Nadhani mjadala hapa ni namna gani Beach zetu zingeweza kufanywa bora zaidi kwa watu kupumzika na kupunga upepo kuliko kuchoka kwa wanaopunga upepo beach. Nadhani tunawakosea haki watu kuwaambia wamechoka katika hoja hii, kwani kutengeneza beach bora hakutaondoa uchovu wa hawa jamaa, let's not mix the two scenarios.
Mpiga filimbi,shida ni kitu kimbaya sana na madhara yake kisaikolojia pia hayasemeki. Hali ya wananchi kiuchumi ndicho ninachozungumzia pale ninapomention kuchoka kwa wananchi,this time with reference to the picture. Kwasababu kabla mwananchi hajafikiria kwenda beach kupumzika,matatizo na shida wanavyokumbana navyo,mara nyingi hata uwezo wa kupata milo at least miwili kwa siku ni tabu.
Sisi ni wanadamu,na tuna adapt kutokana na mazingira na kama umeshawahi kusafiri mara kwa mara utajua hilo kama wewe ni mtu wa kujifunza.
Kimsingi, kama wananchi hao wangekuwa na hali nzuri ya kiuchumi,basi na ufahamu wao ungekuwa wa tofauti kidogo,tatizo la ku adapt hapa linakuja kwani wengi wamezoea shida na kwasababu upeo wao uko limited,basi ni vigumu kwa wao kutaka mabadiliko.
Ili uweze kufanya biashara ambayo ni sustainable,ni lazima kuwe na consumers,kwetu hapo sisi kwasababu ya umasikini,watu wa biashara huwa wanaprefer watalii foreigners zaidi kwasababu ya foreign currency na uwezo wa watalii hao kuspend.....Na wasipokuja watalii hapo uchumi "Unayumba" Kwani hata Mh Rais atapiga kelele.. Kutokana na hayo,ni vigumu sana kupata viongozi watakaokuwa na uzalendo enough kuwasaidia wananchi hao waliochoka bila ya kuwa na maslahi binafsi.
Mwanakijiji hapo Detroti eneo la Highland park ni mfano halisi wa kile kinachoendelea hapo bongo na kwenye nchi za Africa kwa ujumla. Eneo hilo ambalo community ni predominantly black,wanajamii hao walipoteza kazi zao na hivyo huduma za kijamii zikaanza kupungua,downsizing ikaanza na layoffs kwa mwendo wa mbele. Kuna documentary inayoitwa The water front inayohusiana na tukio hilo,kwani idara ya maji iliathirika na wananchi hao kuanziwa kukatiwa maji mara baada ya kushindwa kullipa bills za maji zilifikia maelfu kwa maelfu kwa mwezi,kwa kawaida hapa USA especially hapa nilipo bills hizo hurange from 20 bucks to 50.
Detroit tunajua imezungukwa na maji,lakini kabla maji hayo hayajatumika ni lazima yawe trated kwenye plant,na hivyo basi maji hayo yalibinafshwa na hivyo kupeleka mgogoro kwenye jamii hiyo,wanajamii hao walikataa ubinafsihswaji wa maji hayo na city council ikabakia na responsibilit hiyo,haijajulikana ni kwanini bills hizo zilipanda lakini habari ndiyo hiyo,kuwa ukibinafsisha watu wanataka kumake profits sometimes beyond means...Wananchi hao walikuja juu,ila hapo ndipo kwenye a thin line between socialism,capitalism and realism....Ukweli ni kwamba socialism inaprevail ila wanazuoni wanataka kuimodify kwani hilo neno ndio tabu, lakini ukweli ni kwamba socialism iko well practiced hapa Marekani. Na mtu asiwadanganye wananchi,serikali bado ina jukumu la kuwaletea wananchi maendeleo in any means necessary na si kuwadanganya kuwa sasa ni capitalism na hivyo kivyao vyao....Na kwasababu matatizo yanayowakabili wananchi ni ya kimsingi kama chakula nk,ni vigumu kufikia levele ya kudai beach nzuri ya kupumzikia, at least huwa wanashiba pilau kubwa wakati wa sikukuu na hivyo kupata fursa ya kupunga upepo.
Kina Kibunango wanadai huko Zenji beach ni all the time,nadhani niliandika something similar to that pale niliposema wananchi hao hawajui matumizi yake na hivyo kuwa shida kwa wao kudai patengenezwe.
Wenzetu wa magharibi walipoanza kusafiri walileta maendeleo kwao,tena watu huwa hata hatujiulizi,walichukua si tu rasilimali,bali pia "Rasilimaliwatu" Sisi ndio tunaondosha kwetu,hapo ndio unapojua kweli maana halisi ya uzalendo,wananchi walio wengi hawafahamu,hawajui correlation ya kile wanachojua viongozi wao vs kile wanachotakiwa kuwafanyia wananchi kwasababu wananchi wenyewe hawana idea ya nini wanataka kifanyike..Na kisaikolojia viongozi ndio wanagandamizia kabisa kwenye fikra za wadanganyika hao kuwa SISI NI MASIKINI, bakuli every now and then whenever wanaposafiri,hakuna kuiga vitendo na mifano ya maendeleo ya kuwanufaisha wananchi,ni bakuli tuu.
Unaona serikali ya Obama inataka sheria ipitishwe kuhusu ujenzi wa nyumba ili zifikie viwango vilivyowekwa ili ziwe more energy efficient na hivyo kupunguza matumizi/gharama za heat,air condition nk.
Serikali ni lazima ibuni mipango ambayo itawasaidia wananchi hata kama wananchi hao hawajui ama hawana habari na manufaa hayo kwani manufaa hayo yatawageuza kisaikolojia na kuwafanya wawe wa wa kupenda maendeleo....Wananchi wakiwezeshwa uvhumi ukiwa mzuri everything else falls on its part.
Mwanakijiji bado tunasubiri makala hiyo na kama imeshatoka tufahamishane.
Mpiga filimbi,huwezi kukwepa kuzungumzia hali halisi ya wananchi hao na kuzungumzia beach peke yake,kuna correlation bila shaka.