Clouds Media wamwandalia Kikwete Birthday 2010?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Happy birthday, Mr. President!

Hafla fupi ya rais kikwete akisherehekea siku yake ya kuzaliwa usiku wa kuamkia leo

Friday, October 8, 2010



23.jpg

Keki safi kabisa ikimeta meta kabla ya kukatwa.

22.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.,kulia kwake ni Mama Salma Kikwete.

21.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamkia leo,Mh Jk usiku wa kuamkia leo alikuwa anatimiza miaka 60.

20.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Group,Bw.Joseph Kussaga usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya taasisi ya WAMA,jijini Dar.

19.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd,Juhayna Ajmi.Rais Kikwete alipita kila meza kusalimiana na wageni waalikwa waliofikwa kwenye hafla yake fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia leo.

18.jpg

Wafungua shampeni wakiwa tayari kufanya vituuuzzz.

17.jpg

Rais Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitakiana afya njema kwa kucheeers mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo,Rais Kikwete alikuwa akisherehekea siku yake maalum ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 60.

16.jpg

JK akitoa shukurani kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo na kwa waandaaji pia wa shughuli nzima kwa usiku ule.

15.jpg


Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh Ally Hassan Mwinyi akiwa ameongoza na Mh Pius Msekwa wakimpa mkono wa pongezi Mh Jakaya Kikwete kwa kutimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake.


14.jpg

Waziri Mkuu,Mh Pinda akimpa mkono wa pongezi Rais Jakaya Kikwete.

13.jpg

Mtoto wa Rais Kikwete,Ridhiwani Kikwete akimpa zawadi baba yake na pia kumpongeza kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake,kwenye hafla fupi iliofanyika usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya taasisi ya WAMA na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.

12.jpg

Mwenyekiti wa Prime Time Promotions,Juhayna Ajmi na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Grpup,Joseph Kusaga wakimpa mkono wa pongezi Rais Kikwete pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamka leo.

11.jpg

Mtangazaji mahiri wa Clouds FM,Eprahim Kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Morroco Rais Kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.Timu hiyo itacheza na timu ya Taifa,Taifa Stars hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar.

10.jpg

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimpa zawadi Mumewe,Mh Kikwete.

9.jpg

Msanii mahiri wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla hiyo na wimbo wake w Adela uliowachangamsha wageni waalikwa waliofika usiku wa kuamkia leo kwenye hafla hiyo.

8.jpg

Bendi Kongwe ya muziki wa dansi ya Sikinde ilikuwepo kutoa burudani usiku ule kwenye hafla ya Rais Kikwete.

7.jpg

Baaap picha safi kabisa ya ukumbusho.Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Waziri Mkuu Mh Pinda mara baada ya kutumbuiza kibao chake cha Adela.

6.jpg

JK na wageni waalikwa wakiburudika na makamuzi live ya wana Sikinde.

5.jpg

Vijana wa Mjengoni Clouds Media Group na wenyewe wakiserebuka kwa shangwe kabisa


4.jpg

Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay pamoja na Mwana FA wakizungumza jambo na Rais Kikwete na pia kumpa pongezi za dhati kabisa kwenye hafla hiyo iliyokuwa ya kuvutia usiku wa kuamkia leo.

2.jpg

JK akizungumza na wanamuziki wa bendi ya Sikinde

1.jpg

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wana wa Clouds Media Group.

24.jpg

Wageni waalikwa kutoka Clouds Media Group,kulia ni Pitter Mo,Gadna G Habash,mmoja wa wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Gofrey Mkama,Gerald Hando pamoja Mrope.

Source: Michuzi Jr.
 
Wadau Mmeiona hii?

12.jpg

Mwenyekiti wa Prime Time Promotions,Juhayna Ajmi na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Grpup,Joseph Kusaga wakimpa mkono wa pongezi Rais Kikwete pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamka leo.

11.jpg

Mtangazaji mahiri wa Clouds FM,Eprahim Kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Morroco Rais Kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.Timu hiyo itacheza na timu ya Taifa,Taifa Stars hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar.

5.jpg

Vijana wa Mjengoni Clouds Media Group na wenyewe wakiserebuka kwa shangwe kabisa

1.jpg

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wana wa Clouds Media Group.

24.jpg

Wageni waalikwa kutoka Clouds Media Group,kulia ni Pitter Mo,Gadna G Habash,mmoja wa wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Gofrey Mkama,Gerald Hando pamoja Mrope.
 
Akiwa amepewa "zawadi" na redet...ahahahahahaaaaa..."happy death day to youuuuuuu"
 
Naona wazee wa kujipendekeza wooooote walikuwepo!!!

Hongera rais JK.
 
Hivi hiyo Dr. ni kweli kuna watu wako serious nayo???????????? Du bongo kweli tambarare!!!!!!!!!
 
Naona wazee wa kujipendekeza wooooote walikuwepo!!!

Hongera rais JK.


Hawa kwa jina jengine ni wafaidika wa food web iliyopo ambayo JK na masahiba zake wanajaribu kui-maintain.

On serious note, ati wanamtambulisha kwenye bango kama 'Dr', bwe he he , these clowns are living in a fat globe of mediocrity and stupidity.
 
kuna ule msemo unaosema ukitaka kujua tabia ya mtu angalia rafiki zake. Ukiangalia wageni waalikwa wa sherehe hii ya aliyekuwa rais wa Tanzania wa awamu ya nne (JK) huwezi kushangaa kwa nini rais yetu ni mtu wa kudanganywa kirais na "wasaidizi wake".
 
Hivi marais wa awamu zilizopita hawakuwahi kuwa na bethidei...?
Tuwekeeni na picha zao..
 
haya ndio mambo ya bongo ndugu zangu, wazee wa kujipendekeza naona waliitumia vizuri hafla hiyo, nasikia kuna mtu amemwambia JK "mzee usijali utashinda kwa 88 percent"
 
Back
Top Bottom