The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 21,185
- 48,959
Ningekuwa na majibu ningeuliza? Cookies za biskuti na keki nani hazijui? Istoshe hii ni forum ya tech na gadget. Gadget na cookies wapi na wapi kaka!
1. Cookies (vibiskuti) - ni vifaili vidogo ambavyo hutumwa na tovuti unayoitembelea kwa wakati huo kwenda kwenye kifaa unachotumia, kama ni simu ya mkononi, tabiti, au kompyuta yako kupitia browser yakoumuhimu wake...vinasaidia kukusanya taarifa na kuwasaidia wenye tovuti kujua ni watumiaji wangapi wametembelea tovuti yao, pia inaweza saidia kujua ni vifaa vipi hutumika zaidi kufungua mtandao wao,
2. Cache: hii ni kumbukumbu ambayo huwekwa na browser yako kwa kila tovuti unayotembelea, ili wakati mwingine utakapofungua tovuti hiyo au ukurasa huo iwe rahisi kufungua (itachukua muda mchache kufungua cached page kuliko ukurasa mpya)hasara ya cache: kama pc yako ina nafasi ndogo ya kuhifadhi mafaili , cache inawea kuchukua nafasi kubwa sana na itabidi ku clear mara kwa mara.
3. cookies na cache zinaweza kuwa disabled kama hupendi kufuatiliwa habari zako,
Kwa hisani ya UncleUber
Pitia huu uzi pia
cookies na caches ni vitu gani kwny haya mambo ya internet