Clouds Media wamwandalia Kikwete Birthday 2010?

Clouds Media wamwandalia Kikwete Birthday 2010?

- I see ninaijua Clouds toka ikiwa ya Justin kaka yake Joe alipotoka Holland kusoma long time ago na Joe alipotaka kutengeneza Album ya kwanza inayoitwa "Hoya Msella" in 1992 I worked with him in New York na DC kwa hiyo haya sibahatishi, na hawa vijana wa Bongo-Flev ndio wapiga kura wenyewe, sasa nashangaa strategy ya kuwatukana ni dalili za mfa maji au kukata tamaa, again ninasema hivi kama kweli Wapinzani wako serious waungane sasa!,

- Mfano mzuri ni visiwani, wananchi wote wanajua upinzani ni CUF tu ndio maana wana nguvu za ajabu na sasa wataingia kwenye serikali ya pamoja! Bara tutaendelea kurushiana maneno yasiyokuwa na faida kwa taifa mpaka mwisho wa dunia ushindi hakuna!

Es!
Plainly, wewe kwanza hutakuwapo siku ya kupiga kura. Bahati mbaya zaidi hatuna online voting. Na ninahisi hata hiyo shahada huna. Baada ya big fail kule Dom upo hapa kutuchanganya tu na habari za kuungana wapinzani.
Mimi nilikuuliza swali kwamba kama issue ya wapinzani kuungana ni lazima, mbona kwenye kura za maoni kila mtu alivuna kivyake na hamkuungana?
Tutashinda banaaaaaaa
 
- Sidhani kama kuna tatizo, FOX NEWS kuwa Conservative na MPR kuwa Liberally ni uamuzi wa msikilizaji, Clouds wako free kuamua what they want to be, msikilizaji ndiye muamuzi maana you know what you are getting yr self into unapo-watune in!

Es!

Kweli nimebadili mawazo, I once thought that you are undisputable Great Thinker...
 
ThE man and his DREAM, tizama alikoanzia mpaka alipofikia sasa saafi sana Joe ni mfano wa kuigwa kwamba hard work siku zote hulipa, and then wivu na majungu maana yake the hard work is paying!

Tizama Joe na Clouds walikotokea, mpaka kufikia sasa ni mfano wa kuigwa sana na wapenda maendeleo wote Duniani kwamba Hard Work hulipa!

20.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Group,Bw.Joseph Kussaga usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya taasisi ya WAMA,jijini Dar.
 
Plainly, wewe kwanza hutakuwapo siku ya kupiga kura. Bahati mbaya zaidi hatuna online voting. Na ninahisi hata hiyo shahada huna. Baada ya big fail kule Dom upo hapa kutuchanganya tu na habari za kuungana wapinzani.
Mimi nilikuuliza swali kwamba kama issue ya wapinzani kuungana ni lazima, mbona kwenye kura za maoni kila mtu alivuna kivyake na hamkuungana?
Tutashinda banaaaaaaa

- Lo! masikini ya Mungu, huruma sana!, mimi sigombei nafasi yoyote bro naona unahangaika sana pole sana!

Es!
 
Hawana loloye jipya zaidi ya kujipendekeza!

Hivi tatizo nini hasa! kama Clouds wamemfanyia party JK inahusu nini? maana kila chombo cha habari kina mwelekeo wake ambao umewekwa na wamiliki wake. Joseph Kusaga kweli kaanzia U-DJ na sasa yuko juu katika level zetu za Bongo anepinga hilo ni kichaa.
Lakini pia anawatu ambao kwa namna moja au nyingine wame-play part yeye kufika hapo-sina maana kwa kumbeba au kumjaza mapesa lakini hata kwa kumshauri na kumpa mbinu mbalimbali za kutumia, nani anawajua wote.
Pia yeye na vyombo vyake nya habari radio na tv wana dira yao na nahusiano na watu pia serikali na wana uhuru wa kuamua kufanya chochote wanaona ni halali kwao.
HIVI leo wangemfanyia Wilbrod Slaa birthday part ungesema wanajipendekeza??????? hivi watu wengine mnataka kila mtu afuate utashi wenu mnavyotaka au mwelekeo wenu mnaotaka. Tuko huru na kila mtu na kila chombo kina uhuru wake tuache kusakama watu sababu hawako upande wenu amasivyo tutasema ni wivu
 
Siyo birthday, wanamuaga JK kumpisha Dr. Slaa kuwa rais wetu

Acha kupotosha, nyie ndo mnaliaga matokeo yanapotangazwa, na kuishia kusema ooooh tumeibiwa kura, wakati sivyo.
 
Hivi tatizo nini hasa! kama Clouds wamemfanyia party JK inahusu nini? maana kila chombo cha habari kina mwelekeo wake ambao umewekwa na wamiliki wake. Joseph Kusaga kweli kaanzia U-DJ na sasa yuko juu katika level zetu za Bongo anepinga hilo ni kichaa.
Lakini pia anawatu ambao kwa namna moja au nyingine wame-play part yeye kufika hapo-sina maana kwa kumbeba au kumjaza mapesa lakini hata kwa kumshauri na kumpa mbinu mbalimbali za kutumia, nani anawajua wote.
Pia yeye na vyombo vyake nya habari radio na tv wana dira yao na nahusiano na watu pia serikali na wana uhuru wa kuamua kufanya chochote wanaona ni halali kwao.
HIVI leo wangemfanyia Wilbrod Slaa birthday part ungesema wanajipendekeza??????? hivi watu wengine mnataka kila mtu afuate utashi wenu mnavyotaka au mwelekeo wenu mnaotaka. Tuko huru na kila mtu na kila chombo kina uhuru wake tuache kusakama watu sababu hawako upande wenu amasivyo tutasema ni wivu

Unajua raisi ni wa watu wote na sasa anapooonyesha upendeleo kwa media moja na kuziacha nyingine analeta picha gani? Hebu imagine watu kama magic FM, Radio One, Free Africa , TBC watajisikiaje? Bora hata angealika wawakilishi wa kila Radio kuliko kujaza hao jamaa hapo kama kwamba wao ndio wana hisa sana na serikali. Ndio unaweza sema ni private party lakini ilifanyika Ikulu (Wama iko Ikulu) inatakiwa kuwa rational kwenye kualika watu. Ndio maana hawa jamaa wanalobby sana tenda za entertainment kwa sababu wana access na raisi. Unakumbuka issue ya Mr II?
 
Hivi tatizo nini hasa! kama Clouds wamemfanyia party JK inahusu nini? maana kila chombo cha habari kina mwelekeo wake ambao umewekwa na wamiliki wake. Joseph Kusaga kweli kaanzia U-DJ na sasa yuko juu katika level zetu za Bongo anepinga hilo ni kichaa.
Lakini pia anawatu ambao kwa namna moja au nyingine wame-play part yeye kufika hapo-sina maana kwa kumbeba au kumjaza mapesa lakini hata kwa kumshauri na kumpa mbinu mbalimbali za kutumia, nani anawajua wote.
Pia yeye na vyombo vyake nya habari radio na tv wana dira yao na nahusiano na watu pia serikali na wana uhuru wa kuamua kufanya chochote wanaona ni halali kwao.
HIVI leo wangemfanyia Wilbrod Slaa birthday part ungesema wanajipendekeza??????? hivi watu wengine mnataka kila mtu afuate utashi wenu mnavyotaka au mwelekeo wenu mnaotaka. Tuko huru na kila mtu na kila chombo kina uhuru wake tuache kusakama watu sababu hawako upande wenu amasivyo tutasema ni wivu

- Ahsante sana mkuu, unajua ningeelewa kama ningesikia kwamba Rais amealikwa na vituo vingine vya TV na Radio akakataa hapo kweli huu mualiko ungekua na utata, lakini kwenye nchi huru Clouds wamemualika Ris kakubali kwenda si na wengine wamualike tuone kama atakataa! Mkuu Boma tupo pamoja sana hapa!

Respect.

FMEs!
 
ThE man and his DREAM, tizama alikoanzia mpaka alipofikia sasa saafi sana Joe ni mfano wa kuigwa kwamba hard work siku zote hulipa, and then wivu na majungu maana yake the hard work is paying!

Tizama Joe na Clouds walikotokea, mpaka kufikia sasa ni mfano wa kuigwa sana na wapenda maendeleo wote Duniani kwamba Hard Work hulipa!

20.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Group,Bw.Joseph Kussaga usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya taasisi ya WAMA,jijini Dar.

Kweli Ikulu ingehamia kule nyumbani, lol.
 
- Ahsante sana mkuu, unajua ningeelewa kama ningesikia kwamba Rais amealikwa na vituo vingine vya TV na Radio akakataa hapo kweli huu mualiko ungekua na utata, lakini kwenye nchi huru Clouds wamemualika Ris kakubali kwenda si na wengine wamualike tuone kama atakataa! Mkuu Boma tupo pamoja sana hapa!

Respect.

FMEs!

Tatizo Clouds hawajatuonyesha kwamba wao ni chombo habari huru, wamejionyesha kwamba wanafungamana na CCM na Kikwete. Watu tunaotaka habari kutoka kwa vyombo vya habari visivyofungamana na upande wowote tutaona Clouds ni sawa na chombo cha CCM tu.
 
Hivi tatizo nini hasa! kama Clouds wamemfanyia party JK inahusu nini? maana kila chombo cha habari kina mwelekeo wake ambao umewekwa na wamiliki wake. Joseph Kusaga kweli kaanzia U-DJ na sasa yuko juu katika level zetu za Bongo anepinga hilo ni kichaa.
Lakini pia anawatu ambao kwa namna moja au nyingine wame-play part yeye kufika hapo-sina maana kwa kumbeba au kumjaza mapesa lakini hata kwa kumshauri na kumpa mbinu mbalimbali za kutumia, nani anawajua wote.
Pia yeye na vyombo vyake nya habari radio na tv wana dira yao na nahusiano na watu pia serikali na wana uhuru wa kuamua kufanya chochote wanaona ni halali kwao.
HIVI leo wangemfanyia Wilbrod Slaa birthday part ungesema wanajipendekeza??????? hivi watu wengine mnataka kila mtu afuate utashi wenu mnavyotaka au mwelekeo wenu mnaotaka. Tuko huru na kila mtu na kila chombo kina uhuru wake tuache kusakama watu sababu hawako upande wenu amasivyo tutasema ni wivu

Big respect kwako boma2000, umesema kweli. Idumu radio Clouds FM
 
  • Tatizo Clouds hawajatuonyesha kwamba wao ni chombo habari huru, wamejionyesha kwamba wanafungamana na CCM na Kikwete. Watu tunaotaka habari kutoka kwa vyombo vya habari visivyofungamana na upande wowote tutaona Clouds ni sawa na chombo cha CCM tu.
  • Dr. Willibrord Slaa Ahsanteni CLOUDS FM kwa kunitembelea mmenifanya kusikika zaidi. Napenda kuwaomba Watanzania wote wajitokeze kupiga kura October 31 kwa utulivu na amani.Haitakuwa na maana kuwa na ushindi ilihati wanachi wamepoteza maisha ama kujeruhiwa.Tuwe WATULIVU tukitafakari Tanzania ya Kesho.
 
Clouds nao wamezidi kujipendekeza. Nao hao wanaomuita Dr. amesomea wapi ? Hiyo ni digrii inayosotewa miaka 4 sio hiyo ya kupachikwa tu. Mzee Mandela alipachikwa akaikataa. Thabo Mbeki kadhalika. Huyu wa kwetu anaona amesevu ile mbaya!!!!
 
happy birthday, mr. President!

hafla fupi ya rais kikwete akisherehekea siku yake ya kuzaliwa usiku wa kuamkia leo

friday, october 8, 2010

23.jpg

keki safi kabisa ikimeta meta kabla ya kukatwa.

22.jpg

rais jakaya kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya wama.,kulia kwake ni mama salma kikwete.

21.jpg

rais jakaya kikwete akimlisha keki mkewe mama salma kikwete usiku wa kuamkia leo,mh jk usiku wa kuamkia leo alikuwa anatimiza miaka 60.

20.jpg

rais kikwete akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya clouds media group,bw.joseph kussaga usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya taasisi ya wama,jijini dar.

19.jpg

rais kikwete akisalimiana na mwenyekiti wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,prime time promotions ltd,juhayna ajmi.rais kikwete alipita kila meza kusalimiana na wageni waalikwa waliofikwa kwenye hafla yake fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia leo.

18.jpg

wafungua shampeni wakiwa tayari kufanya vituuuzzz.

17.jpg

rais kikwete na mkewe mama salma kikwete wakitakiana afya njema kwa kucheeers mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo,rais kikwete alikuwa akisherehekea siku yake maalum ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 60.

16.jpg

jk akitoa shukurani kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo na kwa waandaaji pia wa shughuli nzima kwa usiku ule.

15.jpg

rais mstaafu wa awamu ya tatu,mh ally hassan mwinyi akiwa ameongoza na mh pius msekwa wakimpa mkono wa pongezi mh jakaya kikwete kwa kutimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake.

14.jpg

waziri mkuu,mh pinda akimpa mkono wa pongezi rais jakaya kikwete.

13.jpg

mtoto wa rais kikwete,ridhiwani kikwete akimpa zawadi baba yake na pia kumpongeza kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake,kwenye hafla fupi iliofanyika usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya taasisi ya wama na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.

12.jpg

mwenyekiti wa prime time promotions,juhayna ajmi na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya clouds media grpup,joseph kusaga wakimpa mkono wa pongezi rais kikwete pamoja na mkewe mama salma kikwete usiku wa kuamka leo.

11.jpg

mtangazaji mahiri wa clouds fm,eprahim kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya taifa ya morroco rais kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.timu hiyo itacheza na timu ya taifa,taifa stars hapo kesho katika uwanja wa taifa jijini dar.

10.jpg

mke wa rais,mama salma kikwete akimpa zawadi mumewe,mh kikwete.

9.jpg

msanii mahiri wa kughani mashairi mrisho mpoto akitumbuiza kwenye hafla hiyo na wimbo wake w adela uliowachangamsha wageni waalikwa waliofika usiku wa kuamkia leo kwenye hafla hiyo.

8.jpg

bendi kongwe ya muziki wa dansi ya sikinde ilikuwepo kutoa burudani usiku ule kwenye hafla ya rais kikwete.

7.jpg

baaap picha safi kabisa ya ukumbusho.mrisho mpoto akiwa amepozi na waziri mkuu mh pinda mara baada ya kutumbuiza kibao chake cha adela.

6.jpg

jk na wageni waalikwa wakiburudika na makamuzi live ya wana sikinde.

5.jpg

vijana wa mjengoni clouds media group na wenyewe wakiserebuka kwa shangwe kabisa

4.jpg

wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,prof jay pamoja na mwana fa wakizungumza jambo na rais kikwete na pia kumpa pongezi za dhati kabisa kwenye hafla hiyo iliyokuwa ya kuvutia usiku wa kuamkia leo.

2.jpg

jk akizungumza na wanamuziki wa bendi ya sikinde

1.jpg

rais kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wana wa clouds media group.

24.jpg

wageni waalikwa kutoka clouds media group,kulia ni pitter mo,gadna g habash,mmoja wa wa wakurugenzi wa prime time promotions ltd,gofrey mkama,gerald hando pamoja mrope.

Source: Michuzi jr.

inatuhusu nini hii sie jf hapa, vitu vingine ni kuwapa watu umaarufu bure, kama walimuandalia sasa inahu?? Ni chombo binafsi na sie hatuna muda wa kuwajadili hapa, hata siku wakiamua kunya barabarani clouds wote sie pia haituhusu..nadhani haikupaswa kuletwa hapa hii..
 
Back
Top Bottom