Colorism ni saratani isiyotambulika rasmi lakini imeenea sana kwenye jamii

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,242
113,627
For the benefit of all those in Rio Linda 🤣, let’s begin by defining what colorism is;

differential treatment based on skin color, especially favoritism toward those with a lighter skin tone and mistreatment or exclusion of those with a darker skin tone, typically among those of the same racial group or ethnicity.

Kimsingi, colorism ni ubaguzi wa ndani kwa ndani. Watu wenye ‘rangi moja’ mnakuwa mnabaguana wenyewe kwa wenyewe kulingana na ukolezo wa rangi nyeusi aliyonayo mtu.

Mifano:

Juzi nimekutana na mdada ambaye nilipotezana naye kwa takriban miaka 5.

Katika maongezi akalalamika kuwa anahangaika kufanya biashara mpaka amekuwa mweusi!

Mwaka jana nilienda Kigamboni kwenye chimbo moja hivi liitwalo The Giant. Kwa sasa halipo tena.

Nimeketi hapo tunasubiri warembo kadhaa waje. Nilikuwa na washikaji wengine wawili.

Warembo wakaja. Mshkaji mmoja akagoma kuongea na mmoja wa wale warembo kisa mrembo alikuwa ‘mweusi’.

Cha ajabu sasa, huyo mshikaji naye ni ‘mweusi’ tii.

Mifano na matukio kama hayo ni mengi sana kwenye jamii.

Aliyetulisha hiyo sumu alituweza sana kwa kweli maana tumeshindwa kabisa kuiondoa kwenye jamii.

Licha ya makelele mengi dhidi ya ubaguzi wa rangi hususan dhidi ya watu weusi, sisi kwa sisi bado tunabaguana kulingana na ukolezo wa rangi ya ngozi aliyonayo mtu.

Inasikitisha na kukatisha kabisa tamaa unapoona jamii inaweka thamani kwenye rangi ya ngozi.

Weusi, kuwa na ngozi nyeusi, hakuna ubaya wowote ule.

Ni ujinga na upumbavu tu kuwaza kuwa kuna ubaya.
 
si tulikubaliana watoto wa kike wanapenda wanaume weusi warefu haya yanatoka wapi tena, na sisi ma light skin acha tupende wanawake weusi tii, hapo hakuna ubaguzi ni kila mtu ashinde mechi zake
 
Kansa hii imeathiri kiasi kikubwa jamii ya watu wa kanda ya Ziwa.
Mwanamke mweupe kwa Wasukuma ni biashara muhimu sana wakati wa kutoza mahari.
Ubaguzi wa rangi hasa upo huko.
 
Colorism ipo sana hata kwa African Americans. Weusi wengi wamebagulia kuliko the lighter skin ones. Uzuri wa AA walio wengi wamegoma kujichubua ngozi kama ilivyo Africa.

Watoto dark skin huwa wanakua wa mwisho kuwa adopted kuliko wengine. This is sad indeed. Nadhani walifanya amendment ya adoption kusiwe na uhuru sana wa kupick and choose.
 
For the benefit of all those in Rio Linda , let’s begin by defining what colorism is;

differential treatment based on skin color, especially favoritism toward those with a lighter skin tone and mistreatment or exclusion of those with a darker skin tone, typically among those of the same racial group or ethnicity.

Kimsingi, colorism ni ubaguzi wa ndani kwa ndani. Watu wenye ‘rangi moja’ mnakuwa mnabaguana wenyewe kwa wenyewe kulingana na ukolezo wa rangi nyeusi aliyonayo mtu.

Mifano:

Juzi nimekutana na mdada ambaye nilipotezana naye kwa takriban miaka 5.

Katika maongezi akalalamika kuwa anahangaika kufanya biashara mpaka amekuwa mweusi!

Mwaka jana nilienda Kigamboni kwenye chimbo moja hivi liitwalo The Giant. Kwa sasa halipo tena.

Nimeketi hapo tunasubiri warembo kadhaa waje. Nilikuwa na washikaji wengine wawili.

Warembo wakaja. Mshkaji mmoja akagoma kuongea na mmoja wa wale warembo kisa mrembo alikuwa ‘mweusi’.

Cha ajabu sasa, huyo mshikaji naye ni ‘mweusi’ tii.

Mifano na matukio kama hayo ni mengi sana kwenye jamii.

Aliyetulisha hiyo sumu alituweza sana kwa kweli maana tumeshindwa kabisa kuiondoa kwenye jamii.

Licha ya makelele mengi dhidi ya ubaguzi wa rangi hususan dhidi ya watu weusi, sisi kwa sisi bado tunabaguana kulingana na ukolezo wa rangi ya ngozi aliyonayo mtu.

Inasikitisha na kukatisha kabisa tamaa unapoona jamii inaweka thamani kwenye rangi ya ngozi.

Weusi, kuwa na ngozi nyeusi, hakuna ubaya wowote ule.

Ni ujinga na upumbavu tu kuwaza kuwa kuna ubaya.
Demu hata awe mweusi tii utamu wake ni balaa so weusi sio hoja kbs
 
Back
Top Bottom