Clouds mnaudharaulisha Wimbo wa Taifa

Ndio na wewe, kwani wewe sio mtanzania nini? Umewahi kuona wimbo wa Kenya, Uganda, hata hao Rwanda mnaoiga filosofi yao inapigwa hovyo hovyo?
Acha jazba. Tuwekee hicho kifungu cha sheria mimi nitakuwa wa kwanza kuwaandama CMG waache kupiga wimbo wa taifa.
 
Haupigwi hovyo hovyo. Unapigwa saa moja kamili kabla ya taarifa ya habari kwa kweli unajenga uzalendo sana hio mida hua niko na mtoto wangu alikua hajui kuiimba lakini sasa hivi anaujua vizuri. Mleta uzi jaribu kwa angle nyingine hii hapana.
 
Wana liona katika positive way
Duh, hatari sana. Juzi Mimi nilishtuka ghafla kuna nini tena, huu wimbo na maudhui yake sijaelewa? Mwisho na sikia shishi baebi!! Duh, nulifedheheka sana. Au kwakuwa waliitwa jukwaani na Mh Rais basi washajiona ndio wanaofuatia baada ya Fulani au?
 
Ruge aliomba kufanya hivo akaruhusiwa
Sababu za kutaka wimbo wa taifa upigwe
1.kuimarisha uzalendo
2.watanzania tuujue
Na unapigwa weekdays saa moja Kamili
Binafsi sioni tatizo
 
Wamevunja sheria? Mbona hujibu? Kuna sheria inasema wimbo huo upigwe kwenye tukio fulani tu?
Wewe hukwenda shule....

Au hata TV hutizami....

Mashuleni wimbo wa taifa huimbwa siku maalumu...tena bendera inapokua inapandishwa..

Unataka nini tena.
 
Ruge ndo aliasisi mpango wa kupiga wimbo wa Taifa saa Moja kamili. Hii kitu inanikera sana.
Clouds acheni kupiga wimbo huu, wimbo huu Si kila radio Au tv inaweza piga tu bila sababu za msingi Na pasipo kuwepo Na special event. Wimbo huu bwana ruge uheshimu, hujautendea haki; hata kama TBC Taifa Radio inaupiga ina haki ya kufanya hivyo kwasababu hiyo ni radio ya Taifa.
Sasa Ruge kama kweli wewe ni mzalendo na unaipenda nchi yako Na kuheshimu wimbo wa Taifa, Nakushauri acha kupiga wimbo wa Taifa mara moja ila napendekeza upige wimbo "Tanzania nakupenda kwa moyo wote, Kila nilalapo nakuota wewe"'Nakuhakikishia Clouds mtaongeza wasikilizaji na matangazo ya biashara kwani wimbo huu ndo wa kizalendo zaidi kuliko hata wimbo wa Taifa (ambao tuliuiga tu kwa wenzetu japo inabidi tu uheshimu kwasababu upo kisheria lakini hautii hamasa ya uzalendo kama huo nilioutaja)
 
Mi naona kusikiliza wimbo wa taifa siyo mbaya ila tatizo muda unao pigwa bora upigwe saa 12kamili asubuhi
 
Ruge aliomba kufanya hivo akaruhusiwa
Sababu za kutaka wimbo wa taifa upigwe
1.kuimarisha uzalendo
2.watanzania tuujue
Na unapigwa weekdays saa moja Kamili
Binafsi sioni tatizo
Mimi sii kichaa kuanzisha uzi huu...

Leo kilichofanyika ni dharau kubwa kwa Wimbo wa TAIFA..
 
Back
Top Bottom