Coding DEEPSEEK ni bora kuliko CHATGPT!

Mkuu natamani sana kujua coding naomba nisaidie wewe ulianzaje napenda computer science lakini siyo ya kwenda shule. Ni learn alone

Practice man Practice. Sema nini man, binafsi nilikaa class nikafundishwa ila kwa sasa hivi ni rahis sana kujifunza coding. Unaweza ukajifunza coding kwa kuchagua unataka udili na app/web. Binafsi nilikuwa najua sana PHP lakini nilitamani sana nijifunze android development, nimejikuta nimejua bila ata kufundishwa kutoka na AI.

Jifunze kuwa assembled developer, ukitaka ujue kuchapa code itachukuwa muda sana, jifunze kutengeneza logic ya kutengeneza kitu kwa kuandika, yaan kwa lugha ya AI kwa sasa ningekushauri ujue kuandika PROMPT inatosha sana kufanya unachotaka especially kwenye coding/design.

Nikupe mfano niliona youtube, jamaa hajui chochote kuhusu coding ila anatamani kumiliki app ya kutoa taarifa ya chakula kama kina calories ngapi ili mtu awe ana balance diet yake wale wanaotaka kupunguza uzito. Alichofanya akachek playstore kama kuna app kama hiyo ili a clone kwa kutumia AI.

Kuna website inaite MOBBIN ina app nyingi sana unaweza ukatafuta idea ya app unayotaka then inakupa UX/UI . Ukishapata UX unaingiza kwenye AI inachapa code kama UI zilivyo. kwaiyo usichome sana mafuta kujifunza kuchapa code , jifunze kutengeneza logic ili Ai ikupe unachotaka kwa 10mins.


Unaweza jifunza kwa kuchek youtube video kile unachotaka kujua ni AI gani inaweza kunisaidia UX/UI, na AI gani inaweza kuchapa code za UI/UX pamoja na database. Uchawi ni PROMPT kwasasa na LOGIC. Ukijua namna ya kuiuliza AI kwa uzuri ume win nowadays...


Last word ingia YOUTUBE KWANZA ULE MCHIMBO UJUE NAMBA YA KUDILI NA AI THEN INGIA FIELD KAMA ENGINEER.
 

 
GROK 3 ni balaa jingine ambayo limeibuka kwa haraka zaidi kutoka kwenye maboresho ya GROK 2. Nimejaribu kutengeneza APP , nimetumia saa 5 kukamilisha kila kitu baada ya AI kuelewa nini nataka kukamilisha . Nilianza kwa kiapa idea na nilishare idea kwa AI zingine kama CHATGPT na DEEKSEEK, nilijikuta nimevutiwa sana na maelezo ya GROK 3 ingawa yalikuwa yanashabiana na CHATGPT ila GROK 3 alitoa UX/UI kali sana kwenye maelezo na akatoa suggestions za features zingine ambazo zitaleta manufaa, nikajikuta nimenasa kwa GROK 3.

Ingawa CHATGPT kwenye kuchora UX/UI ni balaa lingine ikilinganisha na GROK 3, sometimes nachukua maelezo GROK 3 na paste CHATGPT kuona UI/UX ili kujionea UX kulingana na maelezo ya GROK 3. Nilichovutiwa zaidi kwenye GROK 3 ni namna anavyochapa code ni tofaut na CHATGPT, GROK 3 anaanza na app structure, database structure then anaanza kuchapa code kwa mtiririko wa app structure had mwisho na akimaliza anakuuliza swali kama unataka features zingine ambazo anakulistia pale , ukisema ndio anabadilisha app structure, database na kuanzan kuchapa code na anakumbuka maelezo yako ya mwanzo ata mchat conversation nyingi vipi , uwa ana kukumbusha alafu anaendelea na kitu kingine kama unataka.

Anakupa gharama ya project nzima na namna ya kupunguza gharama kwa MVP, kitu ambacho CHATGPT hafanyi ad umuulize. Kitu ambacho anazingua server zake zinazidiwa sana ikianza kuzingua ndio bas tena labda ufungue new conservation, nikajua ni kwangu kwasababu anatumia free nilijaribu kupaste ile server error twitter nakaona wana kibao nao wanalalamika ad wale waliolipia.

Nilitaka niwaulize wadau kama kuna mtu alisha experience server reconnect ya kwenye GROK 3. Kinachonishangaza GROK 3 ya ndani X ni tofauti na grok.com, nikajua nitakuta history kwenye grok.com . Nilitaka nilipie nimalize project sasa nimepangawa kinooma. Nimepakiza feature kama tu ambazo GROK alishauri niliona zina manufaa ambazo ni search_filter na notifications kwa admin.

Nimejaribu sana ku reconnect lakini inagoma inaniambia nifungue new conversation, nimejaribu kufungua new conversation GROK hakumbuki tena kile ambacho tume left kwenye old coversation. Nimejaribu kumkumbusha mwana hakumbuki tena. Hapa nimepangawa sijui nafanyaje.

Mwenye solutions naomba waseee.
 


Chatgpt kwenye ubora wake . UX/UI ni balaa
 
Unataka ku generate different result from the same code, jaribu grok, grok ni 🔥
 
Kama wewe ni side hustle unaweza ukajichomeka kwenye Music AI kwa kutengeza nyimbo(mp3) na kupakia spotify ukapige mpunga, leo nilijaribu kugenerate nyimbo(mp3) mazee AI ni balaa sana nyimbo kali balaa ata nataka kushawishika nilipie ili nipate license ya commercial use na ku upload spotify . Kitu kimenishangaza sana leo , kama una mtaji wa $30/$100 unaweza ukaanza hii side hustle ya ku generate songs kwa AI na kwenda kuuza spotify. Na unaweza uka generate album kabisa bro ukaenda kupakia spotify ukala mpunga kule.

Nyimbo hizi :
1. Love Me or Leave Me Listen and Download | AI Music Generator
2. Love Me or Leave Me Listen and Download | AI Music Generator
3. https://suno.com/s/MGY5VrgqTTYhnHPb
 
Wabongo bbwana!! hapo unakuta umeandika code ya web au app moja tu, au mara moja tu tayari umeshatoa maoni. Kuweni watumiaji wa muda mrefu wa hizi products za mitandaoni, ili muweze kutoa accurate reviews.
 
Jaribu na hii AI mpya mjini:

 
Kuna kitu inatwa Grok Ai , mpaka cyber security si coding tu
Japokuwa sas ahiv wameondoa free ila malipo kidogo, so efficent
 
Kuna kitu inatwa Grok Ai , mpaka cyber security si coding tu
Japokuwa sas ahiv wameondoa free ila malipo kidogo, so efficent
Namtumia pia kwenye coding. Anapiga kiswahili kama mzaramo. Manus AI inafanya utafiti then anatengeneza backend na frontend. Naye ni balaaa
 
No one will beat Google. Agentic AI ilizokuja nazo ni robustly catastrophic! Includi tons of development options.
 
No one will beat Google. Agentic AI ilizokuja nazo ni robustly catastrophic! Includi tons of development options.
Google walionekana kuachwa nyuma, but wamekuja ku rise gafla kwenye game, no moja ya top services sasa

Apple ndio wameachwa nyuma kabisaa
 
No one will beat Google. Agentic AI ilizokuja nazo ni robustly catastrophic! Includi tons of development options.
Bro uko vzr kutumia tensorFlow nataka unipe shule nataka nifanye AI trading system kwa python
 
Google walionekana kuachwa nyuma, but wamekuja ku rise gafla kwenye game, no moja ya top services sasa

Apple ndio wameachwa nyuma kabisaa
Google kwenye upande upi budda. Inayokimbiza kwa sasa ni Veo 3. Gemini bado sana kwa chatgpt/grok. Kwenye kuchora app UI design ni chatGPT ni bora zaidi.
 
Iyo solution kufix ni grok sio wewe coz grok itakua ana lack memory
ChatGPT iko na memory nzur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…