#COVID19 Corona ilivyonipa fundisho la maisha

Expensive life

JF-Expert Member
May 2, 2020
1,691
5,451
Janga la covid19 lilishika kasi hapa kwetu Tanzania mwanzoni mwa mwezi wa nne 2020 hapa ndio tahadhari zikaanza kuwekwa na serikali ikiwemo mikusanyiko na uvaaji wa barakoa.

Wakati janga hili linashika kasi, kampuni ambayo nilikuwa naifanyia kazi mkataba wangu wa kazi ndio ulikuwa ukingoni.

Kwa hali ivyokuwa nilijua tu kunalolote linaweza kutokea, kweli bwana kama nilivyowaza nakumbuka nikiwa naendelea na majukumu yangu ya kazi simu ya boss ikaingia akiniomba siku inayofuata tuonane, hapa kijasho kikanitoka.

Basi kesho yake asubuhi nikafika ofisini nikaendelea na majukumu yangu, mida ya saa saba mchana boss akaniita huku uso wake ukionesha kuwa huzuni fulani siyo kama nilivyomzoea, nikajua tu hapa sina changu.

Akaniambia kutokana na hali ilivyo tumeona tukusimamishe kazi kwa muda, sikuwa na jinsi nikakubaliana na hali ilivyo.

Kipindi nasimamishwa kazi wife alikuwa kwao alipata matatizo ya kifamilia baba yake alipata ajali mbaya iliyompelekea kukatwa mguu.

Nikamficha kuwa kazi nimesimama, baada ya muda akarudi ikabidi nimueleze hali halisi, akiba pesa nilikuwa nayo ya kula hata miezi sita mbele.

Kwa kuwa pesa nilikuwa nayo sikuwa na hofu yoyote, kutokana na janga la corona lilivyoshika kasi nikawaza nikifungua biashara nitapoteza tu pesa zangu kulingana na hali ilivyokuwa kipindi kile.

Siku zikasonga kumbuka pesa zinatoka tu haziingii, kibaya zaidi nikajiingiza kwenye betting hapa nilipingwa nikachakaa, miezi sita imepita nipo tu nyumbani.

..........Nitaendelea.........
 
Yaani uliposema tu habari za kubet ninajua kinachofuata huko mbele kwa stori yako
 
Back
Top Bottom