Kando na pipi za pamba, unajua ni bidhaa gani nyingine zinazoweza kusababisha saratani?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138

Kando na pipi za pamba, unajua ni bidhaa gani nyingine zinazoweza kusababisha saratani?​

ds

Maelezo ya picha,
Uuzaji wa pipi za pamba umepigwa marufuku katika jimbo moja huko India

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na Idara ya Usalama wa Chakula katika jimbo la Tamil Nadu nchini India, umebaini kuwepo kwa kemikali za Rhodamine B katika pipi za pamba ambazo ni kipenzi cha watoto.
Kwa hivyo pipi za pamba za rangi ya waridi na nyekundu, mojawapo ya peremende zinazopendwa zaidi na watoto, sasa zimepigwa marufuku na serikali ya Tamil Nadu.
Ni vyakula gani vingine vyenye kemikali hizo? Ni ipi athari zake kiafya?

Kemikali za Rhodamine B ni nini?​

i

Maelezo ya picha,
Rhodamine B inapatikana katika pipi ya pamba

Rhodamine B inaundwa kwa kemikali ya rangi. Inaweza kutoa rangi nyekundu au pinki. Rangi hii ya kemikali hutumiwa sana katika nguo, karatasi na ngozi.
Ni kwa sababu inaweza kuingiliana na maji na bei yake ni ya chini. Kemikali hizo haziozi zinastahimili joto na mwanga.
Tume ya Usalama wa Chakula na Udhibiti ya Tamil Nadu imeweka miongozo ambayo viungo vinaweza kutumika na kwa kiasi gani na imepiga marufuku matumizi ya Rhodamine B katika bidhaa za chakula kutokana na madhara yake.
Wale wanaotumia rhodamine B katika utayarishaji, usindikaji na usambazaji wa bidhaa za chakula wataadhibiwa chini ya Sheria ya Usalama wa Chakula na Udhibiti ya (2006).

Ni vyakula gani vina Rhodamine B?​

dfc

Maelezo ya picha,
Rhodamine B ni marufuku kwa matumizi ya bidhaa za chakula

Sathish Kumar, Afisa katika Idara ya Usalama wa Chakula, Wilaya ya Chennai anasema, "Rhodamine B, inayopatikana kwenye pipi ya pamba, pia hupatikana katika mtindi mzito wa rangi, ubuyu, figili nyekundu."
"Kuna rangi ambazo zinaruhusiwa katika bidhaa za chakula. Kwa mfano, Allura Red kwa rangi nyekundu, Apple Green kwa rangi ya kijani. Pia zinapaswa kuwepo katika bidhaa za chakula kwa kiasi fulani tu. Lakini hii rhodamine B hairuhusiwi kuwa katika bidhaa yoyote ya chakula hata kwa kiwango kidogo," alisisitiza.
Sio bidhaa zote za chakula zilizo na rhodamine B zinaweza kugunduliwa mara moja na mtumiaji. Hata hivyo, kuna baadhi ya vipimo unaweza kufanya nyumbani ili kugundua uwepo wa Rhodamine B katika baadhi ya vyakula.
Rhodamine B huchanganyika kwa urahisi katika maji na mafuta. Mamlaka ya Usalama wa Chakula na Udhibiti wa Ubora imetoa miongozo ya kugundua uwepo wa Rhodamine B yenye sifa hii.

Jinsi ya kuigundua​

sx

Maelezo ya picha,
Rhodamine B huchanganywa katika maziwa mazito ambayo ni maarufu kwa watu

Wateja hawawezi kuwa na uhakika kama pipi ya pamba ina Rhodamine B au la. Uwepo wa rhodamine B unaweza kuthibitishwa tu baada ya sampuli kupimwa katika maabara ya usalama wa chakula.
Idara ya Usalama wa Chakula hivi majuzi imetangaza sampuli zilizokusanywa Tamil Nadu kuwa si salama baada tu ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara.
"Mtu hawezi kusema kwa uhakika ikiwa bidhaa ya chakula ina rangi iliyopigwa marufuku au la. Lakini kile ambacho watu wanapaswa kukumbuka ni kwamba ikiwa kuna rangi angavu inayovutia macho yako, iwe ni mboga, matunda, chokoleti, keki ni vyema kuziepuka kwa sababu rangi asilia hazing'ari," anasema Satish Kumar, Afisa Usalama wa Chakula, Wilaya ya Chennai.
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa rhodamine inaweza kusababisha magonjwa ya ngozi, athari za kupumua, uharibifu wa ini na figo. Kwa hiyo, rhodamine B ni marufuku katika bidhaa za chakula kwa kuwa haifai kwa matumizi ya binadamu.

Rhodamine B inasababisha saratani?​

dsc

Mkuu wa Idara ya Famasia wa Hospitali ya Serikali ya Stanley huko Chennai alisema utumiaji wa Rhodamine B utasababisha uharibifu wa ini.
“Matumizi ya mara kwa mara ya rhodamine B yanaweza pia kusababisha saratani ya ini. Uhusiano kati ya rhodamine B na uharibifu wa ini umethibitishwa katika tafiti nyingi."
Ulaji wa rhodamine B huathiri mfumo wa neva pamoja na ini. Kutokana na hili, kutakuwa na kizuizi katika kazi za ubongo. Dk Chandrasekhar anataja kuwa neva na uharibifu wa uti wa mgongo pia utatokea.
Kwa ujumla, ulaji wa kemikali husababisha madhara makubwa. Haijalishi kemikali hii ni nini, itakuwa na madhara zaidi ikiwa inatumiwa kwa kuendelea.
“Unaweza kusababisha sumu kali mwilini. Hii inaweza kutokea kulingana na kiasi gani cha rhodamine kinachanganywa kwenye chakula na kulingana na mfumo wa kinga wa kila mtu," Dk. Chandrasekhar alieleza alipokuwa akizungumza na BBC.
 
asante kwa mada nzuri mkuu, hivi saratani ukiacha hivyo vitu gani vingine vinaweza kusabaisha, na ni jinsi gani unaweza kujikinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom