Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 536
Wadau, nimekuwa nikijiuliza mwenendo wa hizi Radio station mbili ambazo huwa nazisikiliza kwa vipindi vyao maalumu. Nimeshituka kumsikia Regina Mwalekwa akiwa na Kibonde kwenye kipindi cha Jahazi ambacho awali ilikuwa Gadner na Kibonde. Anyway, wanajitahidi sana ila pengo la Gadner ni dhahiri na kwa kiasi fulani kipindi kimepoteza mvuto kama wakati wa Gadner.
Lakini pia Radio One imepoteza sana watangazaji mahiri ambao wamejiunga na Clouds ambao ni Regina Mwalekwa, Milad Ayo, Abdul Mohammed. Hawa wamejiunga na Michael Maluwe na Paul John ingawa sijasikia Clouds kupoteza Watangazaji kwenda Radio One.
Hili ni pigo kubwa sana kwa Wasikilizaji wa Kipndi cha Kiswahili kila Jumamosi ambacho Regina alikuwa ndiyo muandaaji. Vipindi vingine havijapata pigo kwani Vijana waliojiunga na Radio One kama vile Reuben Mchome na Anwar Mkama wanajitahidi. Hii ina ishara gani kwa Radio hizi mbili (Clouds na Radio One), ni kama kuna bifu fulani baina yao ambalo katika hilo wanaopoteza ni Radio One.