zote.
 
Waje wajifunze Tanzania namna ya kuishinda Corona, hakika tumeishinda na maisha yanaendelea.. Wasione aibu waje tuwafundishe.

Pia usisahau tunaomboleza kifo cha Rais Mkapa kilichotokea leo hii RIP Mkapa
 
Back
Top Bottom