Copper Smelters around the World - Capacity less or equal to 100,000 tons per year

Kwa kufahamisha tena, ili kutunza mazingira kutokana na hiyo sumu, lazima hapo hapo kujengwe kiwanda cha kuzalisha sulfuric acid, hapo hapo ilikuzuia vumbi lazima kijengwe kiwanda cha kuzalisha gypsum. Inahitajika mtaji mkubwa sana
Hili suala ni la kitaaluma zaidi, ila ikiwekwa mihemuko ya kiasa hatutafanikiwa kabisa.

Ndiyo maana Nyerere aliwaza kuhusu mafuta baharini akasema yaacheni tu kwa sasa.
 
Mkuu Ndola Mine wanakiwanda cha kutengeneza sulfuric acid na inawaingizia pesa nyingi kuliko hata hiyo dhahabu tena wana export huko huko china nimefanyakazi pale miaka nane kabla ya kustaafu.
Mbona ore yao ni oxide, hiyo sulfur ya kuzalisha sulfuric acid wanaitoa wapi. Nifundishe na mimi niongeze ujuzi
 
mkuu technologia hiyo ya kuchengua ndio hiyohiyo inayotumiwa na masonara ambayo tunajifunza form two.
We jamaa unachekesha kweli!!! Eti tuliyojifunza form ii...nini? Electrolysis sio?

Yaani unataka kulinganisha smelting and (electro) plating?
 
Mkuu Ndola Mine wanakiwanda cha kutengeneza sulfuric acid na inawaingizia pesa nyingi kuliko hata hiyo dhahabu tena wana export huko huko china nimefanyakazi pale miaka nane kabla ya kustaafu.
Sawa mkuu ila unajua grade ya ore yao pale ni zaidi ya asilimia 85 copper.

Sasa kwetu ni 14-20%, hicho kiwanda hakitakua na faida.
Kumbuka wao pia husafirisha blister copper kwa ajili ya kuwa refined nchi za wenzetu. Waulize watu wa bandari dar watakuambia.
 
Mbona watu wagumu kuelewa. Tofautisha copper na copper concentrate. Mbona hizo hata bongo zipo na nishawahi kuelezea hapa. Kuna kampuni maeneo ya posta/mmnazi mmoja inaitwa danformation inafanya hiyo kazi. Hizo nchi ore yake ni copper oxide na ya Tanzania nyingi ni copper zenye sulfur.
Basi tujenge za kusafisha hizo copper zenye sulphur, kwanini hamtaki swala kuwa na chako badala ya kupangisha?! Kila mtu anataka aishi kwake, sijasikia mtu akidai anawo uwezo lakini atapanga na kugombana na mwenye nyumba mpaka afe wakati anaweza kuwa na boma lake, hata kama ni chumba na sebule, au kiwanda chake, taratibu mpaka kitakuwa kikubwa, tuanze na kidogo...
 
wacha porojo 85% copper? utakuwa mfanyakazi wa TMAA bashite kama bosi wako anaesema 90% ya container ni dhahabu
 
Basi tujenge za kusafisha hizo copper zenye sulphur, kwanini hamtaki swala kuwa na chako badala ya kupangisha?! Kila mtu anataka aishi kwake, sijasikia mtu akidai anawo uwezo lakini atapanga na kugombana na mwenye nyumba mpaka afe wakati anaweza kuwa na boma lake, hata kama ni chumba na sebule, au kiwanda chake, taratibu mpaka kitakuwa kikubwa, tuanze na kidogo...
Hata wao wamesema kama tuna uwezo tujenge. Ishu ni mtaji, wao hawataki wajenge halafu waingie hasara. Wao wanafanya biashara, ndio maana hata kule tulawaka waliona chenga wakaacha, leo Stamigold wanahangaika.
 
  • Thanks
Reactions: GSL
mimi naona ifikie hatua wataalamu wenye uelewa wa jambo hili na WENYE NIA NJEMA NA TAIFA HILI kujitokeza na kueleza hili jambo kinaga ubaga kwenye vyombo vya habari ili kuelimisha umma wa watanzania ambao wengi wetu ni mambumbumbu ambao tunaendelea kupumbazwa na wanasiasa ambao wana take advantage ya umbumbumbu wetu na sisi kwa sababu itikadi za siasa tumeziweka mbele basi ndio tunazidi kuliangamiza Taifa na kulifanya si sehemu nzuri ya kuishi kwa vizazi vijavyo.

Tanzania kwanza.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mkuu Ndola Mine wanakiwanda cha kutengeneza sulfuric acid na inawaingizia pesa nyingi kuliko hata hiyo dhahabu tena wana export huko huko china nimefanyakazi pale miaka nane kabla ya kustaafu.
Hiyo Ndola Mine wanafanya uchimbaji wa nini?

Nimekupa mfano ambao hata hapa Tanzania upo!!! Hapa kuna migodi kv Mara na mingineyo ambayo dhahabu inakuwa haipo embedded na madini mengine! Hawa hawana haja ya kusafirisha mchanga kwa sababu teknolojia hata ya hapa inaruhusu!!!

Hao unaowatolea mifano ni wazalishaji wa copper ambayo kwa kiasi kikubwa haipo embedded na madini mengine na ndio maana huwa wanamaliza kila kitu wenyewe kama wanavyofanya wachimbaji wengine wa dhahabu hapa Tanzania!!!

Issue ya Bulyanhulu na Buzwagi ni tofauti!!

Inawezekana ni kweli ipo cheap technology lakini by the time TMAA wametoa ile ripoti walikuwa sahihi!!! Hata ukiangalia kule Japan, zile copper concentrate zinatoka nchi mbalimbali including USA!! Wote hawa hawawezi kuwa wapumbavu!!!!

Indonesia na wenyewe walikuwa na tatizo kama la kwetu! Mwaka jana au mwakajuzi makampuni yakaungana pamoja na serikali kujenga mtambo wao wenyewe wenye uwezo wa kuchenjua tani 500K kwa mwaka kwa thamani ya USD 1.5 Billion!!

Hao nao tusidhani ni wapumbavu kwamba walikuwa wanapeleka China!!!
 
Ta

tizo ndiyo hilo ............. watu wanachanganya!!

Nilivyoelewa mimi migodi ipo hapa kwa ajili ya dhahabu. Baada ya kuzalisha hiyo dhahabu mchanga unaobaki huwa unakuwa na dhahabu kidogo na madini mengine kama shaba n.k. Sasa kwa technology iliyopo hawawezi kuextract hayo madini hapa ............ ndipo hapo suala la machanga kupelekwa nje linapokuja.

Lakini ukisikiliza sana watu humu kunaupotoshaji mkubwa!!

Siyo kwamba unabaki hiyo ni moja ya intended product na dhahabu kwenye huu mchanga iko chemically bonded na madini copper and the only way to separate them is smelting followed refining and lastly electrowinning to seperate copper, gold, silver etc
 
Mbona watu wagumu kuelewa. Tofautisha copper na copper concentrate. Mbona hizo hata bongo zipo na nishawahi kuelezea hapa. Kuna kampuni maeneo ya posta/mmnazi mmoja inaitwa danformation inafanya hiyo kazi. Hizo nchi ore yake ni copper oxide na ya Tanzania nyingi ni copper zenye sulfur.
Hayo mambo ni ya kitaalam ni vigumu mno kwa MTU wa kawaida kuyaelewa, Pyrometallurgy .
 
Kwa mara nyingine tena nadiriki kusema uzi huu unarudisha ile hadhi ya JF iliyojaa majadiriano ya kisomi. Nimefarijika sana kusoma mawazo ya kila mchangiaji na nimejifunza kitu kikubwa sana. Nawaombeni wachangiaji katika fani hii muendelee kutiririka ili sisi ambao hatujabobea tuelimike. Hongereni sana.
 
zambia wanzalisha makinia 15,000 wanachengua wenyewe tena malori ya hans pope ndio yanayoisomba kuileta dar sisi tunazalisha 25,000 tena tuko bandarini tunasema hatuwezi, hapa lazima tuna upungufu fulani vichwani mwetu.
mkuu huna haja ya kuchangia, sio lazima
 
The Top Copper Producing Countries In The World
Rank Country Copper Production (in thousand tonnes), 2014
1 Chile 5,750
2 China 1,760
3 Peru 1,380
4 United States 1,360
5 Democratic Republic of Congo 1,030
6 Australia 970
7 Russia 742
8 Zambia 708
9 Canada 696
10 Mexico 515
 
...Indonesia na wenyewe walikuwa na tatizo kama la kwetu! Mwaka jana au mwakajuzi makampuni yakaungana pamoja na serikali kujenga mtambo wao wenyewe wenye uwezo wa kuchenjua tani 500K kwa mwaka kwa thamani ya USD 1.5 Billion!!
Kumbe yawezekana, basi tuwaige Indonesia, wakuu kujitegemea hasa kwenye rasilimali zetu ni muhimu kuliko WaTZ..
 
Mkuu usiwe muongo. Zambia migodi yake ina dhahabu
Nyie mnaongelea vitu viwili tofauti ktk uchenjuaji. Ule mchanga wenye mabaki ya dhahabu, silver and copper unaweza kuchenjuliwa kwa njia mbili roasting au Oxidation ambapo process hizo ndio lazima uwe na technology ya kisasa Roasting unachoma mchanga kati ya centigrade 750-1200 hivyo inahitaji uwe na mtambo huo na unatumia umeme mwingi sana.
 
Hiyo Ndola Mine wanafanya uchimbaji wa nini?

Nimekupa mfano ambao hata hapa Tanzania upo!!! Hapa kuna migodi kv Mara na mingineyo ambayo dhahabu inakuwa haipo embedded na madini mengine! Hawa hawana haja ya kusafirisha mchanga kwa sababu teknolojia hata ya hapa inaruhusu!!!

Hao unaowatolea mifano ni wazalishaji wa copper ambayo kwa kiasi kikubwa haipo embedded na madini mengine na ndio maana huwa wanamaliza kila kitu wenyewe kama wanavyofanya wachimbaji wengine wa dhahabu hapa Tanzania!!!

Issue ya Bulyanhulu na Buzwagi ni tofauti!!

Inawezekana ni kweli ipo cheap technology lakini by the time TMAA wametoa ile ripoti walikuwa sahihi!!! Hata ukiangalia kule Japan, zile copper concentrate zinatoka nchi mbalimbali including USA!! Wote hawa hawawezi kuwa wapumbavu!!!!

Indonesia na wenyewe walikuwa na tatizo kama la kwetu! Mwaka jana au mwakajuzi makampuni yakaungana pamoja na serikali kujenga mtambo wao wenyewe wenye uwezo wa kuchenjua tani 500K kwa mwaka kwa thamani ya USD 1.5 Billion!!

Hao nao tusidhani ni wapumbavu kwamba walikuwa wanapeleka China!!!

Kumbuka capital and operating costs of smelter + its peripherals is determined by its size (its capacity tons of concentrate it treats per year)
 
Nyie mnaongelea vitu viwili tofauti ktk uchenjuaji. Ule mchanga wenye mabaki ya dhahabu, silver and copper unaweza kuchenjuliwa kwa njia mbili roasting au Oxidation ambapo process hizo ndio lazima uwe na technology ya kisasa Roasting unachoma mchanga kati ya centigrade 750-1200 hivyo inahitaji uwe na mtambo huo na unatumia umeme mwingi sana.

Mwingi kiasi gani be specific, by the way unajua kwamba roasting is an exothermic reaction?
 
Nyie mnaongelea vitu viwili tofauti ktk uchenjuaji. Ule mchanga wenye mabaki ya dhahabu, silver and copper unaweza kuchenjuliwa kwa njia mbili roasting au Oxidation ambapo process hizo ndio lazima uwe na technology ya kisasa Roasting unachoma mchanga kati ya centigrade 750-1200 hivyo inahitaji uwe na mtambo huo na unatumia umeme mwingi sana.
Mkuu oxidation nadhani ni kwa mchanga ambao hauna sulfur kama Zambia. Nipo tayari kujifunza
 
Sijaweka smelters zote zenye uwezo zaidi ya 100,000 tons per lakini hata za japani na nchi nyingine pia zipo. Zipo zenye uwezo hadi 500,000 tons per year (Chuquicamata cha chile). Nilitaka tu kuonyesha zenye uwezo chini ya 100,000 tons per year.
upload_2017-3-28_12-13-34.png

Hizo ndizo Gold smelters za Dunia
 
Back
Top Bottom