Namnukuu hayati Bob Marley aliposema "Sisimami upande wa Mungu wala upande wa Shetani,bali nasimama upande wa Haki".
Clouds media wameharakia sana kuanzisha TV station huku wakiwa hawana watangazaji wa uhakika,wenye vipaji mbali na elimu ya uandishi wahabari,mvuto (namna ya kumvutia mtazamaji atizame kipindi chako) na vingine vingi tofauti na EATV.Wakati anaondoka Salama ktk kipindi cha planet bongo,mtangazaji ambaye aliteka hisia za watu na kukamata mashabiki wengi wlompenda na waliomchukia,waliamua kufanya mchakato wa kumpata mrithi wake na katika huo mchakato wakapata vipaji vingine ambavyo vilikuja na mawazo mapya mfano Allan Lucky!
Cloudz inabidi wajifunze kupitia kwa watu na si kujiona wanajua kila kitu!