Ulichoandika kina matundu mengi tu, na inaonesha aina ya imani uliyonayo!
Hebu angalia hapo pekundu ndio utajua! Eti unaiita ni privilege, nakuapia unapaswa kujua kuwa Mungu ndiye anayewapeleka na kuwaponya hao watu, mtu kufanya upuuzi wa kuwatia watu makwazo eti halafu wewe unaiita privilege kuwa nae, kisa analipia ofisi na kucoordinate safari za kwenda huko, kwani amelazimishwa?!
Unalopaswa kujua ni kwamba hata asingekuwepo, Mungu angeinua mtu mwingine wa kufanya hilo, hivyo wakati unamshauri kiroho kama ulivyosema, mwambie asijivishe umungu mtu kisa ana direct access na prophet, maana hiyo siyo guarantee ya kuingia mbinguni, she has to work her way through it all. Kila mtu ataingia mwenyewe kule.
Ona eti unasema kuwa wale wahudumu wa SCOAN, they tell it to your face na Martha ni cha mtoto?! Huoni hata aibu kuyasema haya humu?! Sijui ulilenga kusifia ama kulaani?! unaleta ushabiki kwenye mambo ya kipuuzi, kwani kuwa mhudumu wa TB Joshua ndiyo standard ya jambo jema na baya?! Kama wanafanya kitu cha kibaya kinabaki kuwa kibaya, so hao unaowasema kuwa ni zaidi ya huyu wa huku kwetu, pata nafasi ya kuwashauri pia kuliko kuja kutetea ujinga humu.
Najua wengi wenu katika hatua mlofikia hamjazoea kuambiwa ukweli jinsi ulivyo.
Imeandikwa wanaojikweza watashushwa
!