Ruge ndo aliasisi mpango wa kupiga wimbo wa Taifa saa Moja kamili. Hii kitu inanikera sana.
Clouds acheni kupiga wimbo huu, wimbo huu Si kila radio Au tv inaweza piga tu bila sababu za msingi Na pasipo kuwepo Na special event. Wimbo huu bwana ruge uheshimu, hujautendea haki; hata kama TBC Taifa Radio inaupiga ina haki ya kufanya hivyo kwasababu hiyo ni radio ya Taifa.
Sasa Ruge kama kweli wewe ni mzalendo na unaipenda nchi yako Na kuheshimu wimbo wa Taifa, Nakushauri acha kupiga wimbo wa Taifa mara moja ila napendekeza upige wimbo "Tanzania nakupenda kwa moyo wote, Kila nilalapo nakuota wewe"'Nakuhakikishia Clouds mtaongeza wasikilizaji na matangazo ya biashara kwani wimbo huu ndo wa kizalendo zaidi kuliko hata wimbo wa Taifa (ambao tuliuiga tu kwa wenzetu japo inabidi tu uheshimu kwasababu upo kisheria lakini hautii hamasa ya uzalendo kama huo nilioutaja)